CCM na mamluki 14/12/2014

CCM na mamluki 14/12/2014

kailakarama

Member
Joined
Aug 30, 2014
Posts
73
Reaction score
30
Serikali ya CCM na mikakati ya ushindi wa uchaguzi watu serikali za mitaa tarehe 14/12/2014.

Ama kweli huu ni uchaguzi wa ndondo maana serikali ya CCM ndiyo inaamua na kupanga kila kitu.

Kwa kuwa wanajua hawakubaliki kwa wakazi wa mitaa husika wanatumia pesa kufanikisha ushindi wao.

Hatua ya kwanza
kuandikisha mamluki wa kutosha.
Utaratibu
1.Zitatumika form za kuandikisha wagombea zisizokuwa na sehemu ya namba za nyumba
2.kuwaacha watu wote waandikishwe kwa kisingizio cha kuwa ukimzuia utasababisha vurugu
3.kuwapa Imani wapinzani kuwa mapingamizi ya wapiga kura ambao siyo wakazi yatashughulikiwa kwa uwazi na uadilifu kumbe ni uongo.

Hatua ya pili
Kuwapa hela Shilingi elfu tano kwa kila mamluki wakati kuandikisha na hela watapewa wanapoenda kukabidhi namba na jina kwa kiongozi wa Tawi la CCM la mtaa atakayekuwa amepewa kazi hiyo maalum.

Hatua ya Tatu
Kuwasilisha mapingamizi
Utaratibu
1.kufuatilia Kwenye orodha ni watu kiasi gani wameandikwa na wa CCM uhakika ni wangapi wa vyama vingine wangapi na wasioeleweka wangapi
2.mapingamizi yote ni lazima aliyeweka pingamizi ndiyo athibitishe kuwa aliyemuwekea pingamizi siyo mkazi.
Jambo Hilo litakuwa gumu kwa sababu ya kukosekana namba za nyumba Kwenye orodha.
Na njia sahihi ilikuwa anayewekewa pingamizi ndiyo athibitishe kuwa yeye ni mkazi wa mtaa husika.
3.kuhakikisha mapingamizi yote dhidi ya mamluki yanashindwa kushughulikiwa.

Hatua ya nne
Siku ya kupiga kura
Kuwakumbusha namba zao mamluki na kuwalipa Shilingi elfu kumi baada ya kupiga kura.
 
Daah, jamani maccm yanatupeleka wapiiii, jamani jamani. Ngumu kumesa khaa!
 
Back
Top Bottom