CCM: Mwenyekiti na changamoto

CCM: Mwenyekiti na changamoto

Liganga

Senior Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
165
Reaction score
128
Baada ya muda mrefu sana wa kuwa pembeni nikitazama yanayojitokeza nimepata msukumo wa kutafakari kwa kina kazi iliyombele ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.

Nikiitazama hali hii nakumbuka miaka ya 1934 pale Adolf Hitler na chama chake walipokamata madaraka ya Ujerumani.

Katika vuguvugu la kuchukua madaraka pale Ujerumani, Adolf na kundi lake waliunda mtandao mpana ulionea nchi nzima wakitumia ushawishi, nguvu na shurutisho kupamabana na wapinzani wao pamoja na serikali iliyokuwa madarakani.

Baada ya kufanikiwa kuwa chansela haikupita mda mrefu Adolf kubaini alikuwa na kibarua kigumu kudhibiti nguvu ya mtandao aliounda kuhakikisha ushindi wake.

Moja ya changamoto alizakabiliana nazo ni kile kikundi cha Sturmabteilung (SA) kilichokuwa chini ya uongozi wa Ernst Röhm. Kundi hili lilikuwa ni kubwa ukilinganisha na mengine likifikia idadi ya wafuasi zaidi ya milioni tatu.

Bwana Ernst Röhm binafsi hakuwa anaridhishwa na utendaji wa Adolf akiamini kuwa malengo ya kukamata madaraka yalikuwa hayajatekelezwa kwa ukamilifu na aliamini kuwa kunahitajika mapinduzi mengine.

Adolf binafsi alikuwa anatambua nguvu kubwa ya Ernst Röhm and jeshi kubwa la wafuasi milioni tatu nyuma yake. Haikuchukua mda ugomvi kuibuka kati yao na Ernst Röhm kuanza kumpinga Adolf na hata kuwatumia watu wa pembeni lakin wenye nguvu na ushawishi katika Ujerumani kupingana na Adolf.

Mnamo mwezi Julai 1934 Adolf alipoona uhai wa chama cha Nazi unatishiwa ikiwemo nguvu ya serikali yake, alifanya safari ya ghafla alfajiri kuelekea Bad Wiessee akiwa ameambatana na kikosi chake cha intelijensia kilichofaamika kama Schutzstaffel (SS). Siku hiyo ndio ilianza oparesheni MAALUM ya kuwashugulikia viongozi wote wa SA waliokuwa mstari wa mbele wa kuuvuruga uongozi wa Nazi na serikali ya Adolf.

Oparesheni hii maalum ilifahamika kama "The Night of the Long Knives".

Wanajamvi nimeona niwaletee hii historia.

Hii ni wiki nzuri ya kutafakari namana m/kiti atakavyokabili changamoto mbalimbali hadi kufikia Jumapili.

Hii kazi pia kwa kiasi fulani inafanana na namana m/kiti wa wakati ule alivyokabiliana na changamoto za kumpata mrithi wa Karume mwaka 1972.

Kanali Seif Bakari alikuya ndiye mwenye nguvu, ndiye kipenz cha wengi, ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kutekeleza kwa vitendo sera za utawala wa hayati Abeid Karume.

M/kiti aliibuka na hoja nzito za kumkataa Kanali Bakari na kumpendekeza Alhaj Aboud Jumbe

Pia nguvu ya m/kiti kumudu changamoto ilijidhiirisha tena mwaka 1984, pale alipoitisha kikao cha dharura Dodoma kuchukua hatua dhidi ya yaliyokuwa yanajili Visiwani.

Pale Dodoma paliwaka moto, makundi mawili kutoka visiwani yakipambana, moja kumzamisha Alhaj Jumbe na lingine kuhakikisha anabaki imara.

Pamoja na kukosa urais mwaka 1972, Kanali Bakari alikuwa miongoni wa waliopambana kuhakikisha Jumbe haanguki.

M/kiti alifanikiwa kuendesha kikao kilichozimia kumvua mdaraka yote ndani ya serikali na chama alhaj Jumbe.

M/kiti hakuishia hapo, alihakikisha aliyekuwa m/sheria mkuu wa visiwan wakati ule, raia wa Ghana, anapewa notisi ya kuondoka nchini ndani ya masaa 24.

Waziri Kiongozi Ramadhani Haji yeye alipelekwa kizuizini.

Waziri wa Nchi Bw. Aboud Talib nae pia alitiwa kizuizini.

Aliyepata kuwa jaji mkuu, Bw. Dourado nae alitiwa kizuizini.

Kanali Bakari, mtetezi mkuu wa Alhaj pale Dodoma nae alielekezwa kizuizini

Hatimaye na Rais Aboud Jumbe nae alipelekwa kizuizini.

Hatua hizi zilichukuliwa ikiwa ni jitihada mahusus za kudhibiti na kuweka sawa hali ya hewa kule visiwani.

Jambo hili liliacha taswira ya upeo na nguvu ya m/kiti wa chama.

Kwa mara nyingine tena siasa za visiwani zilimpa m/kiti changamoto kwenye mbio za kumpata mrithi wake 1985.

Chama kilidhibit idadi ya wagombea kuwa WATATU tuu.

Wakipambana;
- Alhaji Hassan Mwinyi
- Bw. Rashid M. Kawawa
- Dk. Salim H. Salim

Vita ilikuwa ni kali pale mpambano ulipobaki kwa wawil tuu baada ya Bw. Kawawa kujitoa.

Rejea historia kujua kilichojiri, lakin m/kiti safari hii alishindwa aliyokusudia.

Nguvu ya kambi ya Mzee Talib, Mzee Natepe, Mzee Haji, Mzee Bomani na Bi Mongella iliibuka mshindi baada ya Alhaj H. Mwinyi kupata ushindi wa kuwa rais wa pili wa Tanzania.

Waliokuwa kikaoni wanaelewa kazi ilivyokuwa ngumu, ushawishi mkumbwa ulifanyika na hoja zilivyosukwa vyema.

Hoja kuu ikiwa kidemokrasi na kiuongozi si vyema kumwacha Alhaj Hassan Mwinye aliyekuwa rais wa visiwan na kumpitisha Dk. Salim aliyekuwa waziri mkuu kuwa rais wa pili wa Tanzania.

Kwa hoja ya mtiririko wa MAMLAKA na succession (kupeana vijiti) ilikuwa ni busara kuacha achukue Alhaj Mwinyi. Hapo m/kiti hakuwa na uwezo wa kupinga bali kukubali hoja hiyo.
 
Mhhh

Kwa mfumo wa sasa ulivyo, mwenyekiti hawezi kutumia SS kuwashughulukia SA?
 
Mfumo huu ni wa kipindi kile cha SA...Taifa bado ni changa.
 
mwenyekiti hata hana shida kama unavyofikiria ww..... yeye kazi yake ni kuongoza vikao na wanachama japo tareh 12/7 ni kupiga tu mhuri kwan kazi ilishaisha miaka 20 iliyopita
 
M/kiti anawajibika kuendesha kikao vyema na kuhakikisha maamuzi sahihi kwa mustakabali wa chama yanafikiwa.

Kila mjumbe anao uhuru wa kuchangia kwa kadiri ya agenda zilivyo lakini maamuzi ufikiwa na kuridhiwa na wajumbe wote.
 
mwenyekiti hata hana shida kama unavyofikiria ww..... yeye kazi yake ni kuongoza vikao na wanachama japo tareh 12/7 ni kupiga tu mhuri kwan kazi ilishaisha miaka 20 iliyopita
Kazi iliisha 2008 kama unanielewa lakini.
 
Kiongozi ni maono au kwa lugha nyepesi ni kuiona kesho kabla haijawadia na kisha kuwashawishi wenzio kuchonga njia kuelekea kule kiongozi anapoamini kuwa ni sahihi.

Haijalishi maamuzi yalifanyika mwaka gani, msingi ni je tupo kwenye njia sahihi? Je maamuzi hayo yanatupeleka kwenye ustawi zaidi kama Taifa na hata katika ngazi ya chama?
 
Ingawaje post yako imebeba uhalisia wa kiongozi, JK keshamaliza muda wake sanasana sasa hivi anafikiria legacy yake, itakuwaje huko baadae.

Hila katika kipindi hiki bado ana nafasi kama raisi na mwenyekiti wa chama kutakafakari sana hoja uliyoileta anataka atuwache vipi kuelekea mbele na anaionaje Tanzania ya kesho iwapo watu ambao sio sahihi ndio wanaoliongoza taifa hili je kunamategemeo yeyote ya kuwa na serikari bora na yenye kujenga maendeleo.

Make no mistake waliochota kipindi cha zamani walikuwa wachache na ilikuwa raisi kuwajua kutokana na nafasi zao za juu, ila kwa leo wachotaji ni wengi zaidi wametapakaa na wanachukua kingi zaidi kupita kipindi chochote cha uhuru wetu.

JK ingawa ana maliza muda wake keshaziona changamoto za kazi kutokuwa na mgombea wake aisadii lazima aone mtu ambaye ana mawazo na mbinu za kuweza kuzimudu changamoto zenyewe kwa faida ya watu millioni 50: rafiki, long terms associate sio kigezo, maslahi ya afya ya chama chao mpaka hapa alipokiacha kinaitaji kiongozi gani atakaeweza rudhisha utamaduni unaoheshimika na wenye kusimamiwa na kila mwanachama bila ya kusahau weledi wa kuisimamia na kuiongoza serikari iiyojaa wababaifu wengi wasio na maslahi ya wengi kwenye utendaji.

Kiongozi huyo lazima awe asiye na makundi na mwenye uwezo wa kumudu changamoto za taifa za kesho, JK lazima asimame na loyalty ya watu na afya ya chama chake ilikibaki miaka hamsini zaidi (atleast on their perspective) vinginevyo atakuwa ametukosea sana watanzania na pengine wanachama wenzake wa CCM wenye nia njema iwapo kiongozi ajaye atakuwa sio mtu sahihi kwa ustawi wa vyote viwili.

Mzee Mwinyi, Mkapa, Salmini Amour, JK na Jaji Warioba wakitafuniwa wasifu wa wagombea na fikra zao kwa pamoja wanaweza pata mmoja katika waliojitokeza kwa kujua changamoto za kazi ya uraisi.
 
Hii kazi pia kwa kiasi fulani inafanana na namana m/kiti wa wakati ule alivyokabiliana na changamoto za kumpata mrithi wa Karume mwaka 1972.

Kanali Seif Bakari alikuya ndiye mwenye nguvu, ndiye kipenz cha wengi, ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kutekeleza kwa vitendo sera za utawala wa hayati Abeid Karume.

M/kiti aliibuka na hoja nzito za kumkataa Kanali Bakari na kumpendekeza Alhaj Aboud Jumbe
 
Sifa moje kuu katika uteuzi wa Alhaj jumbe ilikuwa ni kutokuwa na MAKUNDI. Hekima za m/kiti ziliegemea hapa zaidi katika kuwashinda wajumbe wengine.

Wajumbe waliambiwa kumteau Kanali kumrithi Hayati Karume ingetafsiriwa kuwa mauaji yale yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi. Hakika wajumbe wote waliomtaka kanali walinywea.

Hii ndio huitwa kalama ya uongozi, m/kiti alipangua hoja za wajumbe kwa mstakabali sahihi wa nchi.
 
Pia nguvu ya m/kiti kumudu changamoto ilijidhiirisha tena mwaka 1984, pale alipoitisha kikao cha dharura Dodoma kuchukua hatua dhidi ya yaliyokuwa yanajili Visiwani.

Pale Dodoma paliwaka moto, makundi mawili kutoka visiwani yakipambana, moja kumzamisha Alhaj Jumbe na lingine kuhakikisha anabaki imara.

Pamoja na kukosa urais mwaka 1972, Kanali Bakari alikuwa miongoni wa waliopambana kuhakikisha Jumbe haanguki.

M/kiti alifanikiwa kuendesha kikao kilichozimia kumvua mdaraka yote ndani ya serikali na chama alhaj Jumbe.

M/kiti hakuishia hapo, alihakikisha aliyekuwa m/sheria mkuu wa visiwan wakati ule, raia wa Ghana, anapewa notisi ya kuondoka nchini ndani ya masaa 24.

Waziri Kiongozi Ramadhani Haji yeye alipelekwa kizuizini.

Waziri wa Nchi Bw. Aboud Talib nae pia alitiwa kizuizini.

Aliyepata kuwa jaji mkuu, Bw. Dourado nae alitiwa kizuizini.

Kanali Bakari, mtetezi mkuu wa Alhaj pale Dodoma nae alielekezwa kizuizini

Hatimaye na Rais Aboud Jumbe nae alipelekwa kizuizini.

Hatua hizi zilichukuliwa ikiwa ni jitihada mahusus za kudhibiti na kuweka sawa hali ya hewa kule visiwani.

Jambo hili liliacha taswira ya upeo na nguvu ya m/kiti wa chama.
 
Kwa mara nyingine tena siasa za visiwani zilimpa m/kiti changamoto kwenye mbio za kumpata mrithi wake 1985.

Chama kilidhibit idadi ya wagombea kuwa WATATU tuu.

Wakipambana;
- Alhaji Hassan Mwinyi
- Bw. Rashid M. Kawawa
- Dk. Salim H. Salim

Vita ilikuwa ni kali pale mpambano ulipobaki kwa wawil tuu baada ya Bw. Kawawa kujitoa.

Rejea historia kujua kilichojiri, lakin m/kiti safari hii alishindwa aliyokusudia.

Nguvu ya kambi ya Mzee Talib, Mzee Natepe, Mzee Haji, Mzee Bomani na Bi Mongella iliibuka mshindi baada ya Alhaj H. Mwinyi kupata ushindi wa kuwa rais wa pili wa Tanzania.

Waliokuwa kikaoni wanaelewa kazi ilivyokuwa ngumu, ushawishi mkumbwa ulifanyika na hoja zilivyosukwa vyema.

Hoja kuu ikiwa kidemokrasi na kiuongozi si vyema kumwacha Alhaj Hassan Mwinye aliyekuwa rais wa visiwan na kumpitisha Dk. Salim aliyekuwa waziri mkuu kuwa rais wa pili wa Tanzania.

Kwa hoja ya mtiririko wa MAMLAKA na succession (kupeana vijiti) ilikuwa ni busara kuacha achukue Alhaj Mwinyi. Hapo m/kiti hakuwa na uwezo wa kupinga bali kukubali hoja hiyo.
 
Kuna wanaoamini kuwa historia ina desturi ya kujirudia, japo si kwa asilimia mia
 
Imesomeka vizuri mkuu ila hii inatokea tu kama mlengwa anajitambua na ni muadirifu, inakuwa vigumu kuwacha mtu mwadirifu katika nafasi yoyote iwayo. Na pili, kama alivyowatahadharisha JK mara hii siasa zimebadirika sana, kwamba mgombea wa CCM ndo anakuwa rais tayari, kwasahiv mambo hayako hivyo tena. Sahivi mtatakiwa kumpata mtu aliye msafi na atakayeuzika kwa wepesi la sivyo mtakuwa mmekiweka chama chenu rehani, uzuri JK ni mwanasisa kwa hasiri yake na anaelewa na kuona ambacho wengi hamkioni lakini kama mtafata historia basi aliwaambia mjiandae kisaikolojia
 
Cha msingi zaidi ni maamuzi ambayo yanalenga kuhakikisha ustawi wa chama na taifa, maana kwa mwaka huu wa 2015 mzani bado upo sawa yeyote kati ya chama TAWALA na UKAWA anaweza kamata dola ikiwa mchezo utachezwa kwa haki bila kusiskiliiza matakwa ya wadhamini.
 
mkuu unaonekana uko smart sana upstairs.
endelea kutudadavulia hiyo historia iliyotukuka.

Pia nguvu ya m/kiti kumudu changamoto ilijidhiirisha tena mwaka 1984, pale alipoitisha kikao cha dharura Dodoma kuchukua hatua dhidi ya yaliyokuwa yanajili Visiwani.

Pale Dodoma paliwaka moto, makundi mawili kutoka visiwani yakipambana, moja kumzamisha Alhaj Jumbe na lingine kuhakikisha anabaki imara.

Pamoja na kukosa urais mwaka 1972, Kanali Bakari alikuwa miongoni wa waliopambana kuhakikisha Jumbe haanguki.

M/kiti alifanikiwa kuendesha kikao kilichozimia kumvua mdaraka yote ndani ya serikali na chama alhaj Jumbe.

M/kiti hakuishia hapo, alihakikisha aliyekuwa m/sheria mkuu wa visiwan wakati ule, raia wa Ghana, anapewa notisi ya kuondoka nchini ndani ya masaa 24.

Waziri Kiongozi Ramadhani Haji yeye alipelekwa kizuizini.

Waziri wa Nchi Bw. Aboud Talib nae pia alitiwa kizuizini.

Aliyepata kuwa jaji mkuu, Bw. Dourado nae alitiwa kizuizini.

Kanali Bakari, mtetezi mkuu wa Alhaj pale Dodoma nae alielekezwa kizuizini

Hatimaye na Rais Aboud Jumbe nae alipelekwa kizuizini.

Hatua hizi zilichukuliwa ikiwa ni jitihada mahusus za kudhibiti na kuweka sawa hali ya hewa kule visiwani.

Jambo hili liliacha taswira ya upeo na nguvu ya m/kiti wa chama.
 
Je, m/kiti amecheza vema?

Je, m/kiti ameweka msingi wa kukivusha chama na kukielekeza kwenye ustawi?
 
Tusisahau katika kufikia maamuzi, uongozi unaweza kupata ushauri toka idara ya Usalama wa Taifa. Hawa wanajua nani ji nani na kafanya nini.
CC kwa wakati huu, itafanya maamuzi pia kwa kutumia taarifa ya kamati ya maadili.
Kazi ya Mwenyekiti ni kuwashawishi wajumbe kutopuuza usalama wa taifa na kamati ya maadili. Ni vyombo ambayo kwa namna moja ana vi influence sana.
Maana yake kwa kifupi, atakalo mwenyekiti, ndiyo litakuwa!
 
Back
Top Bottom