CCM Mwanza kumwonjesha Kikwete Shubiri

CCM Mwanza kumwonjesha Kikwete Shubiri

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
1,025
Reaction score
475
CCM Mwanza kumwonjesha Kikwete Shubiri

Makada wa CCM wamo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha wanaonyesha chukizo lao kwa Mwenyekiti wa Chama hicho kutokana na madai ya kuwapuuza kwa muda mrefu kutekeleza mapendekezo yao yanayolenga katika kukijenga chama.

Moja ya pendekezo la makada hao ni kuhusu mchakato wa uteuzi wa wakuu wa wilaya ambao wao walimshauri Mwenyekiti wao kuweka viongozi wenye sifa na uwezo wa kutumikia wananchi na si nafasi za kirafiki na kulipa hisani.

Wanasema wanasikitishwa mno na mwenendo mzima wa kiongozi huyo ambao unaonekana kama ni kulipa kisasi kwa kuwa upinzani ulitwaa viti katika wilaya nyingi za mkoa wa Mwanza.Mmoja wa Makada hao (jina limehifadhiwa) kanukuliwa akisema ‘’ kama ni kisasi sasa hiki kimezidi maana haiwezekani unachagua wakuu wa wilaya wapya sabini hakuna hata mmoja anayetoka mwanza, uwiano uko wapi hapa.

Hivi ni kweli kabisa katika watendaji na makada wa chama waliopo hapa Mza, hakuna hata mmoja analiye na uwezo wa kuwa Mkuu wa wilaya?’’ kamaliza kwa kuhoji kada huyo.

Makada hao wenye nguvu na ushawishi mkubwa walikuwa katika kikao ambacho lengo lao ni kuhakikisha wanaweka umoja na kusambaza ujumbe wao wa SAY NO 2 CCM.

Mpango wa awali ni kuhakikisha hawachukui fomu wala kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi ujao wa CCM.Wanabainisha kuwa hakuna shaka yoyote CCM itakayosalia baada ya utawala huu itakuwa imemeguka mapande ya kutosha tu ambayo bila shaka hayatakuwa na nguvu yoyote ya kuhimili nguvu ya Upinzani.

Wametolea mfano sakata la sasa la huko Tarime ambapo madiwani wote wamemsusia Mkuu wa Wilaya na wamesema hawatashiriki kikao chochote mpaka mkuu huyo wa wilaya aondoshwe katika nafasi hiyo.

Huu unaonekana kuwa mwanzo wa anguko la jumla la CCM katika eneo la ukanda wa Ziwa kutokana na kukinzana huko kwa masilahi kunakodaiwa kukumbatiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.

Agenda iliyopo mezani kwa sasa ni kuweka mazingira yatakayoipa uwezo nguvu yao ambayo wameilezea kuwa imejikita zaidi kwa mashabiki wa chama hicho ambao wote wanaonyesha kukatishwa tama na kwa namna ambavyo Mwenyekiti wao wa Taifa amekuwa akipuza mapendekezo lukuki ya Makada hao wa Mwanza.

ADIOS


Angalizo:


Mada hii ishachangiwa na nimeipost kwa ajili ya kuweka kumbukumbu zetu sawa hapa JF maana hata katika account ya GR haipo kama latest thread started, nahisi ni kutokana na tatizo la server ambalo sina shaka litakuwa limeathiri watumiaji wengi wa JF.

Ukijisikia kama una hoja ya ziada bado unaweza kuchangia.

Nilipoisaka kupitia google na baadaye kulink JF nilipata ujumbe kama inavyoonekana hapa chini. Mkuu INVISSIBLE litazame hili:

JamiiForums Message
GHOST RYDER, you do not have permission to access this page. This could be due to one of several reasons:
1. Your user account may not have sufficient privileges to access this page. Are you trying to edit someone else's post, access administrative features or some other privileged system?
2. If you are trying to post, your account may be awaiting activation (if already registered).
CCM Mwanza kumwonjesha Kikwete shubiri
www.jamiiforums.com › ... › Jukwaa la SiasaCached - Translate this page
You +1'd this publicly. Undo
26 posts - 17 authors - 4 days ago
CCM Mwanza kumwonjesha Kikwete Shubiri Wakati ambapo vikao vya NEC huko Dodoma vinatarajiwa kuwaadabisha baadhi ya makada wa ...
Get more discussion results



 
Yaani wakuu wa wilaya70 hakuna hata mmoja atokaye mkoani mwanza???????????? Kama ni visasi hivi ni too much, mpaka nataka niamini story kwamba Babu Seya yupo Jela maisha kwasababu alimkanyagia sehemu.:A S 103::A S 103::A S 103::A S 103:
 
Yaani wakuu wa wilaya70 hakuna hata mmoja atokaye mkoani mwanza???????????? Kama ni visasi hivi ni too much, mpaka nataka niamini story kwamba Babu Seya yupo Jela maisha kwasababu alimkanyagia sehemu.:A S 103::A S 103::A S 103::A S 103:

Mkuu babu seya alikuwa anapiga demu ambaye mkulu alikuwa anakula. Huyo demu alikuwa na mume wake (alikuwa na ndoa yake). Mkulu alivyokuwa na roho ya korosho, ilimuuma sana utafikili nae alikuwa aibi kwa huyo demu. In short wote (mkulu na babu seya) walikuwa wanaiba. Baada ya mkulu kuingiwa nyongo, ndiyo babu seya yakamkuta yaliyomkuta. In short mkulu ni mtu wa visasa sana...
 
Kwani ccm ni baba yenu? kwanza mmebaki nyiye tu, mwanza nzima ni upinzani na mwenyekiti wenu analijua hilo na ndiyo maana hakuchagua mtu wa mwanza. jiwekeni wazi.
 
Kuna costa J. Kanyasu anatokea mwanza ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Ngara, Duh! ccm ondoeni vyeo vya kupeana ulaji kama wakuu wa wilaya, mtamalizana! sisi yetu macho
 
mimi kama kada wa ccm mbona nape hajibu hoja sikuhizi ana nikatisha tamaa kijana wake alafu tangazo kwa wanachama wenzangu wa ccm blog yetu imefunguliwa tuitembelee basi tutoa maoni yetu kule tuwaachieni jamii forum yenu.
 
mimi kama kada wa ccm mbona nape hajibu hoja sikuhizi ana nikatisha tamaa kijana wake alafu tangazo kwa wanachama wenzangu wa ccm blog yetu imefunguliwa tuitembelee basi tutoa maoni yetu kule tuwaachieni jamii forum yenu.

Hiyo blog ya ccm haina kijana humu JF wote humu ni CDM so,,,blog ikikosa wateja kinachofuatia ni kufungwa,,kweli ccm kazi mnayo kila mkianzisha hakipati mshirika,,hata gazeti lenu la UHURU siku hizi linanunuliwa na makada wa ccm tuu,,emu angalia gazeti kama,TZ daima, mwananchi, Nipashe jinsi yanavyonunuliwa yani yanatoka asubuhi na ikifika saa 6 mchana huwezi kuyapa...kazi mnayo ccm.
 
Back
Top Bottom