Salvatory Mkami
Senior Member
- Apr 17, 2013
- 146
- 245
Katika kipindi hiki ambacho taifa linaingia katika hatua muhimu kabisa ya kikatiba kwa maana ya Uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani nimejaribu kutafakari sana kama kweli bado Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake (Chama Dola) kinaweza kujitutumua kusimama na kujinadi majukwaani kutaka kupewa tena ridhaa ya kuendelea kuwatumikia wananchi ambao kwa sasa ni kama wamekata tamaa kutokana na kuchoshwa na uongozi mbovu wa serikali ya chama hicho ambao licha ya kushindwa wameenda mbali na kuonyesha dharau wananchi ambao ndio haohao wanaowategemea wawapigie kura ili waweze kurudi madarakani nikaona sio vibaya iwapo nitashiriki nanyi maswali haya machache kati ya milioni yanayoweza kuulizwa:
1. Ni kwanini viongozi wa ngazi za juu wa CCM ambao tulitegemea wawe mfano bora na wa kuigwa kwa jamii wawadharau na kuwatusi Watanzania hususani wale wanaounga mkono upinzani (UKAWA) kwamba ni Vibaka, wanywa Viroba na wamenunuliwa kisa tu wametumia haki yao ya kikatiba kujitokeza kumdhamini na kumshabikia mgombea wao wa urais wanayempenda?
2. Twiga alifikishwa vipi uwanja wa ndege (airport) na kupakizwa kwenye ndege pasipo vyombo vya ulinzi na usalama kubaini usafirishaji huo batili wa nyara za serikali?
3. Mwenyekiti wa Chama chenu na ambaye ni rais wa Tanzania alisema kwa uhakika kabisa kwamba anayo majina ya viongozi wa dini na vigogo wauza unga (madawa ya kulevya), Je yeye na serikali ya chama chake (CCM) wamewachukulia hatua gani wahusika?
4. Wale waliorudisha pesa za EPA walirudisha Tsh ngapi? Na je, wale waliokataa kurudisha wamechukuliwa hatua gani?
5. Pembe za ndovu zinapita vipi katika uwanja wetu wa ndege mpaka nje ya nchi hata kukamatwa na vyombo vya usalama vya nchi nyingine? Kuna kigogo wa ngazi ya juu katika chama kimoja maarufu ambaye amekuwa akituhumiwa katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari kujihusisha na biashara haramu ya pembe za ndovu je, Serikali ya CCM imewahi kufuatilia tuhuma hizo au hazina mashiko?
6. Swala la Escrow limeishia wapi? Na je, ni kigezo gani kilichotumiwa na CCM kuwapitisha Prof. Anna Tibaijuja, Andrew Chenge na Joseph Ngeleja kugombea Ubunge katika majimbo yao licha ya kuwa na tuhuma za ufiswadi ambazo ziliwakabili miezi michache iliyopita?
7. Swala La Richmond likoje? Awali tuliaminishwa na wapinzani kwamba Mhe. Edward Lowassa ndiye kinara na mhusika mkuu katika sakata hilo na kutokana na ushahidi wa kimazingira tuliamini hivyo lakini Majuzi baada ya Mhe. Edward Lowassa kuhamia upinzani aliamua kutoa ya moyonu na kusema wazi kwa vyombo vya habari kwamba yeye alitaka kuvunjwa kwa Mkataba wa Richmond lakini mamlaka ya Juu (rais) ilikataa na kushinikiza mkataba huo upitishwe" Mpaka muda huu ninapoandika waraka huu hakuna yeyote ndani ya Serikali wala CCM aliyejitokeza na kupinga tuhuma hizo je, tuendelee kuamini kwamba tuhuma Mhe. Lowasa alizozitoa zilikuwa ni za kweli na ndio sababu ya kutokanushwa?
8. Je, kwa hali ya maisha ilivyo ngumu kwa gharama za maisha kupanda na uchumi wa nchi kudorora ndio tuseme hali hiyo inasadifu ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania?
9. Ni kwanini Rasimu ya Katiba ya iliyokuwa Tume ya Katiba Chini ya Mhe. Jaji Joseph Warioba ilichakachuliwa kinyume na matakwa ya wananchi huku wajumbe wote waliobariki uchakachuaji wa rasimu hiyo wakiwa ni wa CCM?
10. Kitambulisho cha kupigia kura ni mali ya mpiga kura, iweje watumishi wa vyombo vya usalama (Mf. Polisi) waamriwe waviwakilishe vitambulisho hivyo katika sehemu zao za kazi ili utawala uchukue taarifa za vitambulisho hivyo? Je lengo ni lipi haswa?
11. Suala la uhakiki wa majina na vitambulisho vya wapiga kura lina utata gani? Nini kinasubiriwa ilihali uandikishaji wa daftari la wapiga kura umemalizika nchi nzima? Au Tume inasubiri muda uishe watuambie uhakiki hauwezi kufanyika?Haya ni baadhi tu ya maswali machache kati ya milioni yanayoweza kuulizwa ambayo iwapo yatatoa majibu kuntu ya maswali hayo ushindi katika uchaguzi mkuu 2015 ni wa CCM, lakini iwapo yatakosa majibu ni wazi kwamba hakutakuwa na haja kwa wananchi kukichagua chama hicho ambacho kimeamua kwa dhati kuendelea kuwadanganya, kuwadharau na kuwatusi Watanzania.
Haya ni baadhi tu ya maswali machache kati ya milioni yanayoweza kuulizwa ambayo iwapo yatatoa majibu kuntu ya maswali hayo ushindi katika uchaguzi mkuu 2015 ni wa CCM, lakini iwapo yatakosa majibu ni wazi kwamba hakutakuwa na haja kwa wananchi kukichagua chama hicho ambacho kimeamua kwa dhati kuendelea kuwadanganya, kuwadharau na kuwatusi Watanzania.