Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,205
- 25,535
Kadiri ninavyoyafuatilia mambo ya kisiasa, siasa ina mambo ya raha na karaha. Kama mambo mengi yako vyema ndani ya chama, viongozi na wanachama wa chama husika huwa na raha isiyo na kifani. Raha hiyo huwa karaha kwa chama au vyama pinzani kwa chama husika. Kunapotokea nafasi ya 'kuchochea moto' ndani ya chama kimojawapo, kazi hiyo hufanywa kwa furaha kubwa na chama pinzani na kuwa karaha kuu kwa chama husika. Hizo ndizo raha za kisiasa.
Wakati wa sakata la Zitto Kabwe Ruyagwa na wenzake ndani ya CHADEMA, watetezi wao wakubwa walikuwa ni wanachama na mashabiki wa CCM. Wanachama na mashabiki hao walikuwa na raha isiyo kifani kumtetea Zitto na wenzake katika kile kilichoonekana kama kuchochea moto ndani ya CHADEMA na hivyo kukinyima pumzi ya kupumzika chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Kwa CHADEMA, utetezi huo ulikuwa karaha.Wakati CUF ikiendelea kuchemka kwa migogoro, ni raha kwa wapinzani wa CUF kuona moto waendelea kuwaka.
Hainishangazi kuwaona wanachama na mashabiki wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wakijichora kama watetezi na wanaomuunga mkono Ndugu Benard Membe. Raha ya watetezi na waunga mkono hao ni kuona kuna mabishano, malumbano na mtifuano ndani ya CCM huku wao wakiendelea kuchochea kuni Zaidi. Kisiasa, si kwamba watetezi na waunga mkono wa Membe wanamkubali na kuwa naye kweli, ila wanaburudika kuona na kusikia ndani ya CCM kuna mjadala wa mabishano na kukosa maelewano.
Kimsingi, kuchochea kuni kwenye chama kingine ni mojawapo ya raha kubwa za kisiasa kwa wanasiasa. Kila anayeonekana kupingwa au kuzungumzwa kwa namna ya kushughulikiwa kwenye chama chake huzoa watetezi na wanamuunga mkono ambao wengi wao kama si wote ni bandia. Wao wanafaidi tu wanapoona kuna moto ukiwaka kwenye nyumba husika. Na mambo haya huwa ya zamu kwa zamu. Huhama kutoka chama kimoja hadi kingine. Kwahiyo, wanachama na mashabiki wa CCM msikereke. Hata nyinyi mlifurahi kwa muda wenu!