CCM msikereke , raha hii ya kisiasa ni zamu kwa zamu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,198
25,517
Kadiri ninavyoyafuatilia mambo ya kisiasa, siasa ina mambo ya raha na karaha. Kama mambo mengi yako vyema ndani ya chama, viongozi na wanachama wa chama husika huwa na raha isiyo na kifani. Raha hiyo huwa karaha kwa chama au vyama pinzani kwa chama husika. Kunapotokea nafasi ya 'kuchochea moto' ndani ya chama kimojawapo, kazi hiyo hufanywa kwa furaha kubwa na chama pinzani na kuwa karaha kuu kwa chama husika. Hizo ndizo raha za kisiasa.

Wakati wa sakata la Zitto Kabwe Ruyagwa na wenzake ndani ya CHADEMA, watetezi wao wakubwa walikuwa ni wanachama na mashabiki wa CCM. Wanachama na mashabiki hao walikuwa na raha isiyo kifani kumtetea Zitto na wenzake katika kile kilichoonekana kama kuchochea moto ndani ya CHADEMA na hivyo kukinyima pumzi ya kupumzika chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Kwa CHADEMA, utetezi huo ulikuwa karaha.Wakati CUF ikiendelea kuchemka kwa migogoro, ni raha kwa wapinzani wa CUF kuona moto waendelea kuwaka.

Hainishangazi kuwaona wanachama na mashabiki wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wakijichora kama watetezi na wanaomuunga mkono Ndugu Benard Membe. Raha ya watetezi na waunga mkono hao ni kuona kuna mabishano, malumbano na mtifuano ndani ya CCM huku wao wakiendelea kuchochea kuni Zaidi. Kisiasa, si kwamba watetezi na waunga mkono wa Membe wanamkubali na kuwa naye kweli, ila wanaburudika kuona na kusikia ndani ya CCM kuna mjadala wa mabishano na kukosa maelewano.

Kimsingi, kuchochea kuni kwenye chama kingine ni mojawapo ya raha kubwa za kisiasa kwa wanasiasa. Kila anayeonekana kupingwa au kuzungumzwa kwa namna ya kushughulikiwa kwenye chama chake huzoa watetezi na wanamuunga mkono ambao wengi wao kama si wote ni bandia. Wao wanafaidi tu wanapoona kuna moto ukiwaka kwenye nyumba husika. Na mambo haya huwa ya zamu kwa zamu. Huhama kutoka chama kimoja hadi kingine. Kwahiyo, wanachama na mashabiki wa CCM msikereke. Hata nyinyi mlifurahi kwa muda wenu!
 
Kimsingi, kuchochea kuni kwenye chama kingine ni mojawapo ya raha kubwa za kisiasa kwa wanasiasa. Kila anayeonekana kupingwa au kuzungumzwa kwa namna ya kushughulikiwa kwenye chama chake huzoa watetezi na wanamuunga mkono ambao wengi wao kama si wote ni bandia. Wao wanafaidi tu wanapoona kuna moto ukiwaka kwenye nyumba husika. Na mambo haya huwa ya zamu kwa zamu. Huhama kutoka chama kimoja hadi kingine. Kwahiyo, wanachama na mashabikiwa CCM msikereke. Hata nyinyi mlifurahi kwa muda wenu!
IMG-20181207-WA0010.jpg
 
Ila nadhan wale wapiga kelele wakijinadi kuwa wenyew watetezi wa rais ndo wameyakuza haya mbona ilikuwa game ya kuicheza kimya kimya na yangeisha haya bila kuonesha mtifuano uliomo ndani na kuwapa wapinzan cha kusema
 
Watu hawajua hili ni gemu la CCM, ila makamanda wamsahau mwenzao aendelee kunyea debe.
Lets hope by February/March atatoka.
 
Mtoa hoja hauko sahihi; wanaochochea kuni kwenye sakata la BM ni wana CCM kindakindaki, wafia chama.

haiwezekani mtu atoke chama B ndani ya wiki moja apite chujio la chama chetu bila kupingwa, ndani ya wiki mbili zingine Mbunge; ndani ya wiki mbili zingine Waziri....sisi wafia chama tupo tu tunakodia macho - aaaaahhh
 
kuna dhambi nyingi sana inawatesa ccm yakwanza ni wasiojulikana yapili visasi ya tatu wizi wa kura nanyingine mingi sana
 
Kadiri ninavyoyafuatilia mambo ya kisiasa, siasa ina mambo ya raha na karaha. Kama mambo mengi yako vyema ndani ya chama, viongozi na wanachama wa chama husika huwa na raha isiyo na kifani. Raha hiyo huwa karaha kwa chama au vyama pinzani kwa chama husika. Kunapotokea nafasi ya 'kuchochea moto' ndani ya chama kimojawapo, kazi hiyo hufanywa kwa furaha kubwa na chama pinzani na kuwa karaha kuu kwa chama husika. Hizo ndizo raha za kisiasa.

Wakati wa sakata la Zitto Kabwe Ruyagwa na wenzake ndani ya CHADEMA, watetezi wao wakubwa walikuwa ni wanachama na mashabiki wa CCM. Wanachama na mashabiki hao walikuwa na raha isiyo kifani kumtetea Zitto na wenzake katika kile kilichoonekana kama kuchochea moto ndani ya CHADEMA na hivyo kukinyima pumzi ya kupumzika chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Kwa CHADEMA, utetezi huo ulikuwa karaha.Wakati CUF ikiendelea kuchemka kwa migogoro, ni raha kwa wapinzani wa CUF kuona moto waendelea kuwaka.

Hainishangazi kuwaona wanachama na mashabiki wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wakijichora kama watetezi na wanaomuunga mkono Ndugu Benard Membe. Raha ya watetezi na waunga mkono hao ni kuona kuna mabishano, malumbano na mtifuano ndani ya CCM huku wao wakiendelea kuchochea kuni Zaidi. Kisiasa, si kwamba watetezi na waunga mkono wa Membe wanamkubali na kuwa naye kweli, ila wanaburudika kuona na kusikia ndani ya CCM kuna mjadala wa mabishano na kukosa maelewano.

Kimsingi, kuchochea kuni kwenye chama kingine ni mojawapo ya raha kubwa za kisiasa kwa wanasiasa. Kila anayeonekana kupingwa au kuzungumzwa kwa namna ya kushughulikiwa kwenye chama chake huzoa watetezi na wanamuunga mkono ambao wengi wao kama si wote ni bandia. Wao wanafaidi tu wanapoona kuna moto ukiwaka kwenye nyumba husika. Na mambo haya huwa ya zamu kwa zamu. Huhama kutoka chama kimoja hadi kingine. Kwahiyo, wanachama na mashabiki wa CCM msikereke. Hata nyinyi mlifurahi kwa muda wenu!
Ukweli mtupu kama.hapa nina furaha sana kuona maccm yanatifuana, hata wakatane mapanga sisi kwetu kicheko tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom