ifweero unasema katiba hii lazima ipite, una maana gani wakati wananchi hawajapiga kura ya maoni?Katiba hii ni ya wananchi. Lazima ipigiwe kura ya ndio ipite
Kwako wewe katiba nzuri eti mpaka iwe na serikali tatu ukawa ujuha huu sijui mtafika nao wapi.
Umeshajiuliza na UKAWA kwanini wanasema katiba hii si nzuri na kuwaambia wananchi wapige kura ya hapana?
Kwahiyo wewe unataka nini,usitumie neno wazanzibar tena koma kabisa sema wewe na chagadema yako hakuna mzanzibar anayepinga katiba inayopendekezwa ukiacha malimu sefu ambaye ni wakala wa sultani wengi wote wanaiunga mkono katiba.
Katiba hii ni ya wananchi. Lazima ipigiwe kura ya ndio ipite
Mkuu ungependa uletewe wapi hiyo katiba mbona watu wenye nia nayo karibu wote wanayo unataka ine nyumbani kwako ukiwa umekaa sebuleni au unatakaje,kwahiyo kwako wewe katiba isipogawiwa ndiyo inakuwa mbovu watu wengine kazi kweli.
Kwahiyo wewe unataka nini,usitumie neno wazanzibar tena koma kabisa sema wewe na chagadema yako hakuna mzanzibar anayepinga katiba inayopendekezwa ukiacha malimu sefu ambaye ni wakala wa sultani wengi wote wanaiunga mkono katiba.
Uliishia darasa la ngapi? Au ushabiki maandazi umekufilisi akili kiasi hicho? Pole sana
Kwa kua imeacha maoni yetu wananchi yaliyokuwemo ktk rasimu ya 2 iliyowasilishwa BMK
Na BMK ilikuwa ni wawakilishi wa wananchi.
Kama mlitaka maoni ndio yawe katiba kwanini mlikubali liwepo Bunge Maalum La Katiba?
Na hiy Katiba si inarudishwa kwa wananchi kupigiwa kura? kama huitaki si unasema hapana na wanayoittaka wanasema ndiyo! wakishinda wa hapana itakuwa hakuna katiba mpya mpaka iandikwe upya na wakishinda wa ndiyo, hapo ndiyo hauna ujanja uliyesema hapana, kwani demokrasia ndivyo ilivyo, wengi wape wachache wasikilize.
Katiba hii ni ya wananchi. Lazima ipigiwe kura ya ndio ipite
Katiba hii ni ya wananchi. Lazima ipigiwe kura ya ndio ipite
Ufanyike mkakati maalum wa kuisambaza upya rasimu ya Warioba .Wao wailete tuisome,na wajue tunajua namna ya kuisoma.
Tunachukua ile tuliyomuambia waryoba aandike tunaiweka mkono wa kulia,alafu na hiyo ya sasa mkono wa kushoto,alafu kalamu mkononi tunaanza ku cross read,kifungu kwa kifungu penye tofauti tunarudi kwenye randama ambazo zitakuwa mbele yetu.tunaangalia basis ya mabadiriko kama namna tulivyopendekeza.
.
Jibu hoja acha kutokwa povu!
1. 50/50 hata kama wanawake wenye sifa hawatoshi tutawapa hawara zetu wanaojua kusoma na kuandika1.asilimia 50 ya wanawake na wanaume ktk madaraka hususan ktk siasa
2. haki za wakulima,wafugaji kutambuliwa rasmi kikatiba hatua itakayosaidia kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji na kuwawezesha kupata mikopo na kuboresha kilimo na ufugaji wao.
3. rais wa zanzibar kuwa makam wa rais hatua itakayoimarisha muungano mara dufu
4.uhuru wa vyombo vya habari kutambuliwa rasmi kisheria na zaidi haki za wasanii
Mama shikamoo,naomba unisaidie kitu kimoja, unaweza kutuwekea majina ya BMk wote idadi na majina yao hapa kabla ya bunge kuanza tena ukiweza utenge wale wa bara na znz? Inaonekana watz hawajui hesabu ndio maana hata akidi inawachanganya, upigwaji wa hiyo kura huko kwa wananchi utasimamiwa na tume ya aina gani? Na hiyo tume itatumia mfumo uleule wa S. 6 kupata matokeo? Yaani kura ya hapana ikishinda itaundwa kamati ya maridhiano na wananchi wa hapana ama kura ya ndio itajaziwa na marehemu wa nchi hii akiwepo baba wa taifa? Je watakaopiga kura ya hapana mtawapa adhabu gani maana AG wa znz mmefukuza kazi, je wananchi wa kura ya hapana mtawafukuza nchini ama adhabu gani?
Kwa umri wako nategemea utaweza kutetea vifungu vyenye utata, eti ni kweli katiba hii imewajali sana wananchi kama wakulima, wafugaji, wasanii nk lakini hawatakuwa na nguvu ya kuwawajibisha viongozi kupata haki hizo? Hii 50/50 kwenye uwakilishi ina tija sana? Na mpaka sasa hivi hatujafikia 50/50 kwa sababu katiba ya zamani iliweka 80% wanaume na wanawake 20%? Je tukisema mliojipa wajibu wa kuandika katiba mlibeba jukumu kwa hila na msiloliweza tutakuwa tunakosea? Mama wewe nakuaminia utaweza kujibu maswali yangu maana hao waliokuwa wajumbe wa BMK hatuwaoni wakitoa ufafanuzi zaidi ya kusema hii ni katiba ya wananchi ipigiwe kura ya ndio.