CCM Mnaogopa NINI!!!??

CCM Mnaogopa NINI!!!??

donniebrasco

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
887
Reaction score
775
Kwa yote ambao serikali hii inajitahidi kufanya ( ionekane nzuri ) inasikitisha sana kuona wanatumia nguvu nyingi sana kukandamiza upinzani hii inatupa picha kuwa hawajiamini kabisa na wanayoyafanya na pia wanajua kiukweli kabisa wakiwapa fair chance upinzani basi watakuwa wamekwisha upinzani watachukua nchi mapema....

Lakini hata pamoja na haya wanayoyafanya sisi wananchi tumetulia tunasubiri viwanda vikamilike tutavihesabu 2020.

Na matukio yote tunarekodi tunaahidi kuwapa kura UKAWA maanake nyie mmeichoka Nchi Hii.

Halafu haihitaji akili hata ya sekondari kujua kuwa hawa jamaa wanahatarisha amani ya nchi.

Siasa ndio maisha...
Siasa ndio uchumi...
Siasa ndio afya...
Siasa ndio michezo...
Siasa ndio ubunge...
Siasa ndio urais...

Sasa kauli hii kuwa "sasa sio muda wa SIASA..." kweli WATANZANIA TUWE SERIOUS NA NCHI YETU KUANZIA KWENYE FAMILIA ZETU MPAKA VIJIJINI KWA MABABU ZETU WOTE TUELIMISHANE TU TUTAFIKA KIPINDI HIKI TUNA SILAHA KUBWA YA MAWASILIANO NAAMINI KIDOGO HUMU TUNAJITAMBUA TUSIKATE TAMAA JAPO WAPO WACHACHE WANATUHARIBIA MIJADALA ( WENGINE WANAUSALAMA WAMETUMWA KUITETEA SERIKALI HUMU)
 
Kinachokera zaidi hata upinzani nao hauko serious, kama tungekua na wapinzani walio serious nina hakika 2020 tungeweza kumuondoa huyu dikteta uchwara.

Tatizo upinzani wenyewe haueleweki upo haupo, ukiangalia vizuri ni upinzani maslahi, kama ccm B, kama wachumia tumbo.

Nothing is easier than blaming others for your own problems
 
Mleta uzi, umeandika vema. Na haiwezekani boya mmoja aseme upinzani ni dhaifu wakati hakuna uwanja huru wa kupiga siasa. CCM ni waoga tu. Mfano mdogo ni kuhusu Lowassa. Hivi karibuni bwana Poleharaka alisema hawamuhofii. Ila ukiwa na macho "manene" na ukimuangalia kwa umakini ni kiumbe anayemuhofia sana Lowassa kisiasa.
 
Kwa kinachoendelea Arumeru utasema upinzani uko serious?
Inakera sana hii kitu

Nothing is easier than blaming others for your own problems
 
Kwa kinachoendelea Arumeru utasema upinzani uko serious?
Inakera sana hii kitu

Nothing is easier than blaming others for your own problems
Mkuu, ule uhuni wa wale zumbukuku waliojiuzulu hauwezi kuufanya upinzani wote ukawa wa hovyo. Wale ni mababa majitu mazima. Yanajua (ndani kabisa mioyoni mwao) yanachokifanya. Ukipoteza muda kuwatafakari tutakuletea aspirin!
 
Kwa hiyo wanapojiuzuru we unachukulia sio chama tena badala yake ni watu binafsi?
Wangekua wamefanya mazuri ungesema ni watu binafsi au ungesema ni chama?
Mbona Magufuli hua tunamponda kwa kusema ni ccm in general? Akikosea Magufuli utakubali tuseme ni mtu binafsi na sio ccm? Uwe makini.
Tumuombe Mungu tupate wapinzani makini.

Nothing is easier than blaming others for your own problems
 
Kwa hiyo wanapojiuzuru we unachukulia sio chama tena badala yake ni watu binafsi?
Wangekua wamefanya mazuri ungesema ni watu binafsi au ungesema ni chama?
Mbona Magufuli hua tunamponda kwa kusema ni ccm in general? Akikosea Magufuli utakubali tuseme ni mtu binafsi na sio ccm? Uwe makini.
Tumuombe Mungu tupate wapinzani makini.

Nothing is easier than blaming others for your own problems
Hahahahaaa! Siyo kila jambo uliwekee mtiririko kadiri unavyoona. Lengo la wao kujiuzulu (kushawishiwa kimazingira) ni kutaka kuonesha kule upinzani ni kichaka kinukacho mkojo. Nami naamini lengo lao, kama ilivyopangwa, linakaribia kutimia. Hata weye unaingia mkenge. Siasa za dunia hii zimejaa ujanjaujanja, fitna, husda, propaganda na mengine kadha wa kadha.
Sasa basi, usipokuwa makini utaingizwa chaka hadi uimbe hallelujah! Hivi kwa akili ya kawaida, weye unadhani CCM wanafurahia wanavyoburuzwa na UKAWA kule kaskazini? Basi, ndiyo maana wamepiga kambi kule kupambana nao. Sikulazimishi kuamini hayo ila nenda zaidi ya uyaonayo kwa macho.
 
Ukiona hivyo ujue ushindi ulikuwa wa bao la mkono.
Mtu aliyeshinda kihalali huwa hateteleki hata siku mmoja.
Soma historia ya ADOLF HITLER ndiyo ujue sifa za madikiteta. Madikiteta wote huwa hawajiamini
 
hofu lazima mkuu, wakijiamini 2020 wanachomoka asubuhi tu kabla ya misa ya pili
 
Ni aibu,ni fedheha,ni kero tena ni karaha mwanaume kulialia kama mtoto mdogo kila siku,aaargh!jamani tumewachoka. Unaonewa vipi wakati una macho?si uone tu? Unakandamizwa kwani wewe mwanamke!fair play gani kati ya tembo na swala? Badilikeni bana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom