CCM mnaipeleka wapi nchi hii?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
23,519
21,549
Mwishoni mwa karne ya 19 mabepari wa kikoloni waliketi huko Berlin nchini Ujerumani wakapanga mikakati ya kuligawana na kulitawala Bara la Afrika kwa maslahi yao binafsi. Juhudi zao zilifanikiwa kwa 99% na unyama waliowafanyia waafrika kila mtu anaufahamu – tulinyonywa, tukaonewa, na kudhalilishwa kwa kiwango cha mwendokasi.

Africa_1914.jpg

Ni jambo la kusikitisha kuona CCM nao wanataka kuiga mtindo huu wa “Divide And Rule” uliotumiwa na wakoloni kututawala. Siku za karibuni CCM na serikali yake wameanza kuwagawa watanzania kwa malengo yale yale ya kikoloni.

Jana tumeshuhudia wanafunzi wa UDOM amabo ni wafuasi wa CHADEMA/UKAWA wakizuiwa kufanya mahafali yao huku wale wa CCM wakiruhusiwa kuendelea na mahafali yao huko Iringa bila kubughudhiwa. Aidha, maandamano na mikutano ya kisiasa ya UKAWA imepigwa marufuku wakati mikutano na maandamano ya CCM yanaendelea kama kawaida. Juzi kati wafuasi wa CCM waliandamana huko Mwanza na mpaka leo hatujasikia wakitiwa msukosuko wowote na polisi wao.

Ninachoona sio tu kwamba CCM wanagawanya na kutawala lakini pia wanajaribu kulifanya kundi moja liwe na chuki dhidi ya serikali na kulijengea mentality ya kulipiza visasi. Ikiwa kundi kandamizwa litaona linaonewa sana kwa kutumia CCM militia, nao hawakawii kufikiria kuanzisha vyombo vyao vya kujilinda. Ndio. Sasa wewe unadhani wataendelea kunyanyaswa mpaka lini? Haiwezekani kundi moja likawa na vyombo vyao vya ulinzi vinavyomiliki kila aina ya silaha wakati kundi la pili halimiliki hata kirungu kimoja.

Hii mbegu ya ukabila ilianza kumea kwa miaka mingi huku CCM wakishuhudia na kuchekelea kwa kuwa wanafurahia uwepo wa mgawanyiko huu. Tujiulize tumefikaje hapa. Hadi leo hii kuna vikundi vya kikabila na kikanda katika vyuo vikuu ambavyo hufanya mahafali yao kwa misingi ya kikabila na kikanda. Utaratibu huu umefumbiwa macho na uongozi wa vyuo vikuu na serikali kwa muda mrefu sasa. Baada ya mihemko ya kisiasa kuingizwa vyuoni na CCM, sasa ukanda na ukabila huu umehamia kwenye vyama vya siasa. Na kinachoudhi zaidi ni kuona kundi moja linaandamwa na kunyanyaswa huku kundi la pili likiendelea na shughuli zao bila kubughudhiwa.

Mwanzo wa ngoma ni lele. Ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha kamwe. Ulaji wa nyama ya mtu ni sawa na ubaguzi. CCM imelea mgawanyiko wa kikanda na kikabila katika vyuo vikuu hadi umezaa mgawanyiko wa kiitikadi za vyama (CCM vs UKAWA). Kuna taarifa kuwa mgawanyo huu umeingia hadi kwa wahadhiri wa vyuo vikuu – kuna wahadhiri wenye muelekeo wa CCM na wahadhiri wenye muelekeo wa UKAWA. Ikiwa mgawanyiko huu utazidi kufumbiwa macho, tutafika hadi kugawana madarasa ya mihadhara (lecture theatres). Kutakuwa na madarasa wanayosoma wanaCCM wakifundishwa na wahadhiri wa CCM na kutakuwa na madarasa ya UKAWA yanayofundishwa na wahadhiri wa UKAWA. Bila shaka huku ndiko CCM wanakotaka kutupeleka.

Dhambi ya ubaguzi haitaishia hapo tu bali itasambaa hadi hapa mitaani. Kule Zanzibar sasa tunashuhudia mgawanyiko mkubwa sana. Watu hawashirikiani katika misiba, harusi, na matatizo mengine kwa misingi hiyo hiyo ya kisiasa iliyoasisiwa na kupaliliwa na CCM kwa ajili ya Divide And Rule. Baada ya kufanikwa kuwagawanya wazanzibar sasa wanataka kuhamishia ubaguzi wao huko Tanganyika. Watanganyika kuweni makini. Msikubali kugawanywa kizembe hivyo.
 
Mbona hata ndani ya ukawa kuna devide and rule. Hii mbinu huwa inaenda kusomewa vyuoni.
 
Mwishoni mwa karne ya 19 mabepari wa kikoloni waliketi huko Berlin nchini Ujerumani wakapanga mikakati ya kuligawana na kulitawala Bara la Afrika kwa maslahi yao binafsi. Juhudi zao zilifanikiwa kwa 99% na unyama waliowafanyia waafrika kila mtu anaufahamu – tulinyonywa, tukaonewa, na kudhalilishwa kwa kiwango cha mwendokasi.
Ni jambo la kusikitisha kuona CCM nao wanataka kuiga mtindo huu wa “Divide And Rule” uliotumiwa na wakoloni kututawala. Siku za karibuni CCM na serikali yake wameanza kuwagawanya watanzania kwa malengo yale yale ya kikoloni.

divide-and-rule.jpg

Jana tumeshuhudia wanafunzi wa UDOM amabo ni wafuasi wa CHADEMA/UKAWA wakizuiwa kufanya mahafali yao huku wale wa CCM wakiruhusiwa kuendelea na mahafali yao huko Iringa bila kubughudhiwa. Aidha, maandamano na mikutano ya kisiasa ya UKAWA imepigwa marufuku wakati mikutano na maandamano ya CCM yanaendelea kama kawaida. Juzi kati wafuasi wa CCM waliandamana huko Mwanza na mpaka leo hatujasikia wakitiwa msukosuko wowote na polisi wao.

Ninachoona sio tu kwamba CCM wanagawanya na kutawala lakini pia wanajaribu kulifanya kundi moja liwe na chuki dhidi ya serikali na kulijengea mentality ya kulipiza visasi. Ikiwa kundi kandamizwa litaona linaonewa sana kwa kutumia CCM militia, nao hawakawii kufikiria kuanzisha vyombo vyao vya kujilinda. Ndio. Sasa wewe unadhani wataendelea kunyanyaswa mpaka lini? Haiwezekani kundi moja likawa na vyombo vyao vya ulinzi vinavyomiliki kila aina ya silaha wakati kundi la pili halimiliki hata kirungu kimoja.

Hii mbegu ya ukabila ilianza kumea kwa miaka mingi huku CCM wakishuhudia na kuchekelea kwa kuwa wanafurahia uwepo wa mgawanyiko huu. Tujiulize tumefikaje hapa. Hadi leo hii kuna vikundi vya kikabila na kikanda katika vyuo vikuu ambavyo hufanya mahafali yao kwa misingi ya kikabila na kikanda. Utaratibu huu umefumbiwa macho na uongozi wa vyuo vikuu na serikali kwa muda mrefu sasa. Baada ya mihemko ya kisiasa kuingizwa vyuoni na CCM, sasa ukanda na ukabila huu umehamia kwenye vyama vya siasa. Na kinachoudhi zaidi ni kuona kundi moja linaandamwa na kunyanyaswa huku kundi la pili likiendelea na shughuli zao bila kubughudhiwa.

Mwanzo wa ngoma ni lele. Ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha kamwe. Ulaji wa nyama ya mtu ni sawa na ubaguzi. CCM imelea mgawanyiko wa kikanda na kikabila katika vyuo vikuu hadi umezaa mgawanyiko wa kiitikadi za vyama (CCM vs UKAWA). Kuna taarifa kuwa mgawanyo huu umeingia hadi kwa wahadhiri wa vyuo vikuu – kuna wahadhiri wenye muelekeo wa CCM na wahadhiri wenye muelekeo wa UKAWA. Ikiwa mgawanyiko huu utazidi kufumbiwa macho, tutafika hadi kugawana madarasa ya mihadhara (lecture theatres). Kutakuwa na madarasa wanayosoma wanaCCM wakifundishwa na wahadhiri wa CCM na kutakuwa na madarasa ya UKAWA yanayofundishwa na wahadhiri wa UKAWA. Bila shaka huku ndiko CCM wanakotaka kutupeleka.

Dhambi ya ubaguzi haitaishia hapo tu bali itasambaa hadi hapa mitaani. Kule Zanzibar sasa tunashuhudia mgawanyiko mkubwa sana. Watu hawashirikiani katika misiba, harusi, na matatizo mengine kwa misingi hiyo hiyo ya kisiasa iliyoasisiwa na kupaliliwa na CCM kwa ajili ya Divide And Rule. Baada ya kufanikwa kuwagawanya wazanzibar sasa wanataka kuhamishia ubaguzi wao huko Tanganyika. Watanganyika kuweni makini. Msikubali kugawanywa kizembe hivyo.

Kwa hiyo labda tukusaidiaje sasa?
 
Mbona hata ndani ya ukawa kuna devide and rule. Hii mbinu huwa inaenda kusomewa vyuoni.
mkuu, bado hujaelewa mada. hebu rudia tena kusoma kabla ya kutoa maoni yako.
 
Kwa hiyo labda tukusaidaje sasa?
kwa kuwa malengo yenu ni kuwagawa watanzania kwa misingi hiyo ili muwatawale, endeleeni kufanya hivyo kwa bidii zenu zote lakini fahamu kwamba matokeo ya ugawanyaji huo yatawagharimu sana.
 
Hivi nani anayewagawa Watanzania? Kiongozi anaenda kwenye chuo na kuongea na wanafunzi wa Itakdi moja tu, huyo ndio anaunganisha Watanzania au anawagawa?
 
ni nani anayewagawa wanachuo kumbe? poliCCM wanatumiwa kuwatawanya wanachuo wa UKAWA huku wanachuo wa CCM wakiachwa waendelee na mahafali yao. hivi umesoma post yote na je, umefuatilia matukio ya hapa nchini siku za karibuni au uko ughaibuni? acha kujitoa akili mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tunachanganywa au kujichanganya; mtuambuaji majipu ni JPM na akifanya hivyo tunalipuka kumshangilia. Mtuambuaji huyo huyo akituburuza na police wake tunasema CCM inatupeleka pabaya. Natuanze kumtambua anayefanya haya ili tusijichanganye na kupoteza tagert; Zito yuko sahihi.
 
Inashangaza kuona jinsi sera za Magufuli za kupambana na Ufisadi zinavyosababisha anxiety pale Ufipa...
 
Wakati mwingine machozi yananitoka
Kuona wengine wakiruhusiwa huku wengine wakizuiwa kwa mabomu ya machozi
Jana nililia sana kwa hili
Na machozi yamenitoka tena leo baada ya kupata habari kua huko moshi nako wamezuiwa
Nalia kwa uchungu pale wengine wanaporuhusiwa huku wengine mabomu yakitumika
Haki iko wapi jamani
 
uchaguz hata ufanyike kesho bado cCm itashinda, nchi hii bado sana kubadilika
Unajua kwa nini watashinda na kuendelea kushinda?! NEC ni ya CCM na ndio inayomtangaza mshindi. Na kwa nafasi ya raisi hakuna kupinga matokeo mahakamani. Huwezi kupata ushindi kwenye uwanja wa ugenini wakati refa, wasaidizi wake na kamisaa ni wa wenyeji. Kwenye hizi chaguzi vyama vya upinzani huingia kama wageni. Ukumbuki kauli ya Nape? "Tutashinda hata kwa goli la mkono".
 
Back
Top Bottom