Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,789
- 1,732
Juliana Shonza na Mtela Mwampamba walijiunga na CCM tarehe 12 Februari 2013 na kupokelewa na Kamati Kuu ya CCM. Hii ilikuwa ni baada ya wao kufukuzwa Uanachama wa BAVICHA na CHADEMA. Tukio hilo lilionesha kuwa ni kubwa sana kwa CCM na ikaonekana CCM wamepata vijana watakaoisaidia kukijenga chama.
Mara moja Nape Nnauye akawachukua vijana hao na kuanza kuzunguka nao, wakifanya siasa za kuzungumza mabaya ya CHADEMA na uongozi wa juu wa CHADEMA. Mlengwa mkubwa wa kampeni hizo alikuwa Dr. Slaa.
Siasa za kuchafuana huwa zinaweza kuzaa matunda mazuri pale ambapo zinajikita kwenye ukweli. Chama cha siasa kikijenga hoja zake kwa kutumia uongo, na baadaye kikagundulika kuwa kimetumia uongo, watu walio waadilifu wanaotafuta kuunga mkono wanasiasa wenye dira inayoweza kuendeleza nchi wanakwazika. Wale wasiopenda kujihusisha na 'Ulaghai' huamua kujitenga na waongo hao. Wanasiasa hao hujikuta wamebaki na makundi ya watu ama wenye uelewa mdogo, au washabiki kupindukia kiasi wanakuwa na upofu wa kuona kasoro ndani ya chama, au wale wanaofaidika kwa namna fulani (wachumia tumbo).
Juliana Shonza alianzisha shutuma za mpango wa Dr. Slaa kumuua Zitto Kabwe ambazo zilidakwa na gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013.
Lengo la Juliana Shonza lilikuwa kuchonganisha viongozi wa juu wa CHADEMA (Katibu Mkuu na Makamu wake) na kuchafua taswira ya Katibu Mkuu kwa umma.
Leo hii Zitto mwenyewe amekanusha tuhuma hizo kuwa si za kweli https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/424280-siri-ya-kuuwawa-zitto-uwongo.html. Jibu la Zitto linaweza kuwekwa kifupi kwa ujumbe wa twitter aliotuma Zitto mwenyewe:
Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe 2h Mtanzania leo imeandika habari 'Siri ya kuuwawa Zitto yafichuka'. Habari hii sio ya kweli. Sijawahi kukutana na Ben Saanane hata siku moja 3:09 AM - 27 Mär 13 ·
Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe 2h Pia sijawahi kufika na wala siijui Hotel ya Lunch Time Mabibo. Ninaomba Mtanzania wathibitishe na vyanzo vyao habari hiyo 3:11 AM - 27 Mär 13 ·
Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe 2h Siamini kabisa kwamba Katibu Mkuu CHADEMA anaweza panga kuniuwa mie. Hana sababu kufanya hivyo. 3:12 AM - 27 Mär 13·
Juliana Shonza anaonekana ni muongo, na kwa kuwa anawakilisha CCM, propaganda za CCM zinaanza kuthibitika kuwa zinatumia uongo pia.
ANGALISHO
Japo uongozi uliopo sasa wa CCM una vijana Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Lusinde, HKigwangallah n.k), ambao wako tayari kutumia propaganda za majitaka, bado kuna wazee wenye busara: Mangula, Msekwa, Salim, Warioba n.k. ambao sina hakika kama wanafurahia mwenendo wa chama kuanza kuonekana WAONGO.
Wazee kwa vijana, busara itumike ili hao WALIOFUKUZWA CHADEMA, wasiwe chanzo cha kuharibika kwa Taswira ya Chama machoni pa watu wenye hekima zao.
Uongo unaweza kuleta faida za muda mfupi lakini unaweza kusababisha madhara ya muda mrefu.
CCM, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wamepokewa ndani ya chama baada ya kufukuzwa CHADEMA. Kuweni waangalifu kama kweli mmepata au mmepatikana.

By Juliana Shonza![]()
![]()
KUHUSU BEN SAANANE NA KUTUMIKA KUMUUA ZITTO KABWE
Wana jf, Nakili wazi hili swala lilitokea mnamo mwezi wa 5 mwaka 2012 tukiwa Lunch time hotel external kwenye mazungumzo ya kawaida(ambavyo ben saanane anaita ni vikao vya kuhujumu chama). Siku ya tukio tukiwa meza moja na Ben Saanane mkono wake wa kushoto alifunga bandeji akidai ameumia mkono(nakumbuka). Kwa babati mbaya sana katika maongezi yale Ben alilewa pombe (alikuwa anakunywa bia(kilimanjaro). Kulewa kwake pombe alijisahau na kutoa bahasha ya kaki yenye fedha, ndani ya bahasha ile wakati wa kutoa fedha alipe huduma ya chakula na vinywaji alidosha karatasi ya nailoni ndogo ikiwa na unga mwekundu ndani.
Tulimuuliza ni nini hicho akadai ni kuberi,na kuing'ang'ania tusifungue(aliyekiokota ni mwampamba).Lakini Mwampamba aligoma kumpa na kudai lazima ifunguliwe pale pale.
Ben saa nane akiwa katika hali yake ya kulewa alifura kwa hasira kutaka arudishiwe ilekaratasi,haliiliyopelekea uvunjifu wa amani pale lunch time hotel.Mwampamba aliondoka na mzigo ule kwa kukimbia nao, usiku ule Ben alitafutana na mwampamba hadi nyumbani kwake(temeke) akidai huo mzigo(ikumbukwe mwampamba na mm nimeishi kwake na nikaka yangu) . Lakini katika hali ya kusikitisha ben aliomba mzigo ule usiende mbali na kuahidi atasema kweli kile ni nini.
Ben saanane alikili wazi kwamba ile ni sumu lakini anapeleka nyumbani kwa ajili ya kuulia panya, Swala hili halikuishia usiku ule,ben hakufanikiwa kupata mzigo ule kesho yake asubuhi(jumapili) alikwenda kumsihi mwampamba ampatie mzigo.
Sharti lilikuwa aseme ni nini kwasababu huwezi kuwa na sumu eneo la starehe kama pale hotelini huku akisisitiza kuonana na zitto ambaye alisafiri usiku ule kwenda marekani bila kuonana na yeyote kati yetu?
Ndipo Ben saanane akakili ile ni sumu akilenga kumpatia zitto akiwa ametumwa na Dr.slaa.Tulihamaki kusikia kile kitu(hapa tulikua tabata reli stand tukisubiri usafi).Nilimuuliza uthubutu wake wa kufanya kitu kama hicho na kwanini afanye unyama huo,akadai ametumwa Kisa kikiwa ni zitto kumsakama dr.slaa ndani ya vikao vya chama.
Swala hili lilifika mbali kwa kuwekeana mipaka ya kula vyakula mahotelini na kutoshirikiana tena katika ushikaji wetu kama masalia.
Lengo la Juliana Shonza lilikuwa kuchonganisha viongozi wa juu wa CHADEMA (Katibu Mkuu na Makamu wake) na kuchafua taswira ya Katibu Mkuu kwa umma.
Leo hii Zitto mwenyewe amekanusha tuhuma hizo kuwa si za kweli https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/424280-siri-ya-kuuwawa-zitto-uwongo.html. Jibu la Zitto linaweza kuwekwa kifupi kwa ujumbe wa twitter aliotuma Zitto mwenyewe:
Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe 2h Mtanzania leo imeandika habari 'Siri ya kuuwawa Zitto yafichuka'. Habari hii sio ya kweli. Sijawahi kukutana na Ben Saanane hata siku moja 3:09 AM - 27 Mär 13 ·
Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe 2h Pia sijawahi kufika na wala siijui Hotel ya Lunch Time Mabibo. Ninaomba Mtanzania wathibitishe na vyanzo vyao habari hiyo 3:11 AM - 27 Mär 13 ·
Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe 2h Siamini kabisa kwamba Katibu Mkuu CHADEMA anaweza panga kuniuwa mie. Hana sababu kufanya hivyo. 3:12 AM - 27 Mär 13·
Juliana Shonza anaonekana ni muongo, na kwa kuwa anawakilisha CCM, propaganda za CCM zinaanza kuthibitika kuwa zinatumia uongo pia.
ANGALISHO
Japo uongozi uliopo sasa wa CCM una vijana Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Lusinde, HKigwangallah n.k), ambao wako tayari kutumia propaganda za majitaka, bado kuna wazee wenye busara: Mangula, Msekwa, Salim, Warioba n.k. ambao sina hakika kama wanafurahia mwenendo wa chama kuanza kuonekana WAONGO.
Wazee kwa vijana, busara itumike ili hao WALIOFUKUZWA CHADEMA, wasiwe chanzo cha kuharibika kwa Taswira ya Chama machoni pa watu wenye hekima zao.
Uongo unaweza kuleta faida za muda mfupi lakini unaweza kusababisha madhara ya muda mrefu.
CCM, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wamepokewa ndani ya chama baada ya kufukuzwa CHADEMA. Kuweni waangalifu kama kweli mmepata au mmepatikana.
Last edited by a moderator: