CCM mmeridhika na Livingstone Lusinde?

kwa kuangalia picha yake sioni haja ya kumshitaki

389ea4fb-b878-4364-ad90-4499e3e4ac7b.jpg
 
matusi,

kiburi,

hana nidhamu,



hivi kweli LEMA NA LUSINDE aliyevunja rekodi ya kutukana nani????

au jimboni kwake wananchi wooote wanatukanana na ndio tabia yao?????

NAWASILISHA!!!''"'

PJN
 
mods hizi threads za lusinde zimezidi. ni bora ziunganishwe

matusi, kiburi, hana nidhamu, hivi kweli LEMA NA LUSINDE aliyevunja rekodi ya kutukana nani???? au jimboni kwake wananchi wooote wanatukanana na ndio tabia yao????? NAWASILISHA!!!''"' PJN
 
Siwezi kumshangaa LUSINDE,ninaowashangaa ni wana-Mtera waliotuchagulia takataka badala ya mbunge.
 
Niwalambe nisiwambeeeeee?................................Walambeeeeeeee!!!!!!!!! kwa staili ile mwanadiplomasia Chigwiyemisi ilikuwa lazima aoondoke tu. Anye bulayi hivi hapo Mtera hakuna kijana makini wa CDM aanze kupiga jaramba kuchukua nafasi........Hilo jimbo liko wazi changamkeni.
 
Katika hotuba hiyo yote sijaona,mahali ambapo sera zimeongelewa na zimemgusa mwananchi wa ARUMERU mashariki,CCM alipitaje kwenye kura za maoni huyu?
 
Sera za ushawishi zimewaishia ndiyo maana wanaporomosha matusi. Huoni wanavyodandia shughuli zisizo wahusu. Ufisadi wamedandia, katiba mpya wamedandia, misiba wanadandia, n.k.
 
Hivi huyu jamaa ana upeo gani wa elimu? na katika jimbo lake anajuwa vizuri kero za wananchi wake? Mwenye profile yake tafadhari aiweke hapa, maana vitu vingine vinaweza kuwa ni issue ya knowledge. Hii ni sawa na taarabu au ngonjera. Kuna Tamalizeni au wale jamaa wa Fataki anaweza kujiunga nao maana ana kipaji.
 
Naona amefanikiwa kusahaulisha "utani wa Mkapa", na hiyo ndiyo iliyokuwa dhima ya "ngojera kibudu" ya 'Mh'. Lusinde.
 
Nilishawahi kuwaambia wana JF kuwa huyu Lusinde ni mwendawazimu, bahati nzuri yeye mwenyewe amewathibitishia. Nafikiri huyu ni mmoja wa wale vijana ambao Wasira alisema wanavuta bangi.
 
Kweli nimeamini mwisho wa magamba umefika. Kama matusi ndio sera!! Hivi watoto wa Lusinde wakisoma hizi habari wanajisikiaje? Au hana watoto? Shame on him!!!!
 
asilimia kubwa kama sio yote ya wabunge na viongozi wa ccm ni wa aina hiyo,...yaani hata maovu yanayofanyika katika mahabusu na magereza yetu, yeye anafagilia tu, hicho ndio chama tawala
 
Jamani samahani wana jf kuna mjinga hapa wa ccm aamini kama lusinde alitukana naomba mnikumbushe ni ukurasagani nimesahau au aliyetuma matusi anitumie tena narudia samahani hawa kenge wananisumbua hapa
 
Kudadadeki,usidanganyike na rangi utamu wa chai sukari,kama hauoni papasa utapata majibu au na hilo unataka mtu kutoka dodoma aje kuwaambia? Au haujui kama lusinde analiwa? Kudadadeki.
 
Wataka matusi ya Muhishimiwa Lusinde (MB) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Sisiem??? Usikonde haya hapa.....................................................................

Mh mwenyekiti wa chama, waheshimiwa viongozi wenzangu na wanachama wenzangu, nataka nianze kutofautiana hapahapa jukwaani na wenzangu, habari ya sisi kutukanwa halafu tunasema sisi hatutukani hatufanyi kazi ya kanisa hapa, kudadadeeeki matusi yakija nitatukana hoja zikija nitasema, potelea mbali

CCM oyeeeee.......oyeeee!

Niseme nisiseme.....semaaaaaa!

Unajua kuna wabunge wa chadema maji marefu unawalea sana, wewe ndio uliowachanja chale mpaka matakoni leo wanakutukana, nataka niwaambieni wenzetu wanajifanya wanajua kutukana hapa mwisho! ndio maana nimekuja kuwapasha kwamba hoja nyingine za kipuuzi wanazozisema chadema wanajitukana mpaka wao wenyewe, kuja kusema hapa kwamba mgombea wa ccm katoboa sikio kwa hiyo ni shoga maana yake na baba yake slaa nae ni shoga maana nae katoboa sikio kudadadeeeki CCM oyeeee....oyeeeee


Nataka niwaambie ndugu zangu msindanywe, msidanganywe na rangi utamu wa chai sukari, wale waliojazana katika chadema wote karibu nusu baba zao wametoboa masikio kwa hiyo na wao mashoga? Niwaambie nisiwaambie. . . .waambie! mbunge wa arusha mjini juzi alikua mahabusu na si tunajua kule mahabusu alifanywa nini, lakini hatutaki kusema

tuwalambe tusiwalambe.....walambeee!

Ndungu zangu nataka niwaambieni kwa habari ya lugha chafu wote sisi tunazo wala msifikiri hatujui sisi hatuna, tunajua Lema alikua mahabusu amepata bwana kule tunajua, na kuna wanaume wengine wameolewa sisi tunawafahamu, nataka kuwasihi sana, kwenye uchaguzi, kwenye uchaguzi tunajenga hoja za msingi lakini wakileta maneno ya honyo na hapa yapo, kudadadeeeki

nataka niwasihi sana, hakuna mtu asiye na makosa duniani, leo dr slaa anapita kuwasema wenzake wakati yeye upadri ulimshinda kanisa likamfukuza kwa kutia mimba wanakwaya

Sioi oyeeee! Oyeeee!

Mi nawafahamu wale, unajua tukiendelea kuwachekea hivi tukiendelea kuwambeleza hivi itafika mahali watatuchokoa machoni bora tule nao sahani moja, kuna bwe.ge mwingine yuko mle, kuna bweg.e mwingine yuko mle anajiita campain manager wa chadema, ukoo wa nyerere, baba yake mzazi wa nyerere akiitwa buhito alikua akitoboa masikio, alikua shoga? anajitukana mpaka mwenyewe kwa sababu ya akili mbovu, kutoboa masikio sio ushoga, masai wanatoboa, wagogo wanatoboa, wameru zamani walikua wanatoboa, wa-wakurya wanatoboa, wakamba wanatoboa, ye hajui historia anakuja hapa (huku kabana pua) ng'wee ng'wee ng'weeee, mbona ye ameliwa si hatusemi

ccm oyeee, oyeeeee
wanaokipenda chama mikono juuu!

(sauti ya kike kwa mbaali inasikika - wamekwisha!)

subiri niwaambie, hoja zinazojengwa hapa ni hoja za kipumbavu, kuna watu wanakuja kujenga hoja ya kitoto, kwamba msimchague sioi kwa sababu alizaliwa kenya, sio raia wa tanzania, mtu akizaliwa kwenye ndege anakua raia wa nchi gani? Acheni ushamba nyie, Suala la mtu kuzaliwa na suala na uraia ni vitu viwili tofauti, uchungu unapompata mwanamke anazalia hapohapo hawezi kusubiri, kuna wengine wamezaliwa kwenye mabasi mbona hatuwaiti raia wa basi, washamba wakubwa nyie, hiyo mnaona ni hoja ya kupita mnazungumza, halafu nyingine wanapita wamebana pua, msimchague sioi kwa sababu baba yake alikua mbunge, baba yake atarudi lini? Baba yake anarudi?

Ngojeni niwaeleze, na bahati nzuri najua walipo ntakua napiga hapa afu napiga palepale, kudadadeeeki . . .

PART TWO COMING SOON!

Muendelezo huu hapa

CCM oyeee .....oyeeeee!
Msikubali kudanganywa ndugu zangu maswala ya mtoto kufata kazi ya baba yake, katika tanzania ni kitu cha kawaida, tunao wanajeshi na watoto zao wanajeshi uongo kweli?....kweliiiiii! tunao madereva na watoto wao madereva uongo kweli?.....kweliiii, tunao wapiga debe na watoto zao wapiga debe uongo kweli . . . kweliiii! kuna ajabu gani kwa sioi piga makofi kwake.

Niwaulize nisiwaulize.....ulizaaaaaaa! Marehemu sumari angekua daktari na mtoto wake daktari CHADEMA wangegoma kunywa dawa (sauti ya kimbea kwa mbali inajibu . . . . wathubutu!), washamba nyie!

ccm oyee. . . oyeeee! Niwalambe nisiwalambe. . . . walambeee!

Ndio maana tunataka tuwaambie chama cha mapinduzi ndiyo chenye makamanda wa ukweli sio nyie makamanda feki, Jakaya Kikwete mwenyekiti wa ccm kazi yake zamani alikua mwanajeshi uongo kweli?..... kweliiii, kapteni komba alikua mwanajeshi uongo kweli? .......kweliiii! lakini wanavaa nguo za kijani halafu washamba ambao hata mgambo hawajapita wanavaa makombati.

ccm oyeee.....oyeeee!
Halafu katika washamba hakuna mshamba kama dokta slaa, anavaa kombati kuuubwa akitembea kama kajinyea vile (anapata shangwe kutoka kwa wanaomsikiliza, sorry to say this hapa hata mke wangu alicheka, nikamtazama kwa hasira hadi akaogopa!)

Nipige Nisipigeee?.........Pigaaaaaaa aaaaa
Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .......Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mahindi yanaota na rangi ganiiiiiiiiiiiii?............K ijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mpunga unaota na rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?............... ............Kijaniiiiiiiii.
Piga makofi na vigelegele kwa chama cha mapinduzi.

Nataka niwaambie kama CHADEMA, kama viongozi wa CHADEMA ni vichaa wa kurogwa, mie ni kichaa wa kuzaliwa, kudadadeeeki! tarehe moja, dk slaa juzi, (anaguna) yaani katika watu washamba nimewashangaa dk slaa, anakakaa kwenye tv anasema eti ''ooooh hapa isipochaguliwa chadema patachimbika'' kama ni fujo itaanzia arumeru, kwa nini isingeanzia kwa mke wake? Ngoja niwaambie ndugu zangu, alichokua anakisema slaa, alichokua anatutishia vita slaa mimi namwambia anatishia kujamba wakati anaharisha.

ccm oyeee....oyeeee!. wangapi mtampa kura kura sioi, mikono juu....(watu wananyanyua mikono), hatufanyi kazi ya kanisa hapa! hapa tumekuja kuwaambia kwa suala la kutishana hakuna mtu anayeogopa, wote si tumeaga na nataka niwaambie slaa yule anavimba macho ya watu, lakini kama slaa ana ubavu nipeni mi tuweke ulingo hapa, ngumi moja naua yule, nikikusanya yule nipige mkono mmoja mnakuja kuokota yule, akiona watu wamejaa (anabana pua) ng'weng'weng'wee ng'weng'weng'wee upadri umemshinda ataweza serikali? thubutuu!

Nataka niwaambie, ndugu zangu wa arumeru, suala la uchaguzi mdogo sio suala la kudanganywa, wanakuja CDM hapa wanakudanganyeni, kwamba watapora mashamba ya wazungu wawagawieni, muasisi wa chama cha CDM ndugu mtei ana shamba hapa heka 700 mbona hawampori wawagawie? wangeanza kwanza la mtei, sio kuwadanganya wananchi, kama wanawapenda kweli wa meru wamwambie mzee mtei chukua shamba lako rudisha kwa watu wa meru(sauti ile ya kike. . . hatudanganyiki)

ccm oyeee.....oyeeee!
Niwachane nisiwachane?......wachaneee!

Vijana wenzangu, CDM inawapa pesa za kunywa viroba, mnalewa viroba na bangi mnazomea wazee wenu, halafu wenzenu wanapita na helikopta wanawaona machizi

niseme nisiseme.....semaaa!

Kokote duniani askari wanaoteka nchi ni askari wa miguu wacha wao waruke juu si tunateka nchi, wao wanaruka na helicopter si tunachukua jimbo asubuhi, kudadadeeki, mnakuja mnadanganywa hapa eti ooh chadema, sijui ooh nasari ataleta ajira na soko, ajira atazitoa wapi? Watu hawana shukrani anasimama hapa dk slaa anatukana ccm, hawajafanya kitu, hawajafanya kitu, shule alizosoma yeye zimejengwa na baba yake? shule zimejengwa na serikali ya chama cha mapinduzi, watu wanajiita wamesoma chuo kikuu (chuo hicho) kimejengwa na serikali ya chama cha mapinduzi, nionesheni hapa chuo walichojenga CDM. . . hakunaaa!

ccm oyeee....oyeeee!

Wanatuletea sera ya jogoo, nataka mkatae sera ya CDM ni sera ya jogoo, Jogoo katika makuku maongo hakuna kama jogoo, Jogoo linapokua linamtaka kuku mwenzake linadanganya linamwambia nitakushonea gauni reeefu mpaka huku (anainama huku akizunguka kuonyesha mfano wa jogoo, watu wanalipuka kwa kicheko)

Niseme nisiseme. . . .semaaaa!

Kataeni uongo wa jogoo, linaahidi kushona gauni refu wakati lenyewe likiinama hata chupi halina, waongo wakubwa tunawajua, na hivyo viroba mnavyokunywa vijana, viroba mnavyokunywa vijana mwisho tarehe moja, wataondoka watakuacheni mmetukana wazee wenu, mmewapiga mawe wazee wenu, na mimi nataka niwaambie vijana wa CDM utaonekana kichaa ukionekana unazomea rangi ya kijani maana utakuta mti una rangi gani....kijani! unaanza uhuuuu watu wanasema huyu chizi, mchezaji aliyeumia ni mchezaji wa timu ya ccm tunaweka mchezaji wa ccm, suruali yangu nyeusi imetoboka siwezi kuweka kiraka cheupe kama nina akili nzuri, inabidi niweke cha rangi gani? Kijaniii! Hata hilo mnataka mtu atoke dodoma kuja kuwaambia? Kama huoni kwa macho papasa kwa mkono utapa majibu.

Ccm oyeeeee.....oyeeeee!
Niwaambie nisiwaambie hawa.....waambie!...ngoja niwaambie watu wa CDM nyie

nikakutana na kijana mmoja akanichekesha sana, ananiambia mwanaume mzima, basi kati ya watu ambao hawajui kiswahili mbowe hajui kiswahili, mbowe anasimama anasema nina uchungu mkubwa, bibilia inasema hivi wanawake mtazaa kwa uchungu, wanaume watakula kwa jasho uongo kweli...kweliiii! kama mbowe anauchungu ana mimba?....vicheko

ccm oyeeee.....oyeeee!

Nataka niwaambie, kipindi hiki ni kipindi cha lala salama, ukiona mtu anasikia kichefufu, ukiona mtu anatema mate, ukimuona mtu anaichukia ccm ujue tayari tumeshamtia mimba, ndio maana unawaona saa hizi wanapiga kelele, unaona kina slaa wanapiga kilele, wameshapigwa mimba, mbowe pigwa mimba, nasari pigwa mimba....mayoweee

Tarehe moja wanaenda kujifungua mtoto anaitwa sioi, piga makofii. Kichefuchefu chote kitawaisha utawaona ooh tulikua pamoja tulikua pamoja kudadadeeki.

Niwachane nisiwachane?.....wachane!

we ukiona unapita mwanaccm humsemeshi mtu anakufanyia hivi (anaonesha V, ishara ya CDM) ujue ana mimba ya mapacha, mnunulie udongo, mnunulie maembe mabovu, mnunulie vitu vya uchachu tarehe moja anajifungua sioi anakwenda bungeni na wao mimba wanazaa hapohapo.

Tuwapime wenye mimba tusiwapime....tuwapimeeee
Tuwapime wenye mimba tusiwapime....tuwapimeeee

nitakuuliza swali, nitakuuliza swali, atakaempigia kura sioi anyoshe mkono kama hakunyosha jua ana mimba

ccm oyeeee....oyeeee!


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/03/kudadadeki-matusi-yakija-nitatukana-hoja-zikija-nitasema-potelea-mbali-lusinde.html#ixzz1rL1zYtD7
 
Ebwana huyu jamaa si mzima...sioni tofauti ya domo lake na 'choo'!Huwa siku zote najiuliza, hv kwek huyu jamaa ana 'dini'...dah, mitusi yote ile hadharani??!Lusinde Mitusi anatisha....
 
Back
Top Bottom