CCM mkiitumia JamiiForums vizuri mtanufaika

CCM mkiitumia JamiiForums vizuri mtanufaika

Hii dhana ya CCM na serikali yake kuuona huu mtandao ni hatari kwao ni ya kipuuzi Sana.ccm na serikali mnapaswa muelewe jamii forum ina watu wenye IQ kubwa kuliko vile mnavyo dhani. Jamii forum siyo kijiwe cha kahawa. Huyu musiba atashindwa hawezi kufanikisha ujinga wake dhidi ya jamii forum. Jamii forum imeshaibua mambo mengi ya kuisaidia nchi. Jamii forum si kijiwe cha kulazimishwa kumsifia mtu, humu tuna mawazo huru. Chonde Chonde CCM mkanyeni mtu wenu.kuendelea kuifatilia jamii forum mnapoteza muda.
Wenzio wanafikiria kuteka teka, kuua na kupiga risasi wanao amini hawako upande wao. Jf wanatamani kuiteka na kupoteza.
 
Hii dhana ya CCM na Serikali yake kuuona huu mtandao ni hatari kwao ni ya kipuuzi Sana. CCM na Serikali mnapaswa muelewe jamii forum ina watu wenye IQ kubwa kuliko vile mnavyo dhani. JamiiForums sio kijiwe cha kahawa.

Huyu Musiba atashindwa hawezi kufanikisha ujinga wake dhidi ya JamiiForums. JamiiForums imeshaibua mambo mengi ya kuisaidia nchi.

JamiiForums si kijiwe cha kulazimishwa kumsifia mtu, humu tuna mawazo huru. Chonde Chonde CCM mkanyeni mtu wenu.

Kuendelea kuifatilia JamiiForums mnapoteza muda.
CCM wao wanafanya Mikutano ya Hadhara mkuu humu ni wasioruhusiwa mikutano
 
Ukiona mtu anakimbilia silaha ujue hana hoja,ana vihoja.

Ukiona mtu kaanzisha utamaduni mpya wa kuteka watu ujue hoja hana.

Ukiona watu flani wanashambuliwa kwa mapanga,wanapigwa risasi wakiwa kwenye wajibu wao kwa mujibu wa sheria,tena mchana kweupe,wala hakuna uchunguzi wowote wa maana unaofanyika,ukiona vigazeti uchwara vinaanzishwa na kuwashambulia watu kwa maelekezo kutoka juu,ukiona wabunge na madiwani wa upinzani wananunuliwa nk...ujue watawala hawana hoja,sasa wana vihoja.
 
Ndo maana mimi nislishaachaga kufuatilia mambo ya upande wa huku au wa kule...najitafutiaga tu ugali...nikshiba nalala
Ukija kutekwa ndugu zako watakuwa wanakulilia na kusiwe na wa kukutetea.
Kwa sababu ukipata mkate hiyo kwako inatosha sana,wengine shauri lao sivyo?
 
Sidhani kama CCM inaichukia Jamii Forum.
Kwa mfano toka JF imeanzishwa neno CCM limetamkwa mara nyingi sana,hivyo kuiwezesha CCM kukaa vizuri katika fikra za watu.
Moderators ebu tupeni takwimu ya kama ambavyo neno Israeli ilivyotamkwa katika kitabu kitakatifu Biblia,inayohusu neno CCM kutamkwa/kusemwa/kuandikwa katika jukwaa zenu mbalimbali.
 
Hii dhana ya CCM na Serikali yake kuuona huu mtandao ni hatari kwao ni ya kipuuzi Sana. CCM na Serikali mnapaswa muelewe jamii forum ina watu wenye IQ kubwa kuliko vile mnavyo dhani. JamiiForums sio kijiwe cha kahawa.

Huyu Musiba atashindwa hawezi kufanikisha ujinga wake dhidi ya JamiiForums. JamiiForums imeshaibua mambo mengi ya kuisaidia nchi.

JamiiForums si kijiwe cha kulazimishwa kumsifia mtu, humu tuna mawazo huru. Chonde Chonde CCM mkanyeni mtu wenu.

Kuendelea kuifatilia JamiiForums mnapoteza muda.
CCM wamewekeza kwa Musiba, wasiojulikana, police, msajili wa vyama na tume ya uchaguzi! Wakivuruga JF hawana la kupoteza maana fikra na maarifa kwao hayana faida. Tegemeo lao ni mabavu!
 
Back
Top Bottom