CCM mfukuzeni Jaji J.S.Warioba

CCM mfukuzeni Jaji J.S.Warioba

warioba usitiswe na mtu yeyote yule walitaka uwe fisad kama wao endelea kuonyesha ushupavu wako
 
Kama kweli mnaamini kuwa Jaji Warioba amewasaliti,mfukuzeni. Kama kweli mnaamini kuwa Jaji Warioba na Tume yake 'wamepika' Rasimu kwa chuki na hila zao na kuacha maoni ya wananchi kama mnavyodai,mfukuzeni chamani mwenu. Kama kweli mnaamini kuwa mnahitaji muda wa kutosha wa kumkashifu,kumtusi,kumsimanga na kumkebehi Jaji Warioba ndani ya chama chenu,Bungeni na kwingineko,mtimueni chamani kwa kumvua uanachama wake.

Mkifanya hivyo itakuwa poa. Mtakuwa na kila nafasi na muda wa kusema mtakayo juu yake. Wafuatiliaji wa siasa za nchi hii mnatuchosha. Tunawaona ni wa ndimi-mbili kuigiza kumponda Jaji Warioba wakati mnaye chamani.Na mnamheshimu kama Kada mkongwe na mtiifu kwa chama. Kama mmeweza kumfukuza Mansoor wa Kiembesamaki hivi karibuni,mnashindwa nini kwa Jaji Warioba.

Kama hamuwezi,mwacheni Jaji Warioba asimamie anachokiamini. Asimamie Maoni ya Wananchi aliyoyakusanya na Tume yake toka sehemu mbalimbali za nchi hii na kuyaainisha katika Rasimu. Msiendelee na kuonyesha mchezo wa kuigiza.

Kumbuka Mansoor amefukuzwa kutokana na chokochoko za Wanzanzibar wenyewe kuanzia CCM Mkoa, Kisonge mpaka ofisi kuu ya CCM Kisiwandui. Wakapeleka mapendekezo Kamati Kuu afukuzwe. Watanganyika wanaelewa wanachokifanya haijatokea na haitatokea hata siku moja Mtanganyika kufukuzwa CCM, kama unakumbukumbu waliofukuzwa CCM wote ni Wanzanzibar - Seif Sharif, Soud Yussuf, Mansoor. Wako wana CCM wa Tanganyika waliodai serikali 3 kwenye hadhara lakini hawakuekewa vikao, kukaripiwa au kufukuzwa.
 
NDANI YA CCM MWENYE AKILI NI MWENYEKITI BASI. SIKU JEYKEY AKIBADILI MSIMAMO ( NAAMINI ATABADILI TU KWANI UINGEREZA NA MAREKANI WALISHASEMA MAONI YA WANANCHI YAFUATWE BASI NAO WAO WATAFUATA TU) NA WENGINE WOTE WATAIMBA SANTURI HIYO YA JEYKEY....NDANI YA VIKAO WAJUMBE HUWA WANAPELELEZA SANA KUJUWA NINI MSIMAMO WA MWENYEKITI ILI KUEPUKA KUTOFAUTIANA NAYE...

KUMBUKA KWENYE KIPINDI CHA JENERALI ON MONDAY....MTAZAMAJI MMOJA ALISIKITIKA SANA KUHUSU MATUSI,KEJELI NA MIPASHO KWENYE BUNGE LA KATIBA. JENERALI ALISEMA ."....HIVYO NDIVYO VIKAO VYA CCM VINANYO ENDESHWA, NIMEYASHUHUDIA SANA NA KWA UHAKIKA HALI HUWA HIVYO NDANI YA VIKAO..."

JAJI WARIOBA KWENYE DK 45 (ii) ALISEMA RAIS ALIPEWA HABARI NA TAARIFA YA KILA HATUA YA MCHAKATO WA KATIBA NA MAUDHUI YA RIPOTI NZIMA. SASA NINI ANACHOKIFANYA SASA????
 
Mkataba ungevunja Muugano maana ingekuwa sawa na ilivyo East Africa Community. Na hadidu rejea zilisema Muungano uboreshwe na sio kuvunjwa.

Hivyo namna pekee ya kudumisha Muungano na kuondokana na kero za miaka 50 ni serikali 3, pendekezo ambalo linakubalika Zanzibar (badala ya serikali 2).

Sasa ndugu yangu kwani umesahau kwamba katika rasimu hii mpya kuna kipengele/kipindi cha mpito cha miaka minne(4) ambapo tutakuwa tunagawana Mali!sasa wewe unaona kuna muungano tena hapo? halafu lazima ujue kuwa kubadili mfumo wa kiutawala na kiutendaji wa nchi sio jambo Dogo na linahitaji ridhaa ya wenyewe wenye nchi ambao sasa ndio unaona tumegawanyika vipandevipande,Hapo ndipo tume ilipaswa kupendekeza ifanyike referendum kabla ya wao kuja na mfumo mpya(yaani baada ya kuona maoni yanaelekea kubadili mfumo wa nchi na ukizingatia muda waliokuwa wamepewa wao isingewezekana wao kupata maoni ya wananchi wengi).kuwa makini hapo kidogo ndugu yangu siasa weka nyuma kwanza.hivi wewe unafikiri Zanzibar kabla ya kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa,ingeundwa tume tu kama ya warioba na kuja na takwimu kwamba watu hawataki umoja huo,unafikiri kingeeleweka? ndio maana wakafanya referendum kwanza na ndio maana ukaona hakukuwa na shida katika lile japo kuna watu hawakutaka lakini utampigia kelele nani na referendum imefanyika?
 
Ninachofikiri Jaykei hataki serikali mbili anahitaji serikali tatu ila anahofia atagawanya chama kwanini ?
Kama asingetaka serikali tatu asingeruhusu itoke maana yake nini ? Angepitia na angezuia upitishwaji na uwasilishwaji wa rasimu ya pili ili isifike bungeni ikajadiliwe ambayo kimsingi anapingana nayo.
Hii inaonesha kuna baadhi ya watu kwenye chama wana nguvu hao ndio wanaotaka serikali mbili kwa matakwa yao.
Ila huyu aliwataadharisha wapokee chochote kitakachotokea hapa alikuwa alikuwa anawataadharisha wale wachache wanaotaka serikali mbili. Hapa JeyKei anajificha kwenye kivuli cha wapinzani kufikisha mawazo yake.
Nini kitatokea?
Serikali tatu lazima zipite huyo Nape anatumika ila inawezekana hajui kwa namna moja au nyingine. Ndio maana hawawezi kumuacha wala kumfukuza Jaji J S Warioba. Hilo ndio ninaloamini
 
  • Thanks
Reactions: MTK
tatizo la CCM ya leo inawatisha hadi wazee waliokulia ndani ya chama na kushika nyadhifa nyeti kama huyu mzee wetu.
 
Ukiondoa watu kama aina ya kina John Komba wenye akili mgando wanaofikiri kwa kutumia matumbo; hakuna mtu mwenye akili anayeweza kufikiria kumtimua Jaji Warioba halafu CCM ikabaki salama hata kidogo.
wataendelea kulalama tu hovyo; dozi Jaji kawapa wataendelea kuugulia na kugugumia tu na hawamfanyi kitu N'go!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nafikiri kwa mtazamo wangu jaji hakuwa pekeyake ktk kamati ni muhimu sasa uwekwe mjadala mmoja utakaojumuisha wajumbe karibu wote na kwa umoja waao watuambie wao wanaonaje m/kiti wao
kushambuliwa na wale waliowatuma na watoe msimamo wao hadharani .kwa maoni yangu mdahalo huo urushwe hewani na tv na redio zote bila ubaguzi ili watanzania wasikie mojakwamoja toka kwa iliyokuwa tume
 
NDANI YA CCM MWENYE AKILI NI MWENYEKITI BASI. SIKU JEYKEY AKIBADILI MSIMAMO ( NAAMINI ATABADILI TU KWANI UINGEREZA NA MAREKANI WALISHASEMA MAONI YA WANANCHI YAFUATWE BASI NAO WAO WATAFUATA TU) NA WENGINE WOTE WATAIMBA SANTURI HIYO YA JEYKEY....NDANI YA VIKAO WAJUMBE HUWA WANAPELELEZA SANA KUJUWA NINI MSIMAMO WA MWENYEKITI ILI KUEPUKA KUTOFAUTIANA NAYE...

KUMBUKA KWENYE KIPINDI CHA JENERALI ON MONDAY....MTAZAMAJI MMOJA ALISIKITIKA SANA KUHUSU MATUSI,KEJELI NA MIPASHO KWENYE BUNGE LA KATIBA. JENERALI ALISEMA ."....HIVYO NDIVYO VIKAO VYA CCM VINANYO ENDESHWA, NIMEYASHUHUDIA SANA NA KWA UHAKIKA HALI HUWA HIVYO NDANI YA VIKAO..."

JAJI WARIOBA KWENYE DK 45 (ii) ALISEMA RAIS ALIPEWA HABARI NA TAARIFA YA KILA HATUA YA MCHAKATO WA KATIBA NA MAUDHUI YA RIPOTI NZIMA. SASA NINI ANACHOKIFANYA SASA????

Mzee wa usafi a.k.a akili za TV,unahitaji msaada mkubwa sana,japo umemsifia JK lakini unashindwa kufuata nasaha,hekima na busara zake,na JK huyo huyo ndio alisema akili za kuambiwa/kusikia please changanya na zako,sasa wewe ukisikia tu kwenye TV unaandika JF,dah!matatizo sana,hatahivyo wewe na ndugu Yangu mmoja Hapo page ya kwanza ya Uzi huu anayeitwa HIMIDINI hamjui kwamba rais ni taasisi isitoshe hamjui utaratibu wa utendaji,mkisikia Rais alikuwa anapewa taarifa juu ya mchakato ulivyokuwa unaenda maana yake sio kwamba alikuwa anaulizwa kwamba Mzee tumeweka serikali tatu vipi inafaa? au hata yeye akiona eti aseme hapana hiyo toweni,basi ingekuwa ni rasimu ya Rais na hakukuwa na haja ya kuunda tume angetafuta watu wa ku-type maoni yake tu na angeiita ndio rasimu,hata ukisikia amesaini/amekabidhiwa rasimu,sio kwamba airekebishe bali hizo ni procedure tu, yaani ndio utaratibu tu,sasa mnaposhangaa ilipita kwake na hakuikataa ni kwamba sheria hazimruhusu kufanya hivyo.halafu wana CCM hawafuati mkumbo wanasimamia kitu kilichopo au sasa hivi kuna serikali 3? ila wewe na wenzako ndio mnafuata akili za mbowe na Lissu kwani kabla ya wao kuanzisha 3,hatukuwahi kukusikia Mzee wa usafi humu JF ukililia 3,sasa kama si akili za mbowe ni nini? halafu wewe na generali mmesahau kwamba nyinyi ndio mlianzisha kauli za uchochezi na matusi,NOTE: mbowe-nchi haitatawalika mpaka kieleweke,kibabu slaa naye-nchi haitatawalika,NASARI alianza matusi bungeni,JUSA-wawakilishi wameufyata, bi Aisha wa ccm akamjibu,WENJE- 201 wananjaa wamehongwa misosi,CHIKU AGWAO-bora tuue muungano tubaki na Tanganyika yetu,LIPUMBA-201 na ccm intarahamwe,hapo ya mnyika na sugu nimeyaweka pending,halafu eti ukawa wanasema wamekimbia matusi na vijembe,shame on you!
 
DEVAGY...naona una hasira na kila anaye kwenda tofauti na wewe...Mimi nimeripoti nilichosikia.sasa hebu nionyeshe ni wapi nimesama mambo ya Mbowe na Lissu?. Marehemu Jaji Nyalali alipotoa ripoti yake Mbowe na Lissu hawakuwa wanajulikana kwenye siasa za nchi hii lakini naye alisema serikali tatu. White paper ya Jaji Kisanga nayo serikali tatu, Jaji Warioba haye serikali tatu. Je nao ni wanachama wa Chadema? Mwakyembe mwanafunzi wa LLM naye alisema serikali tatu je naye ni mwanachadema? Tufike mahali tukubali Muungano wetu una matatizo ya kimsingi sio hizo changamoto na kero zinazo ripotiwa na serikali yetu.
Mbowe Lissu na wengine wenye mawazo tofauti nao ni watz na wana uhuru wa kuwa na mawazo tofauti na mtu yeyote. Na kila anayekuwa na mawazo tofauti si CDM wala mpinzani ndo ubinadamu huo, ninachopinga mimi ni matusi, kejeli na mapovu yanayotolewa na baddhi ya wajumbe wa bunge wa ccm....katiba haiundwi hivyo
 
devagy...naona una hasira na kila anaye kwenda tofauti na wewe...mimi nimeripoti nilichosikia.sasa hebu nionyeshe ni wapi nimesama mambo ya mbowe na lissu?. Marehemu jaji nyalali alipotoa ripoti yake mbowe na lissu hawakuwa wanajulikana kwenye siasa za nchi hii lakini naye alisema serikali tatu. White paper ya jaji kisanga nayo serikali tatu, jaji warioba haye serikali tatu. Je nao ni wanachama wa chadema? Mwakyembe mwanafunzi wa llm naye alisema serikali tatu je naye ni mwanachadema? Tufike mahali tukubali muungano wetu una matatizo ya kimsingi sio hizo changamoto na kero zinazo ripotiwa na serikali yetu.
Mbowe lissu na wengine wenye mawazo tofauti nao ni watz na wana uhuru wa kuwa na mawazo tofauti na mtu yeyote. Na kila anayekuwa na mawazo tofauti si cdm wala mpinzani ndo ubinadamu huo, ninachopinga mimi ni matusi, kejeli na mapovu yanayotolewa na baddhi ya wajumbe wa bunge wa ccm....katiba haiundwi hivyo

hakuna wa kuzuia serikali 3 .
 
Back
Top Bottom