CCM, Mchawi wako ni WEWE na wala sio CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, Mchawi wako ni WEWE na wala sio CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elli, Mar 5, 2011.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Wakati nikiwa mdogo nilishawahi kuambiwa kuwa, "mchawi wako ni wewe mwenyewe" kamwe sijawahi kuelewa maneno yale, lakini kadiri mambo yalivyokuwa yakibadilika kuna siku nililazimika kuamini usemi huo.

  Kwa hali ilivyo sasa, ni wazi kuwa CCM wanaiona CDM kama mchawi wao, shetani wao na kaburi lao, zaidi pengine kifo chao!! Siwalaumu hata punje, Simlaumu JK kwa kukimbilia kuwalaumu CDM, pia simlaumu Simba wala Chiligati si kwa vigezo tu vya kuwa kwao na elimu ndogo na kuzungumzia mambo makubwa lakini Wasira nae labda amesukumwa na Ukubwa wa umbo lake kutamka aliyoyatamka...ndio waswahili waaminivyo kuwa..."kama unaamini fulani ndio kakuroga...basi ukimuona mweleze ukweli kwamba wewe ndio mchawi wangu" na kwa kufanya hivi basi mchawi huyo hatakusumbua tena. Jamani, nani asiyejua adha ya uchawi?

  Timu ya CCM ikiongozwa na JK wako katika harakati za kumpa "Laivu" Mchawi wao ili asiendelee kuwaroga na kuwanyima usingizi, ni kweli kwa imani zao inaweza kuwasaidia lakini katika uhalisia wa mambo...tunajiuliza sisi majirani zao, kwa nini arogwe yeye tu? Kila siku asumbuliwe yeye tu na si mwingine? labda ni wivu...

  Baada ya kufanya ramli na tambiko kwa niaba yao, nimegundua kuwa CCM wala hawahitaji kunilipa hata senti tano, mimi nimeshamjua mchawi wao...na kwa kuwa sihitaji hata senti tano toka kwao nawaambia wazi kuwa...Mchawi wao ni wao wenyewe wakisaidiwa sana na kiongozi wao DOWANS, Richmond, IPTL na wajukuu kibao.

  Hivi kweli, Tanzania ya leo, usimpe mshahara mtu hadi leo ( refer tangazo lililowekwa NIT-Mabibo lenye ujumbe kuwa salary hadi 15th March) halafu unamdanganya kwamba yote haya ni kwa sababu ya fulani...huyu mtu atakuelewa kweli?

  CCM, ondoeni hiyo magogo machoni mwenu ili muweze kuoona vizuri vibanzi vya macho ya CDM, Vinginevyo, hata uimbe mchana kutwa na usiku kucha...kuna gharika inakuja, yes, Inakuja, I can see and feel it, si mbali, tunakaribia sana.
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ccm hawajui hilo kaka
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  CCM Out CCM Out CCM Out CCM Out, huyu kupe katunyonya muda mrefu sana sasa Rungu limmefikia anaweweseka sana, anaongea kama gadaffi, anatapatapa saana maji yemmfika shingoni, hiki chama si cha ridhaa ya wananchi sababu kiketawala kwa mabavu miaka yote hii tokea enzi za mfumo wa chama kimoja, CCm imetutia umasikini mkubwaa saana kutokana na viongozi wake kuwa wabinafsi mno, wanaopenda kujilimbikizia mali, kutojali wananchi na sasa hebu fikiria Rais anayetapeliwa kila kukicha, Rais asiye na nguvu za kukemea na kukamata wezi wa mali ya umma, Rais anayelinda mafisadi na wezi wa mali ya umma, Mawaziri wenye uchu wa utajiri wa haraka haraka mie sitaki kuzsikia upuuzi wa CCM hilo ni donda ndugu tulikatae CHADEMA HOYEEEE!!!!
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazo wangu naona dhahiri tungeendelea kutawaliwa na wakoloni tungekua mbali zaidi ya hivi vichache vizuri walivyofanya ccm na mengi mabaya, labda niwataarifu ccm mwisho wa ubaya ni aibu je mtu angemwambia mubaraki angekuja dhalilika ivyo angeamini?pia ata akifanya mabadiliko sasa they are too laite
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  CCM haaooooooooooooooo, maskini kama umande wa asubuhi kwenye jua
   
Loading...