CCM Mbozi yaanza kuwawajibisha madiwani wake

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225SAKATA la madiwani kutishia kumshushia kipigo Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo na Mwenyeykiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Erick Ambakisye limechukua sula mpya, baada ya Chama cha Mapinduzi wilayani humo kumwandikia barua diwani wake ya kumtaka ajieleze kutokana na kitendo alichokofanya kwenye kikao cha kutoa vitisho.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa barua hiyo yenye Kumb .Na. CCM/MBZ/VOL.1/112 ya Septemba 9 mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mwenezi wilayani hapa Clemence Mnkondya kwa imedai kuwa diwani kata ya Nkangamo Weston Simwelu alitoa kashifa kwa chama chake na kwa viongozi wa serikali ya wilaya ya Mbozi.

“Ulitoa maneno ya kashifa kwa chama chako cha mapinduzi na uongozi wake na uongozi wa serikali ya wilaya ya Mbozi pale uliposema; chukueni kikadi chenu cha chama cha mapinduzi sasa hivi, viongozi wa chama cha mapinduzi wa wilaya wote ni wanafiki na wajinga na mkuu wa wilaya ni mjinga na mpumbavu”ilisema sehemu ya barua hiyo.

Aidha kutokana na kukiuka kanuni za viongozi wa CCM ibara1.8 kabla hajachukuliwa hatua kali za kinidhamu kutokana na kashifa alizotoa kwa chama chake, viongozi na serikali yake ya wilaya anatakiwa ajieleze ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya barua hiyo.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Diwani huyo Weston Simwelu amekana kupokea barua hiyo, lakini hata hivyo amedai kuwa juzi alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu akimwarifu aende achuke barua yake, hivyo anadhani huenda ikawa ndiyo hiyo.

Simwelu alipoulizwa juu ya kutakiwa kujieleza alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni za baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya diwani anapofanya jambo lolote katika kikao cha baraza haruhusiwi kuhojiwa na chombo chochote.

Hata hivyo Diwani huyo alisema iwapo akipata barua hiyo atakuwa tayari kuijibu kwa mujibu wa kanuni husika ambazo alidai haziruhusu kuhojiwa.

Dalili za kutokuwapo amani katika vikao vya madiwani zilianza kuibuka Septemba 5mwaka huu katika kikao cha Kamati ya Mipango, Ujenzi na Mazingira diwani huyo alifanya fujo katika kikao hicho baada ya kutoelewana kwa hoja ya eneo la kuweka makao makuu ya wilaya mpya ya Momba na kusababisha polisi kuingilia kati kwa kuwashikilia madiwani wawili kwa muda

Ilipofika Septemba 7, mwaka huu wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani wakijadili eneo la kuweka makao makuu diwani huyo alionesha utovu wa nidhamu kwa kumpinga wazi wazi mkuu wa wilaya hii Gabriel Kimolo kutokana na kitendo chake cha kusoma barua ya chama chake ikiwa ni msimamo wa chama hicho kuhusiana na ajenda iliyokuwa ikijadiliwa.
Chanzo ni Francis Godwin.blogspot.com
 

Goldman

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
1,840
2,000
Hakuna ubaya ktk kupishana kauli na mkubwa wako wa kazi kama unasimamia ukweli na haki, na ni haki ya diwani kujieleza anavyojisikia, tuache mawazo potofu ya ndiyo mzee kila mkubwa wako wa kazi anapoongea.
 

NEW TANZANIA

Senior Member
Aug 15, 2011
101
0
nngu007;2505130
"Ulitoa maneno ya kashifa kwa chama chako cha mapinduzi na uongozi wake na uongozi wa serikali ya wilaya ya Mbozi pale uliposema; chukueni kikadi chenu cha chama cha mapinduzi sasa hivi, viongozi wa chama cha mapinduzi wa wilaya wote ni wanafiki na wajinga na mkuu wa wilaya ni mjinga na mpumbavu"ilisema sehemu ya barua hiyo.

Aidha kutokana na kukiuka kanuni za viongozi wa CCM ibara1.8 kabla hajachukuliwa hatua kali za kinidhamu kutokana na kashifa alizotoa kwa chama chake, viongozi na serikali yake ya wilaya anatakiwa ajieleze ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya barua hiyo.

kaisha watukana wanamuogopa nini?
kwanza kwa nini anawatukana watu wazima? yeye ni chizi?
ccm wekeni mambo sawa sio kufuata kanuni kwa watu wenye uchu/hasira za maendeleo tu hali wezi wanatembea huru

Simwelu alipoulizwa juu ya kutakiwa kujieleza alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni za baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya diwani anapofanya jambo lolote katika kikao cha baraza haruhusiwi kuhojiwa na chombo chochote.
hapa ndipo kwenye mgogoro chama kuingilia vikao vya serikali, ina maana kwa sababu ni diwani wa ccm basi hasionyeshe hisia zake kwa kuchoshwa na wizi na dhuruma za mafisadi

 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,555
2,000
Kwa vile kapewa nafasi ya kujitetea basi ajitetee ili kama ni ugali ikiwezekana umwagike kwa masirahi ya wapiga kura wake...ama ajiuzulu kama wa Geita ili ifahamike wazi kwamba hakubaliana na uzandiki wa chama chake cha kifisadi
 

Indume Yene

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
2,925
1,225
Inawezekana yeye alikuwa anasimamia maelekezo kutoka kwa wananchi ndo maana akatofautiana na Mkuu wa Wilaya ambaye alikuwa anasimamia msimamo wa chama chake cha Magamba. Sasa msimamo wa chama ni vipi ukaingizwe kwenye vikao vya halmashauri? Waacheni wananchi waamue wenyewe kuliko chama kuwaamulia. Hilo suala linamgusa kila mmoja hata wasio wanachama wa chama cha magamba.

Kwa msemo wa Rev. Lusekelo, inaonekana hata Mkuu wa Wilaya kichwa chake kina viroboto.
 

Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,483
2,000
hili la kusema '' chukueni kikadi chenu cha chama cha mapinduzi sasa hivi, viongozi wa chama cha mapinduzi wa wilaya wote ni wanafiki na wajinga na mkuu wa wilaya ni mjinga na mpumbavu " HALIVUMILIKI
Ndiyo yaleyale ya Shibuda kukifananisha chama chake na Mlenda ila hapa tuna subiri zaidi busara za CCM
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom