Elections 2010 CCM Mbeya Mjini yajipanga kukomboa jimbo 2015

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
CCM Mbeya Mjini yajipanga kukomboa jimbo 2015

Imeandikwa na Na Joachim Nyambo, Mbeya; Tarehe: 8th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 80; Jumla ya maoni: 0








BAADA ya kupoteza ushindi katika Kata 14 na hata Jimbo la Mbeya Mjini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa kimeanza mikakati ya kuhakikisha kinajipanga upya ili kurejea katika sura yake ya awali itakayowafanya wananchi kurejesha imani.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilayani hapa, Athanas Kapunga aliyasema hayo Alhamisi alipokuwa anatoa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa viongozi wa chama hicho uliowajumuisha pia wenyeviti na makatibu wa mashina, madiwani pamoja na viongozi
wa mitaa wanaotoka kwenye chama hicho.

Kapunga alisema wameona hakuna sababu ya chama ngazi ya wilaya kuanza kujihusisha na migogoro inayoonekana kuibuka katika ngazi ya za juu, wakati katika ngazi yao hawajashughulikia ile inayoonekana kukitafuna chama.

“Tumeona tuanze kwanza kutatua yale yanayokizorotesha chama katika ngazi yetu. Maana hayo ndiyo yaliyofanya tukapoteza jimbo na baadhi ya kata katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2010. Ukweli ni kuwa Wana- CCM wenyewe ndiyo waliohusika kuligawa jimbo kwa wapinzani. Sasa hatutaki haya yaendelee tukabaki kushabikia migogoro ya juu,” alisema.

Alibainisha kuwa makundi na kugeukiana ndiko kulikoifanya CCM iuone mwaka jana kuwa mwaka mbaya, lakini hali hiyo inapaswa kuchukuliwa kama fundisho kwa wanachama kuhakikisha wanajipanga na kuwa na umoja unaolenga kulinda maslahi ya chama chao.

Kapunga ambaye pia ni mstahiki Meya wa jiji la Mbeya, ameitaja mikakati ya kukirejeshea heshima chama kuwa ni pamoja na kuhakikisha vikao vya mara kwa mara vinafanyika katika ngazi za kata na mitaa ili wajumbe na wanachama kupeana taarifa za utekelezaji wa majukumu ya kila mmoja.

Alisema hatua nyingine ni kuhakikisha wanachama wanakuwa wafuatiliaji wa mambo yanayoendelea kwenye maeneo yao ikiwemo utatuzi wa kero za wananchi pamoja na kuufahamisha uongozi wa juu wa chama juu ya kero zinazozikabili jamii zinazowazunguka.

Alisema wanachama kuacha uoga wa kutaja yale yaliyotekelezwa na serikali ikiwa ni katika utekelezaji wa Ilani ya chama ni jambo jingine ambalo litakisaidia chama kwa kiasi kikubwa
kwa wananchi kujua nini kimefanywa na kipi bado, lakini lini kitatekelezwa.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Mbilinyi `Mr II’ au `Sugu’ alinyakua ubunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu, Benson Mpesya wa CCM.
 
PHP:
Kapunga alisema wameona hakuna sababu ya chama ngazi ya wilaya  kuanza  kujihusisha na migogoro inayoonekana kuibuka katika ngazi ya za  juu,  wakati katika ngazi yao hawajashughulikia ile inayoonekana  kukitafuna  chama. 
 
"Tumeona tuanze kwanza kutatua yale yanayokizorotesha chama katika   ngazi yetu. Maana hayo ndiyo yaliyofanya tukapoteza jimbo na baadhi ya   kata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 
2010. Ukweli ni kuwa Wana- CCM wenyewe ndiyo waliohusika kuligawa  jimbo  kwa wapinzani. Sasa hatutaki haya yaendelee tukabaki kushabikia   migogoro ya juu," alisema.

Wrong answers................................kama CCM Makao Makuu inaendeleza dhuluma dhidi ya taifa hili hakuna ambalo ngazi ya mkoa au wailaya italifanya kukinusuru chama kwenye ngazi tajwa.................................samaki mmoja akioza wote wameoza........................
 
Wataendelea kutupa ushindi tu kadri siku zinavyokwenda, CCM hii inayomtegemea tambwe hiza c'mon CCM muwe serious kidogo Makamba kabsaaa naye ni safu ya ushindi, ndo maana hamtaki katiba ibadilishwe mnaogopa kutoka madarakani, Mbeya hampawezi tuachieni sisi!!
 
Huyo Athanas Kapunga ni hopeless kabisa. Ameshindwa kuletwa maendeleo jijini Mbeya, na bado anang;'ang'ania kuongoza.
 
Mbona sasa walishachelewa ?hawawezi tena maana umangi meza wao umepatiwa dawa na CDM...wajipange kupoteza mkoa mzima
 
Wanaweza komboa jimbo lakini sio kupitia kwa mafisadi kama kina kapaddy. Ingekuwa kura inapigwa na wananchi watu kama hao wangetupwa nje. Ndio wamemponza Mpesya mpaka kapoteza nafasi nzuri aliyoishika kwa umakini sana. Kwa ujinga wake Mpesya aliwaamini na kuwategemea hao na kushindwa kuwakemea. CDM itaendelea kutesa ikiwa sauti za vihongwe zitaendelea kuchefua masikio ya wananchi.
 
CCM kwanza wajiulize kwa nini wanachama wao hawalipi ada za uanachama lakn wanavaa mashati, fulana na suruali za bure.. na wakati wa kampeni mabango ya gharama na vipindi kwenye TV hizo fedha zote hizo zinatoka wapi wakati ada ya uanachama hailipwi? CCM imejikita mpaka kwenye mashina (wajumbe wa nyumba kumi), na hao viongozi wote kama makatibu wa mashina, matawi, wilaya, mikoa etc pamoja na makatibu wa uvccm, uwt, wazazi n.k. wanalipwa mishahara na posho pamoja na magari yao HardTop!!! Je, ni kweli hii ni fedha ya Ruzuku tu!!??? CCM kwa kweli haiwezi kujitofautisha na UFISADI ndio maana mabwege kama kina Tambwe Hiza wanakimbilia huko...
 
wananchi wa mbeya mjini naomba kama mnaipenda nchi yenu msiwaonee huruma ccm,mkijaribu tu kuwapa madaraka kiukweli watawatolea uvivu,sisi tuliopo makao makuu ya nchi tunaona maovu wanayofanyiwa watu wa dodoma.hawa ndo wanaolinda rasilimali za makao makuu ni noma je nyinyi itakuwaje,acheni woga hii ni dhambi kubwa sana duniani,chadema juu na ni nguvu ya mabadiriko tanzania.
 
Back
Top Bottom