Ndugu wanajumuia na wana ccm;
Rejeeni taarifa ya bwana Frank Msigwa aliyoitoa Jan. 11. 2011 ambayo kwa mara nyingine tena imezua mtafaruku mkubwa kwenye jumuia yetu yenye amani.
Ni kutokana na mtafaruku huo na ukweli kuhusu taarifa hiyo ndio iliyonifanya nije mbele yenu wanajumuia kutoa ufafanuzi baada ya kuomba radhi kwa mtafaruku huo.
Kama kiongozi wa Tawi hili la CCM napenda kuwaomba radhi wanajumuia na wana CCM kwa yote yaliyotokea na kwamba nitaendelea na jihada za kutosha kuzuia mambo kama haya yasitokee tena.
Kuhusu ukweli wa taarifa hiyo ya bwana Msigwa ni kwamba pamoja na mapungufu makubwa yaliyo katika taarifa hiyo, HAKUNA MAKUBALIANO YOYOTE yaliyofikiwa katika mgogoro huo ingawa kuna jitihada za dhati za kumaliza mgogoro huo.
Mwisho nawasihi wanachama wote wa CCM ambao mmesha jiunga na ccmgroup kutumia mtandao huo kwani kutumia mtandao wa THC kunawakwaza wenzetu ambao si wanachama wa ccm. Na kwa wale ambao hawajajiunga tafadhari fanyeni hima kujiunga ili kujua kinachoendelea na kutoa maoni yenu kwa nafasi bila woga.
NB: TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE ccm groups mapema iwezekanavyo,
Michael Ndejembi
Mwenyekiti
CCM - Marekani.