Hii ilifanyika toka jana(jumamosi) ila umeme ulikatika nikashindwa kuwaletea taarifa kutokana na desktop yangu kuzima. Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Fransis Chaula, mwenezi ni Tito Sovela na mjumbe wa mkutano mkuu ni Onna Nkwama(aliwahi kuwa mwenyekiti wa council,akapigwa chini udiwani kwa kashfa za matumizi mabaya ya mali za umma). Kama kawaida ya siasa, majungu ya hapa na pale yalikuwepo kiasi cha kufanya wajumbe wabaki bila msimamo wa kueleweka. Source ni mimi mwenyewe.