Yawe
Member
- Apr 5, 2013
- 47
- 2
Ukiangalia kwa jicho la juujuu Ni vigumu kugundua machafuko yaliyopo ndani ya chama cha kijani na hii inasababishwa na hali iliyodhahili kwamba Chama hiki kwa sasa Hakuna mwenye Sauti Kama ilivyokuwa Wakati wa marehemu baba wa Taifa mwl Julius kambarage Nyerere, Chama lilikuwa kina nidhamu kwani kilikuwa na mshauri na Mtu makini ambaye alichukua mad mrefu kukemea Watu ovyo ndani ya Chama na mkweli kuhusu matatizo mazito yaliyokuwako ndani ya Chama.
Mwalimu alikuwa Ni baba mwenye nyumba na mmiliki nyumba iliyoitwa (CCM) kitu ambacho kilimfanya kuwa na ujasiri kusema Jambo lolote hata likiwa gumu kiasi gani, kwa sababu ya gharama aliyoitumia kuboresha nyumba ikiwa Ni kuweka msingi, kupandisha hata kutia bati na kuweza kuhamia ikiwa imekamilika, aliweza kuendelea kuboresha siku hadi siku kusudi nyumba iwe na hadhi ya kukaribisha wageni na hata kuweza kiwasitiri watoto waliopo ndani wasinyeshewe na mvua.
Baada ya kuondoka baba WA Taifa kwenye nyumba na kiwaachia walezi ambao sijua Kama wanajua gharama ya nini kilifanyika Wakati WA ujenzi, wamekuja na kuanza kung'oa Milango, madirisha, vitasa, kutoa vitanda na fenicha zote na sasa wengine wanamalizia kuchukua mabati yaliyobaki.
Ukiwa nje na hata ukiwa ndani Ni sawasawa na kuishi nje, kwani mvua itakunyea tu.
Malumbano yaliyopo ndani Ni rahisi kuona sasa Kila mmoja anaona anaweza kujenga na hii itasababisha ugomvi Mkubwa kiasi kwamba kuna uwezekano kwamba kufika 2015 sijui Kama kutakuwa na usalama kwa wana CCM maana hutajua umrushie ngumi nani maana wote mna jezi Za kijani na njano????????
Kazi bado ipo na ugomvi unanukia sana.
Fungueni macho muone