Ccm kutuletea mwana mipasho kawe maanake nini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm kutuletea mwana mipasho kawe maanake nini??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Oct 5, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Jamani sijui nakosea am a la
  yaani kuna huyu ant jaman nimekuwa nikisikiliza mikutanio yake yaani sijui nasema
  na ashukuru amepita kwenye chama cha ccm else uchaguzi ungekuwa mgumu maisha upande wake..anyway najua kupita atapita lakini dada yetu hata kujieleza mwenyewe awezi sasa najiuliza hivi huko bungen ataimba mipasho ama lah

  nikiangalia kwa sura kajitahidi kujichubua lakini sijui ana malengo gani kuingia siasa unajua kule dodoma kuna kazi nyingi sana wengine wana kazi maalum kuwepo mjengoni so sitshangaa akiwa mmoja wao...anyway nakutakia la kheri mama ila jitahd ukiwa na familia ujileeze kabla ya kuja kwa watu
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Na Mwandishi Wetu
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Angela Kizigha ametupiwa skendo nzito ya kummaliza, zikisambazwa nyaraka za kisheria za madai ya nyumba.

  Skendo hiyo, inaenezwa kupitia nyaraka za mahakama, hati ya hukumu na barua za wakala wa ubomoaji ambazo zinasambazwa jimboni kwake bila kujulikana lengo la msambazaji huyo katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu 2010.

  Ijumaa Wikienda, lilipata nakala hizo katika eneo la Tegeta, Dar Jumatano iliyopita lakini katika kuoneshwa kwamba zinaenezwa kwa kasi, siku hiyo hiyo lilipokea taarifa kwamba zipo nyingine zilikuwa zinagawiwa Kawe.

  Kikundi kidogo cha vijana, walikuwa wakisoma nyaraka hizo Tegeta jirani na Soko la Nyuki, lakini mwisho wa mapitio yao, walianza kuhojiana sababu ya nyaraka hizo kusambazwa kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu.

  "Haya mambo ni kuchafuana. Mimi naona hakuna kitu. Sasa hivi tunahitaji kusikiliza sera badala ya kashfa za pembeni," alisema kijana aliyefahamika kwa jina la Bonny lakini mwenzake anayeitwa Judu alijibu: "Kiongozi uadilifu, haya mambo ni vizuri kuyaweka akilini."
  [​IMG]
  Kwa mujibu wa nyaraka hizo, Angela alikuwa anadaiwa na mwanamke anayejulikana kwa jina la Diwani Hussein katika shauri namba 53 la mwaka 2002.

  Kesi hiyo, ilisikilizwa kwenye Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi Mkoa wa Dar es Salaam, Ilala Boma na ikaamuliwa kwamba Angela amlipe Diwani madai yake na hati ya hukumu hiyo ilisainiwa Aprili 25, 2005 na Makamu Mwenyekiti, A. L Kabuta.

  Mbali na hati hiyo, pia nyaraka zingine ambazo zinasambazwa na gazeti hili kuzinasa ni barua ya Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi Wilaya ya Kinondoni kwenda kwa Wakala wa ubomoaji ambaye ni Mwangati Auction Mart ambaye alitakiwa kumhamisha Angela kwenye nyumba ya Diwani.

  Nyaraka nyingine ni kutoka kwa wakala, Mwangati kwenda kwa Mwenyekiti Baraza la Ardhi, Nyumba na Makazi Wilaya ya Kinondoni, likimueleza kuwa agizo la kumhamisha Angela wamelikamilisha.

  Baada ya kuona nyaraka hizo, gazeti hili liliwasiliana na Angela ambaye alikiri kuzifahamu lakini akadai kuwa hizo zinasambazwa kwa lengo la kumharibia katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu.
  "Haya ni mambo ya uchaguzi, najua siasa. Hilo shauri nalijua lakini halipo kama taarifa hizo zinavyosambazwa," alisema Angela na kuongeza:

  "Ukweli ni huu, hilo shauri mimi nadai, halafu mimi sikuwa mpangaji wa huyo mama Diwani, waliokuwa wanakaa pale ni wadogo zangu. Huyo mama nimempeleka mahakamani namdai pesa nyingi.

  "Mimi sishindwi kumlipa, tatizo mimi ndiye namdai. Kama ni yeye kaamua kusambaza hizo nakala lakini ukweli mimi nadai. Kwa wananchi wangu wa Kawe, wakae mbali na uzushi wa namna hii, wasikilize sera za wagombea, wajue nini ambacho nitawafanyia nikiwa mbunge."
   
Loading...