CCM kutoweka kabla ya 2020?

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Kuna dalili ya CCM kutoweka kabla ya 2020 umaarufu wa chama hicho umeshuka kwa kiasi kikubwa imefikia hatua hata wanachama wa chama hicho wamegoma kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali.

Kutoonekana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho kimeongeza mashaka makubwa kwani tulitegemea Katibu Mkuu huyo kuanza kusimamia shughuli za chama hicho haswa katika matayarisho ya uchaguzi mbali mbali wa chama hicho mwaka huu.

Tumesikia huko Tanzania visiwani ndio hali ya chama hicho napo si kizuri.
Taasisi za CCM kama Umoja wa Wanawake na Umoja wa wazazi hauna wenyeviti, kikosi cha kupiga muziki cha TOT kimesambaa.

Jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyosimamia uchumi na kuleta maisha magumu hata kwa wana CCM. Serikali kuu kupora madaraka ya halmashuri na manisipaa na kupelekea makada wengi wa chama hicho kuona machungu.

Huwezi ukawa Virus and then Virus hiyo ikatumika kama tiba. CCM ndiyo imeifikisha Tanzania kwenye hali hii ya kimaisha na haiwezekani CCM hiyohiyo ikawa ndio tiba ya kuwaletea wananchi maisha bora unless tuwe na katiba mpya.
 
Hili ombwe linazidi kuongezeka wapinzani nao hili ombwe hawalioni sijui hawauju mchezo wa judo.
 
Kunana dalili ya CCM kutoweka kabla ya 2020 umaarufu wa chama hicho umeshuka kwa kiasi kikubwa imefikia hatua hata wanachama wa chama hicho wamegoma kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali.
Kutoonekana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho kimeongeza mashaka makubwa kwani tulitegemea Katibu Mkuu huyo kuanza kusimamia shughuli za chama hicho haswa katika matayarisho ya uchaguzi mbali mbali wa chama hicho mwaka huu, tumesikia huko Tanzania visiwani ndio hali ya chama hicho napo si kizuri.
Taasisi za CCM kama Umoja wa Wanawake na Umoja wa wazazi hauna wenyeviti, kikosi cha kupiga muziki cha TOT kimesambaa. Jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyosimamia uchumi na kuleta maisha magumu hata kwa wana CCM. Serikali kuu kupora madaraka ya halmashuri na manisipaa na kupelekea makada wengi wa chama hicho kuona machungu.
Nijuavyo Katibu Mkuu ni selule kule kwa Malkia ninasikia anauuguza majeraha yasiyosikia dawa kwa hiyo mustakabali wa chama chake hauna uhusiano naye.

CCM haiwezi kupoteza leo au kesho hadi ipokonywe dola. Mkate utokanao na CCM kukamata dola ndiyo mtaji wao wakiukosa huo wengi wao watakikimbia chama chao maana mkono mtupu haulambwi.
 
Ni bahati mbaya kuwa mleta uzi ametumia hisia zake za muda huu ku-predict CCM ya sasa na baadaye. Anajichosha. Tathmini ya chama cha Siasa inagaliwa katika mambo Mkuu manne.
Kwanza, uwezo wa chama kitaasisi (functioning party organs - kwa kipimo hiki CCM bado ni imara)
Pili, uwezo wa chama kiutendaji kupanga na kutekeleza sera zake (party operational assessment - kwa kipimo hiki CC bado ni imara)
Tatu, uwezo wa chama kiitikadi na kuonekana bayana kwa watu (party visibility - kwa kipimo hiki CCM bado ni imara - inaonekana, wanachama wapya (vijana) wanajiunga nacho); na
Nne, uwezo wa chama kukusanya rasilimali kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ya kisiasa ( kwa kipimo hiki CCM bado ni imara).

Sasa iwapo upinzani unadhani umefika popote katika milestones za maendeleo ya vyama vyao, basi wajipime katika vipimo hivyo vinne kuijangalia viko wapi. Hisia za kujifurahisha bila kutumia vigezo vya kisayansi ni wehu tu.
 
CCM Ipi?
Unaishi Nchi gani?

Mkoa wa Kusini Unguja kadi za kugombea uongozi ndani ya ccm zimesuswa, Mkuranga, Rufiji, na Kibiti, pamoja na wilaya jirani ya Kilwa zimesuswa. Hii ni nchi gani. Upo hapo Lumumba unakunywa Kahawa hujui hata kinachoendelea ndani ya chama chako.

Pigo kubwa ni hao wafanyakazi 10,000, ambapo kibongobongo mmoja anategemewa na wengine 10, so 10 times 10000= 100,000/=. Hizo lazima sisi ccm tuzikose tu popote. Maana wenye vyeti feki wameachwa wapete na kula kodi zetu, dagaa wote wametimuliwa.

Na hili suala wananchi huku kijijini halijaeleweka, kinachojulikana ni kuwa wamefukuzwa kazi. Sikia hii wamefukuzwa halafu zahanati haina watumishi imefungwa na ndio ilikuwa tegemeo lao, Mkurugenzi hawezi kumpeleka mtu kuziba pengo maana ukimuhamisha mtumishi ni lazima alipwe kwanza kabla ya kuondoka, so what next.

Ni kilio na kusaga meno kwa kyama kyetu kya mapindusi.
 
Ni bahati mbaya kuwa mleta uzi ametumia hisia zake za muda huu ku-predict CCM ya sasa na baadaye. Anajichosha. Tathmini ya chama cha Siasa inagaliwa katika mambo Mkuu manne.
Kwanza, uwezo wa chama kitaasisi (functioning party organs - kwa kipimo hiki CCM bado ni imara)
Pili, uwezo wa chama kiutendaji kupanga na kutekeleza sera zake (party operational assessment - kwa kipimo hiki CC bado ni imara)
Tatu, uwezo wa chama kiitikadi na kuonekana bayana kwa watu (party visibility - kwa kipimo hiki CCM bado ni imara - inaonekana, wanachama wapya (vijana) wanajiunga nacho); na
Nne, uwezo wa chama kukusanya rasilimali kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ya kisiasa ( kwa kipimo hiki CCM bado ni imara).

Sasa iwapo upinzani unadhani umefika popote katika milestones za maendeleo ya vyama vyao, basi wajipime katika vipimo hivyo vinne kuijangalia viko wapi. Hisia za kujifurahisha bila kutumia vigezo vya kisayansi ni wehu tu.
Suala kubwa la serikali iliyopo madarakani ni uchumi. Katika kuendesha uchumi wa nchi hii CCM imeonyesha imeshindwa kabisa. Wananchi watapiga kura kufuatana na hali halisi ya uchumi sio utendaji wa ndani wa CCM. Haiwezekani leo serikali iliyopo madarakani kushindwa kulipa hata umeme wa mahospitali halafu bado utuambie CCM ni chama bora.
 
Sina hakika iwapo unawasilisha maoni yako au unafanya tathmini kisayansi. Hata ukiangalia kwa haraka; masuala ya hospitali kukatiwa umeme yanategemea longevity na kuelewa zaidi kuliko kuguswa. Hapa utahitaji kupata ratio baina ya wanaotambua kuwa umeme kwenye vituo vya afya na mahospitali ni issue kubwa dhidi ya wale wasioona kuwa ni issue. Pili, unatakiwa kujua kuwa hivyo vipimo vinne nilivyoainisha awali kutathmini uwezo wa chama cha siasa vina-impact kwenye daily politics na maamuzi ya wananchi wakati wa uchaguzi kukichagua chama 'wanachokijua'. Kama kuna chama kinadaiwa kufanya vibaya lakini wananchi wanakiujua dhidi ya chama 'kinachofikirika' kuwa 'kinaweza kufanya vizuri', lakini wananchi 'hawakijui', unadhani rational voter atachagua chama gani? Obviously the former! Opposition hapa nchini ume-mess up, period. Umehagua quick wins political project hivyo ku-avoid [badala ya] comprehensive, time consuming, heavy and complicated political reform project.
 
Kunana dalili ya CCM kutoweka kabla ya 2020 umaarufu wa chama hicho umeshuka kwa kiasi kikubwa imefikia hatua hata wanachama wa chama hicho wamegoma kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali.

Kutoonekana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho kimeongeza mashaka makubwa kwani tulitegemea Katibu Mkuu huyo kuanza kusimamia shughuli za chama hicho haswa katika matayarisho ya uchaguzi mbali mbali wa chama hicho mwaka huu.

Tumesikia huko Tanzania visiwani ndio hali ya chama hicho napo si kizuri.
Taasisi za CCM kama Umoja wa Wanawake na Umoja wa wazazi hauna wenyeviti, kikosi cha kupiga muziki cha TOT kimesambaa.

Jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyosimamia uchumi na kuleta maisha magumu hata kwa wana CCM. Serikali kuu kupora madaraka ya halmashuri na manisipaa na kupelekea makada wengi wa chama hicho kuona machungu.

Huwezi ukawa Virus and then Virus hiyo ikatumika kama tiba. CCM ndiyo imeifikisha Tanzania kwenye hali hii ya kimaisha na haiwezekani CCM hiyohiyo ikawa ndio tiba ya kuwaletea wananchi maisha bora unless tuwe na katiba mpya.

Wewe bado unaota mchana sio?
 
Back
Top Bottom