Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Naendelea kuamini kuwa CCM ni mfumo ulioshindwa katika utawala wa nchi hii. CCM kama chama kimekuwa na tabia ya kulindana na kuchekeana hata pale viongozi wa umma na wa kichama wanapokiuka sheria na taratibu za nchi na chama. Wapo viongozi wa umma waliokumbwa na kashfa za wizi/ufisadi wakiwa madarakani. CCM ikaishia kuwashurutisha waachie ngazi na mambo yakaishia hapo.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kushtaki akabaki kimya na viongozi husika wakaendelea kutesa uraiani.
Leo hii katika mchakato wa kumpata mgombea wao,makada wa CCM wanatishana. Wanatishana kwakuwa makada hao wanajiona na kuaminisha wananchi kuwa wao ni watu safi kwakuwa tu hakuna kumbukumbu ya mashtaka dhidi yao. Kule kuchekeana na kulindana ndiko kunakowafanya makada hao watambe sasa na kutishia hata uhai wa chama.
Eti hadi mtuhumiwa wa ufisadi leo anakitisha chama chake? DPP angeshamaliza kazi kwa kumburuza mahakamani leo hii asingekuwepo hapo kutishia kuwa akikatwa jina patachimbika.
Nasema tena na tena CCM ni mfumo ulioshindwa na hauwezi tena kutupa Rais mwenye mapenzi mema kwa watanzania. Naye ataanzia kwenye kulindana na kuchekeana na kuishia hapa kwenye kutishana. Muda wa maadiliko ya kimfumo ni huu watanzania wenzangu.