Pole sana mkuu, hii ndiyo JF!Mkuu umeniacha solemba
Siyo lazima kuondoka kwake iwepo nguvu toka nje yake, itajisambaratisha yenyewe sababu ya kugombea madaraka na maslahi1. Tume ya uchaguzu inachaguliwa au kufutwa kazi na mwenyekeiti wa CCM
2. Msajili wa vyama vya siasa huteuliwa au kufutwa kazi na mwenyekeiti wa CCM
3. Rais ambaye ni mwenyekeiti wa CCM ndiye anatafuta pesa za uchaguzi
4. Jaji mkuu anateuliwa na kufukuzwa kazi na mwenyekeiti wa CCM
5. Mkuu wa majeshi anateuliwa na kufutwa kazi mwenyekeiti wa CCM
6. Wakuu wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama huteuliwa na kufutwa kazi mwenyekeiti wa CCM
7. Baraza la mawaziri huteuliuiwa au kuvunjwa na mwenyekeiti wa CCM
8. Wabunge wa CCM hupitishwa na mwenyekeiti wa CCM kugombea ubunge
9. Jina la spika kugombea uspika hupendekezwa na mwenyekeiti wa CCM na kupigiwa kura na wanachama waliopitishwa na CCM. Wakipingana na mwenyekiti mwenyekiti wa CCM anaweza kulivunja bunge tukaanza upya.
10. Wakuu wa wilaya,wakurugenzi, wakuu wa mikoa, RAS huteuliwa na mwenyekiti wa CCM.
11. Mchakato wa katiba mpya mpaka uitishwe na mwenyekiti wa CCM.
Kwa mtazamo wangu kuitoa CCM madarakani haiwezekani
😉 NGUME KUMEZA
Kama afanyavyo Biden wa USA au Putin wa Urusi au Malkia wa UK!?Anabadiri kofia lkn mtu ni yule yule hakuna check and balance
Huoni kama Nchi hii itaingizwa kwenye machafuko kama yale ya Tigrai.Kwa mfumo ulivyo katiba ni ngumu kuipata kwa sababu mpaka mwenyekiti wa CCM aamue km hisani.
Shikiria BAADHI!Marekani baadhi ya nyazifa mpaka bunge la masenata lilipishe.
Hebu soma historia ya Nchi zilizoingia kwenye machafuko Barani Afrika halafu tafakari.Machafuko yatatoka wapi wakati dola ipo chini ya Chama tawala, ukifanya fyoo ndani miaka kadhaa, kwani kesi zipo nyingi.
Sio kazi ya Raisi,ni jukumu la kila Mwananchi Wanajeshi na Polisi hawazidi laki tatu wakati kuna mamilioni ya Wananchi.Ukumbuke kuwa kazi kubwa ya Rais ni kulinda amani ya nchi.
Soma historia ya Ivory Coast iliyokuwa na Wananchi wapole kuliko Tanzania.Si kwa sisi watanzania wa leo labda baada ya miaka 100.