Kwasasa nimegundua kuna tatizo kuwa kila anayeshabikia serikali tatu au sera au hoja ambayo imeshasemwa na ccm basi huyo ni mwana ccm. Na wale wanoshabikia kuitukana ccm basi wao ndiyo watanzania. tunaipeleka wapi hii nchi?
UKAWA isiporudi bungeni jumatano basi nitaamini kile nilichoambiwa na mtu mmoja kuwa UKAWA ndiyo chanzo cha kifo cha chadema. Sababu alizotoa ni kwamba chadema wasipoingia bungeni, ngo inayo walipa kila mwana ukawa shilingi za kitanzania 450,000/= zinazotolewa na ngo fulani inayoitwa Konrad-Adenauer-Stiftungkwa kifupi KAS itafungiwa kufanya shughuli zake hapa nchini kwa kusababisha mgogoro wa kidiplomasia na kwenda kinyume na sheria za nchi. Kisha itakua vigumu kuwalipa wana ukawa na hivyo baadhi yao kulazimika kurudi bungeni ili waambulie angalao kidogo kuliko kukosa kabisa, kitu ambacho kitazua mgogoro ndani ya vyama hasa chama chenye wabunge wengi wa bara ambacho ni chadema. Kwanini siyo CUF maana ina wabunge wengi kwa nchi nzima zaidi ya chadema? anajibu kuwa Zanzibar ajenda yao iko wazi ni serikali ya mkataba na si serikali tatu na hivyo hawatakua na cha kupoteza.
Tujihadhari kabla ya shari. chadema muwe mnasikiliza mashauri siyo kujisukumiza tu kama wote ni kina sugu, lisu na lema.