CCM kumpongeza Trump ni unafiki

VIVIANET

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2015
Posts
2,129
Reaction score
2,922
Ndugu wapendwa sibahatishi kwa hiki ninachoandika, ninazo sababu tatu za kusema CCM kumpongeza Trump ni unafiki tena wa kifarisayo. Hapa USA wanachukia sana watu wenye tabia ya unafiki na ni moja ya sababu zilizomwangusha Bi Clinton maana walimuona kuwa mwongo ktk mambo fulani.

Sababu tatu za kusema CCM ni wanafiki

1-CCM hawaamini kuwa ni haki wapinzani kuchukuwa dola ila wenye haki hiyo ni chama tawala, kwahiyo kumpongeza mpinzani ni unafiki

2-CCM wanaamini kwamba mtu akipingwa na chama chake na akaanza juhudi zake binafsi kutafuta uongozi huyo ana uchu wa madaraka, Trump alipingwa sana na hata baadhi ya viongozi wakuu wa chama chake walitangaza hadharani kutokumuunga mkono ktk harakati zake za kuwania uongozi. Hakuna tofauti ya kupambana kwa Trump na Lowassa ila kwa CCM Lowassa ana uchu wa madaraka lakini Trump ni mpambanaji huo nao unafiki

3-CCM wanaamini mtu akihama chama chake kwenda kutafuta ungozi kupitia chama kingine ni makapi na hafai kabisa wamesahau Trump wanayempongeza leo alikuwa mwanachama wa Democratic tena mfadhili mkubwa kabla hajahamia Republican

Kwa sababu hizo nasema CCM kumpongeza Trump ni unafiki
 
na tukirogwa kupigia kura chama kingine nchi itageuka libya au iraq
 
Hata ukionyesha dalili ya kutenda haki na haki yenyewe iwe upande wa upinzani wanakutishia kukunyang'anya kadi kama walivyomtishia marehemu nanilii kumnyang'anya kadi kisa kuwapa uhuru wa kutoa hoja bungeni na kusimamia bunge live kipindi chake haya masisiemu NOMA sana hayafai 2020 tuyatupe kule ilipo KANU
 
TULIA ANASIKITIKA BI. CLINTON KASHINDWA, HAKUMBUKI HAPA TULIKUWA NA MGOMBEA URAISI MAMA ANNA KUTOKA ACT WAZALENDO

Muulize sasa Tulia alimpigia kura nani? Ningekuwa ndiyo raisi yule mama ningempa sector nyeti sbb anajiamini na mpambanaji

Ila kwa vile hana kadi ya ssm ameachwa
 
Just make a little research Trump alikuwa mwanachama wa Democratic part
 
Si unfiki hata kidogo kwa CCM kumpongeza Trump. Wameonesha rangi yao asili ya kidhalimu.Kumbukeni CCM bila aibu wala fedheha wamempongeza JECHA kwa ufisadi na dhulma alioifanya kwa wananchi wa Zanzibar tena mbele ya kadamnasi.
 
Unafiki tena kiwango cha Phd
 
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya nje kwa Mwamvuli wa Diplomasia ndio inatakiwa kumpongeza rasmi Rais Trump.

Labda CCM ituambie inapitia mwamvuli upi? Au ndio kujipendekeza au kuyakata makali ya sera zitakazo kuja kuitikisha Afrika au kwa ajili ya Demokratiki walivyotuchokora kuhusu suala la Zanzibari?
Wizara ya Mambo ya nje ya Marekali, sera zake za nje nyingi hazibadiliki. Miaka 4 sio hoja, Wamerekani wanapanga mbele zaidi ya miaka 300 ijayo.

Bado Tanzania kidonda cha kushirikiana na Israel kipo kibichi.
Hakuna anayepinga Mtu yeyote kudhuru Israel, Jerusalemu ardhi takatifu. Kila mmoja ana haki ya kwenda Jerusalemu. Hapa tunapinga wazi Awamu ya 5 kushirikiana na Wahalifu wa Kizayuni. Na hili sio suala la dini, hili ni suala la kibinaadamu. Hili suala ni endelezo la Wapiganiaji Mashuhuri wa Haki za Binaadamu hapa Afrika na duniani kote akina Nyerere, Nelson Mandela, Robert Mugabe na Fidel Castro.

Hatuwapingi Wa Israeli kwa vile wao ni Mayahudi na walimkataa Yesu.

Na ishitoshe walianzisha taifa la Israeli mwaka 1948 sio kizazi kitakatifu cha wana Israeli, hawa Wazayuni ni Wazungu bhana, sio Wamasai au Wasemeti. Tuwacheni kudanganywa kwenye hili suala la Utakatifu wa Israel. Hata sisi Waafrika leo hii ni Watakatifu. Tena sana.

Tunaipinga Israel kwa ajili ya tawala yake ya Kizayuni ya Kibaguzi iliyokuwa mbaya zaidi kuliko ile ya Makaburu. Awamu ya 5 kushirikiana na Israel itakuwaa ni tamaa tuu "opportunism" au kutojua nini thamani ya "Ubinaadamu". Mwalim Nyerere hawakuwa wajinga kuwapinga Wazayuni.

Pia Ushirikiano na Moroko ni shaka kubwa, wakati Western Sahara hawajapewa haki zao.

Israel na Morocco, wote hawa ni watu wana haha, wanatafua "weak links, opportunists and desperate Governements wanatengeneza uhusiano, nchi kama Afrika Kusini inayojua nini maana ya Ubinaadamu na nini maana ya kunyanyaswa wamewaekea vikwazo baridi Morocco na Israel.

Tuone aibu jamani, tuwe na msimamo. Tuweke Ubinaadamu mbele.
 
Unafiki kwa ccm no kawaida kabsaaaaaaa pole kama umechelewa kulifahamu hilo
 
Ccm wengi walikuwa wanamsaport Clinton, hata mkuu wa mkoa wa DSM alikuwa anampost sana insta nahc kafuta zile picha
 
Wapi Nimesema Lowassa Kajinyea? Nimesema Trump hakuwahi Kujinyea Jukwaani acha kunilisha Maneno bwa shee!

Huwezi kujua Umri wa Baba yangu Kama hujui Umri wangu acha kujifanya Mtabiri!
Ipo Siku wewe utajinyea mchana kweupeee, chunga mdomo ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…