CCM kumkomoa Masha kwa sababu alihama chama 2015 ni Ujinga mkubwa

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,859
Wengi mtakuwa mnajiuliza kwanini CCM walipiga kura za kukomoana jana kwa Wenje na Masha. Kubwa ninaloliona hapa ni visasi, vitisho kwa wana CCM wengine wenye nia ya kufanya siasa nje ya CCM na chuki za kijinga.

Pia ufinyu wa akili zao wamemkomoa Masha kwa sababu alihama chama wakati wa uchaguzi. Wanachosahau nafasi zile ni za CDM tu hata aridhi ipasuke. Walichosahau kingine Wenje na Masha wanaenda kuiwakilisha nchi na sio CDM au CCM wote pamoja na wale wa CCM baada ya kuchaguliwa ajenda yao kubwa inabaki ni nchi sio vyama.Nina wahasa chuki hazijengi ziku zote zinabomoa.

Wenje,Huyu walimkataa kwa kinyongo, Mtakumbuka amekuwa mwiba kwa CCM muda wote na ilifikia wakadhamiria yeye na Kafulila watawafuta kwenye siasa za nchi kwa gharama yoyote. Leo wametekeleza kisasi mbele ya kamera na macho ya watanzania bila aibu. Cha kusikitisha zaidi baada ya uhasi huu kwa taifa. Kesho CCM hao hao wakiongozwa na spika utawasikia wakisema tuweke utaifa mbele na uzalendo na si vyama vyetu.Utawasikia wakisema si kila jambo ziingizwe siasa, unafiki mkubwa.

Kwa hali hii kama taifa.Viwanda na uchumi wa kati tutabaki kusoma kwenye magazeti ya Kenya na Rwanda tu.Huku sisi tukirudi enzi za kikoloni na kujiona bado tuna uhuru wa kifikra na kiuchumi.
 
Hivi ni kukomoa au ni uchaguzi ambao kila mtu yuko huru kumchagua mgombea anayemvutia?Acha wacheze ngoma hiyo wenyewe sisi huku tunacheki tu
 
Kwa bongo hii mtu asikudanganye kusema eti tuweke itikadi za vyama pembeni!
Usije muamini atakuliza bure,hicho kitu kwa tanzania yetu kimeshindikana
 
Mbona masha na wenje? kwani CDM hakuna watu makini ambao wana weza kuliwakilisha taifa letu kwa weredi na si kupeleka watu ambao kazi yao ni kupinga tu hata kwenye mafanikio?
 
Jana jioni, kwa wagombea ambao kwa maoni yangu walikuwa the most qualified kutuwakilisha EALA wameshindwa kupata kura za kutosha kuwa wabunge.

*kuna mtu alitegemea matokeo tofauti?*

mm nilitegemea yaliyotikea yangetokea. Kwa jinsi siasa zetu zilivyo za kichama ilikuwa vigumu kwa Masha na Wenje kupata kura za Kutosha kutoka kwa Wabunge wa CCM... *tatizo ni chama chao na wala sio ugombea wao*

Hata Prof Kitila jana angekuwa anagombea kwa tiketi ya Chadema, kwasababu tu anatoka Chadema, angekosa kura za kutosha kama walivyokosa WeNje na Masha.

Kuna watu wanatajiribu kujenga hoja ati kutobalansi jinsia kumewacost... *mm nasema hakuna kitu kama hicho* tatizo wao ni chadema na kura za maamuzi zinatoka CCM..

Yani hata Ingekuwa Shilole wa ACT anashindana Na Zitto wa Chadema.....CCM wangempa kura Shishi na kumuacha Zitto wa Chadema....hili hata Zitto mwenyewe analijua vizuri..anajua partisan politics za Bungeni...ndiyo mana alikuwa na uhakika kama ACT wangeshindanishwa na wangombea wengine wa upinzani..hasa Chadema....mgombea wa ACT angepata kura nyingi zaidi kutoka CCM ambao ndiyo wanamfanya mgombea ashinde.


*Hapa ndipo tulipo fika*

Na huu ujinga upo hata hapa kindini. Yeyote ambaye ana maoni tofauti na maoni yenye mwelekeo wa kichadema...anaonekana adui. Atadhihakiwa atatukanwa kila aina ya tusi...ushahidi upo hapa hapa kundini.

Ndiyo mana i find it amusing, members wa hapa ambao ni mapartisan kupita kiasi..kiasi kwamba hawawez vumilia mawazo ya wengine..ati nao wanawashangaa CCM kutompigia kura mgombea bora kama Laurence Masha.


*hii aibu ya wote*
 
Kwenye uchaguzi wa EALA aliyeshindwa CHADEMA sio Masha wala Wenje bali ni dikteta Mbowe aliyedhani kuwa ana uwezo wa kugawa kila benefit iliyopo CHADEMA. Wabunge wa viti maalum hawapigiwi kura bali Mbowe na madikteta wengine wanawa-hand pick. Utashangaa mwanamke wala hafahamiki CHADEMA tena ni kiongozi ndani ya CCM anachaguliwa kuwa mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA. Aibu kubwa kwa chama kinachojinadi kuwa kinatetea democracy. Kwenye hili la EALA naye kaja tena ku-hand pick watu wawili mwingine hata miaka 2 ndani ya CHADEMA hafikishi. Wanaofahamika kukipigania chama kwa zaidi ya miaka hata 20 wanaomba lakini wala hawapigiwi kura ili ionekane hawakubaliki. Sasa dikteta anaamua lazima Masha na Wenje waingie EALA. Yaani anataka ku-dictate hata kwa bunge!! Hapa ikagonga mwamba. Mbowe lazima ajifunze udikteta una mwisho wake na pia aufanye kwa akili hata kama ni za kuambiwa.
 
Wengi mtakuwa mnajiuliza kwanini ccm walipiga kura za kukomoana jana kwa Wenje na Masha.
Kubwa ninaloliona hapa ni visasi,Vitisho kwa wanaccm wengine wenye nia ya kufanya siasa nje ya Ccm na chuki za kijinga.Pia ufinyu wa akili zao wamemkomoa Masha kwa sababu alihama chama wakati wa uchaguzi.Wanachosahau nafasi zile ni za CDM tu hata aridhi ipasuke.
Walichosahau kingine Wenje na Masha wanaenda kuiwakilisha nchi na sio Cdm au Ccm wote pamoja na wale wa ccm baada ya kuchaguliwa ajenda yao kubwa inabaki ni nchi sio vyama.Nina wahasa chuki hazijengi ziku zote zinabomoa.
Wenje,Huyu walimkataa kwa kinyongo,Mtakumbuka amekuwa mwiba kwa ccm muda wote na ilifikia wakadhamiria yeye na Kafulila watawafuta kwenye siasa za nchi kwa gharama yoyote.Leo wametekeleza kisasi mbele ya kamera na macho ya watanzania bila aibu.
Cha kusikitisha zaidi baada ya uhasi huu kwa taifa.Kesho ccm hao hao wakiongozwa na spika utawasikia wakisema tuweke utaifa mbele na uzalendo na si vyama vyetu.Utawasikia wakisema si kila jambo ziingizwe siasa.Unafiki mkubwa!
Kwa hali hii kama taifa.Viwanda na uchumi wa kati tutabaki kusoma kwenye magazeti ya kenya na Rwanda tu.Huku sisi tukirudi enzi za kikoloni na kujiona bado tuna uhuru wa kifikra na kiuchumi.
ushauri wangu chadema wawaache haohao wapigiwe kura tena,tuone kama kwenye hilo bunge la afrika mashariki watawapeleka hao saba bila wabunge wa chadema.
 
Mleta Hoja nazani umeingia nchini juzi tu...
Hebu anza kuifuatilia hii Sirizi tangu kabla Katibu Mkuu pendwa Dr Slaa hajaamua kupumzika Siasa...
Alafu uielewe dhana ya kuchenji gia hewani....
Ukimaliza na ukiwa umeelewa uje uufute huu uozo ulioandika
 
haya hao wateule wenu 7 hawaapishwi kuwasubiri wa CDM.
Kila mtu lazima apigiwe kura watake wasitake...hii ndio demokrasia yenyewe sasa mnajiita chama cha demokrasia na maendeleo halafu mnaogopa demokrasia? hata hapana nayo ni kura
 
Back
Top Bottom