Ccm kuingia Arusha muda si mrefu

KITENGE KOFIA

Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
35
Reaction score
24
Habari zilizopo ndani ya CCM Arusha zinadai kuwa muda si mrefu CCM ikiongozwa na mwenyekiti wao watatumia mwanya wa kufanya sherehe kwa mji wa Arusha kuwa jiji na kukabiziwa barabara kama njia ya kuwavutia wenyeji wa Arusha.

Inasemekana kuwa siku hiyo kutachinjwa ng'ombe wa kutosha mnajua wenyewe zitatoka kwa nani,ni hapo kwa rich wa monduli..mambo yote itakuwa hapo shekh amr abeid


karibuni muda utakapotangazwa,tutawajulisha
 
CCM walikuwepo Arusha tangu kuanzishwa chama na waliongoza muda mrefu. Waliborongwa, wakachokwa, wakakataliwa, wakalazimisha umeya, wakatumia vitisho na kuua ili wadhoofishe wapinzani, wakaharibu zaidi.

Waje wakiwa na mpango mpya, waje wakiwa na mapya ya kuwaeleza wananchi.

Wajue kuwa, mtu aliyekupenda akisema basi, inakuwa vigumu kumrudisha!

"What anger worse or slower to abate then lovers love when it turns to hate."

 
Yani nimecheka ghafla!! Kwa hiyo ccm inaingia arusha kwa gia ya n'gombe?wakati msosi wa buku kwa mama ntilie unapata ngombe ndani?labda wagawe tanzanite ndio wanaweza kidogo ku break news!ila nyama ya ngombe hapana.
 
Nadhani huyu Lowassa anatafuta ugonjwa wa moyo. Maana atakapouona ukweli huko tuendako atakufa kwa presha. Si hilo tu, laana ya pesa ya wizi ni kwamba ameingiwa na shetani wa kuutaka urais ili arejeshe pesa aliyoiba na afilisike ili afe kwa ugonjwa wa moyo.....Aaaamina.
Hivi hawa Connected Cabal of Mafioso wanadhani watanzania wa sasa ni wale wa mwaka 47? Maskini wanadanganywa na vijana na wanawake waliomo kwenye jumuia zao za aibu kuwa vijana wote ni nyemelezi kama akina Nape,Malisa, Shigella na makapi mengine! Mwaka huu itakula kwao watake wasitake waamini wasiamini.
 
Msiogope mbona kirumba Mwanza walichinja ng'ombe hamsini lakini wakapigwa chini.
 
Labda wamchinje Rich mwenyewe mbona nyama za ngo'mbe kila kona Arusha zipo tumeshazikinai
 
'CCM is direct proportional to Ubwabwa provided Uongo na Matusi are constant'
 
Duh awali kwani si ilikuwepo hapa A town ikadorora,hatudanganywi katu..A TOWN ni ngome ya cdm.
 
Waje tu hakuna shida ni kama mgeni akija kukutembelea huwezi kumkataza. Sema kabisa itakuwa lini ili niwaambie machalii wajiandae beche la bure.
 
Wanataka kufanya mazishi yao sio??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Labda wamchinje Rich mwenyewe mbona nyama za ngo'mbe kila kona Arusha zipo tumeshazikinai

Nimecheka sana kwenye thread ya maudhi. Ahsante MLERAI, nimeipenda sana hii post yako.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…