CCM kuendelea kuliumiza taifa ni kwa sababu ya Udhaifu,uoga na usaliti wa Upinzani!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,159
2,000
Kama kuna kitu ambacho tunashindwa kuelewa ni kwamba hata siku moja haitokaa itokee CCM wakakubali kuachia madaraka kuwaachia wapinzani, walishazoea kupigiwa saluti na kuagiza wanahofu na maisha ya uraiani, hawapendi kuja kua walalamikaji wakiwa wapinzani kama ilivyo kwa CHADEMA na CUF hivi sasa.Haitaki kabisa hali kama hiyo, wengine hata vyeti watakwenda wapi? Hili limejidhihirisha wazi kwenye Uchaguzi wa Rais kule Zanzibar 2015.Niliwahi kumsikia kiongozi mmoja wa chama flani akisema kuna mzee mmoja kiongozi kule SMZ alikua na mikopo ya mamilioni benki na alkua anaamini kua ataendelea kukatwa kwenye mshahara wake mkopo awamu nyingine kwa sababu alikua unajua watashinda tu, sasa aliposikia maalim Seif anaelekea kushinda basi ilikua azimie.


Mpinzani wa kweli haogopi vitisho pale penye ukweli, haogopi kufungwa jela na hata historia inasema hivyo kua wapinzani waliowahi kufanikisha mipango yao ya ushindi duniani. Leo mtu akiwekwa jela siku mbili tu anaanza kumuwaza mke wake pamoja na watoto wake, kesho unategemea akitoka atafanya fyoko? Hawaelewi kua siasa za upinzani ni zaidi ya mke ya wato, upinzani ni zaidi ya mayai na sambusa unazokula nyumbani.Tazama kina Mandela alikaa jela akiwa kijana akatoka akiwa mzee na akasalitiwa na mke wake lakini mwisho wa siku alifanikiwa kulikomboa taifa lake. Angemuwaza mke wake mrembo na sambusa za nyumbani basi mpaka leo makaburu ndio wangekua wakuu wawakilishi wa taifa hilo.


Upinzani kuendelea kuogopa kuzidai haki zao za kikatiba kwa sababu ya kutishwa kufungwa jela au kupigwa mabomu ni uoga uliokubuhu, bila kukabiliana na hili upinzani uatishia kulialia na kutoa matamko tu kila kukicha. Hivi sasa katiba inakanyagwa kwa kuvizuia vyama vya siasa kufanya mikutano kueneza itikadi zao na kuelimisha wananchi juu ya elimu za uraia na haki zao, hili lipo kikatiba na sio ombi. Sasa nashangaa wapinzani wameamua kuweka mikono nyuma na kukubaliana na hilo, wanaogopa kuitwa kua ni waanzishaji wa fujo_Ona CCM wanavyolewa madaraka wanafanya mikutano wao,wanakamata wapinzani kwa sababu tu ya kutembelea miradi ya serikali.


Usaliti pia kirusi ambacho kinamea na kurudisha upinzani nyuma, unakuta mtu anapiga kelele mpaka anataka kulia na kukaukiwa na mate kinywani lakini akipewa ujali basi kimyaa anaibuka na hoja na kauli za kupinzana na wapinzani wenzake.Hapa usitegemee upinzani ukasonga mbele na huu pia ni ujanja unaotumiwa na CCM pale wanapoona mambo yanawaendea kombo, hurubuni wapinzani ili kudhoofisha jitihada zao.
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Hata ccm wenyewe wanamuogopa bwana yule!
Wewe umeona baada ya kutoa tamko la kusema atakae pata mimba hakuna kurudi shule wale wote waliokuwa wanasema warudi wameufyata licha ya kuwa inapingana na kilichomo kwenye ilani yao!

Hapa ni kupambana tu jombaaaa mpaka kieleweke
 

Kwani

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
459
1,000
vyama vinavyokosa msimamo kamwe haviwezi ishinda serikali iliyopo madarakani
mnawezajr kumpa mtu nafasi ya kugobea uraisi na mlimwita fisadi kwa muda wa miaka nane?
hoja zenu kuu ni kukosoa utendaji wa serikali tu hata kwa mambo mazuri;

naamini mbowe akiachia chama watu wengine CHADEMA inaweza kutoa raisi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom