GE2025 CCM kuchangisha pesa si jambo baya wala si geni

GE2025 CCM kuchangisha pesa si jambo baya wala si geni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
580
Baada ya CCM kutangaza kupitia vyombo vya habari kuwa Mwenyekiti wake mama Samia Suluhu Hassani kesho ataongoza harambee ya kuchangia Uchaguzi Mkuu ujao, baadhi ya watu wameibuka wakikosoa na kupinga mkakati huo wakitoa sababu mbalimbali.

Binafsi naona watu tumekosa Cha kujadiri au tumeishiwa. Huo ni mkakati wao CCM. Wanachangishana wao kwa wao, hakuna mtu atakayelazimishwa kuchangia. Harambee huwa ni hiari, Sasa haya maneno yote yanatoka wapi?? Labda cha kuangalia hapo ni je, watakaotoa mahela yao wanategemea kupata favors zozote kutoka Serikalini baada ya Uchaguzi kama malipo kwa kuwezesha Uchaguzi? Vinginevyo haya maneno yote kudai sijui Kuna utakatishaji pesa, ni kupoteza muda tu.

Na Kwa mfumo huu wa harambee ya wazi CCM wamepiga hatua maana miaka iliyopita watu walikuwa wanachanga au kuchangisha kimya kimya kukawapo na madai ya Serikali kuwekwa mfukoni na wafanyabiashara.

Hata wenzetu wa CHADEMA nao wana mfumo wao wa harambee kutoka kwa wanachama na wafuasi wao maarutu kama tone tone. Huwa siyo rasmi wenyewe hutumia jukwaa la mikutano yao kufanya harambee ya vihela vidogo dogo ambavyo hata monitoring yake sidhani kama hufanyika.

Kama CCM kwa ukubwa wao na wingi wao, wana mkakati wa kukusanya bilioni hata 200, ni wao, tuwaache na sisi tukipata nafasi tuendelee na tone tone ya mia mia, jelo, buku nk. Ndo hivyo, safii!!
 
Back
Top Bottom