Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 473
Ilikuwa mwaka ,mwezi , wiki na sasa ni siku tu ndo zinazosubiriwa katika kitimtim cha kumtafuta mgombea atakayerithi, Nafasi ya Rais anayemaliza muda wake Mh Jakaya Mrisho Kikwete ,kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM.
Mtia nia kijana na Mmbunge wa Jimbo la Bumbuli, anapewa nafasi kubwa kuichukua nafasi hii endapo Ajenda ya Rais kijana itafanikiwa kama zilivyo ndoto za Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliyenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kwa sasa atakuwa kijana wa umri wake katika kipindi cha mwaka 1995.
Tabiri nyingi na Tafiti zisizo za kupikwa zinaonekana dhahiri, Nafasi hii ya Hadhi ni kwa Mmbunge wa Bumbuli. Mh January Makamba kwani hana kashfa na tuhuma, kulinganisha na watia nia wengine waliojitokeza kuitaka nafasi hiyo.
Itakuwa kazi rahisi kumnadi kwa wananchi kwa kuangalia sehemu mbalimbali alizopita amedhaminiwa kwa kishindo. Hali hii inatoa mwanga na Imani ndani ya chama cha mapinduzi kutokuwa na hofu dhidi ya upinzani endapo jina la Mtia nia huyo litapitishwa na vikao vya maamuzi ndani ya Chama cha mapinduzi CCM.
Kwa upande wa Mh January Makamba wakati akirudisha fomu za Urais makao makuu ya Chama cha Mapinduzi Dodoma. Alisema amezunguka sehemu mbalimbali za nchi ya Tanzania na kutafuta wadhamini sehemu kubwa alitumia usafiri wa basi.
Ametumia nafasi aliyoipata kuzungumza na wanachama ,Viongozi wa CCM pamoja na wananchi Waliofika kumlaki mamia kwa maelfu na kutoa maoni yao, amepata kufahamu kero zao na ameguswa sana na wingi wao na hamasa kubwa ya watu walionesha kuwa.
''Wananchi wengi hasa vijana wanaangalia CCM Itamteua mgombea wa aina gani, wengi wanataka aina mpya uongozi unaoangalia mbele zaidi, uongozi unaoakisi matarajio yao''.
Kama tunahitaji mabadiliko lazima tuwe na uongozi mmpya sio kutumia mawazo yaleyale yaliyodumu takribani miaka thelathini na nane 38, Rais ajaye lazima aonyeshe ana lipi la kuifanyia Tanzania sio asimamie ilani tu pia ana maono gani juu ya kuiendesha nchi ,hoja sio kwamba tunawabagua wazee lakini tunawahitaji kwa ushauri.
Vijana ni kundi kubwa na kilio chao cha muda mrefu ni ajira,akifafanua katika moja ya hotuba zake Mh January makamba amesema kuwa ''hawa ni watu muhimu na wengi sana. Viongozi wa siasa wameliita tatizo la ajira ni bomu lakini kulieleza taizo sio kulitatua.''
Vilevile bado CCM ni chama imara na kitashinda uchaguzi mkuu kwa kishindo kutoka katika nguvu za wananchi ,wanachama na viongozi wa wanachama kutokana na umahiri na usafi wa viongozi watakaoteuliwa kugombea nafasi mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya mashina.
Kambi ya upinzani itakuwa na wakati mgumu zaidi endapo mgombea huyu kijana atafanikiwa kuipeperusha bendera ya chama cha mapinduzi. Wabunge mbalimbali wa kambi ya Upinzani wamemuelezea kama mgombea mwenye sera nzuri zenye kutekelezeka vile vile Hupendelea siasa safi na ni mzuri katika kujenga hoja zenye mashiko yeye huwaza namna ya kuleta maendeleo.Mmoja kati ya viongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambaye hakupenda jina lake liandikwe kwenye kwenye gazeti hili akielezea kile anachokiamini kutoka kwa January Makamba.
Mwaka 2011 wakati Mh January Makamba akiwa mwenyekiti wa kamati ya Nishati na madini alisimamia kamati hiyo kwa weledi na uaminifu na kuibua hoja kadhaa zilizopelekea kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa nishati na madini Mbunge wa Sengerema Mh William Ngeleja.
Anakumbukwa zaidi pale alipotaka suluhisho la kudumu katika suala la mgao wa Umeme hali iliyopelekea kuonyesha msimamo wake kupinga maslahi ya vigogo wengi hali iliyozorotesha mahusiano yake na wanufaikaji katika nishati ya umeme.
Duru za kisiasa zinamtazamia kama kijana mwenye kulinda na kupigania maslahi ya nchi . kulingana na kumbukumbu nzuri za utendaji wake mzuri katika nafasi mbalimbali alizozitumikia mmpaka sasa wengi wamempachika jina kama kiungo mstaarabu kutokana na siasa safi anayoionyesha na kisasa yenye kuvutia vijana , wanawake na wazee wengi.
Majawabu aliyoyatoa katika siku ya kutangaza nia yameonyeshakuwa ni suluhisho tosha kwa matatizo ya watanzania. Anaweza kuishi na wenye dhiki na kulia nao katika shida zao kwani ni msikivu anayeweza kushaurika, Anaonekana ni mwenye wito zaidi sio mwenye maisha ya anasa na starehe mara zote hutengeneza dira ya kuongozea watu unaweza kuyaona haya katika kitabu chake TANZANIA MMPYA MASWALI 40 Na kitabu cha BUMBULI , ameonekana kuwa ni mpenda haki haongozi kwa ujanjaujanja vilevile anachukizwa na Rushwa.
Vijana wengi wanamuombea Mh January aonekane katika macho ya waamuzi kwani wanamatumaini naye kutokana na nguvu na uwezo alionao katika kufikiria, kuifanyia mambo mapya na mazuri nchi ya Tanzania .
Anaheshimika kwa kuwa na siasa unganishi kwa kila rika sio mwenye maamuzi ya kukurupuka hutoa mawazo yenye kujenga na kushauri juu ya uelekeo wa nchi. Uwezo wa kiongozi huonekana katika nafasi aliyonayo kwa JANUARY MAKAMBA yote yamedhihirika.
Ni kiongozi wa mmfano na hadhina ndani ya chama, macho na masikio yote tunayaelekeza katika mkutano mkuu kama wataamua kutupa karata kwa kijana ama kuwaachia ving'ang'anizi kupambana na changamoto za UKAWA.