CCM Kisonge Zanzibar wanyosheana vidole

CCM Kisonge Zanzibar wanyosheana vidole

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
KISONGE WATAKA CCM YAO WAMTAKA DR. SHEIN KUTIMUA ?RIGHT HAND MAN? WAKE KWAMBA NI MAMLUKI WAMEIGHARIMU CCM
Maskani kaka na makada wahafidhina wa CCM wametaka wanawatuhumu mamluki ndani ya CCM na kutokuwajibika kama sababu ya CCM kushindwa na kumtaka Dr Shein kama makamo Mwenyekiti wa CCM kuwaweka pembeni.

Duru za siasa za kihafidhina ndani ya CCM zikishadidiwa na maskani kaka ya kisonge wanamtaka Dr. Sheni sasa kuwatema rasmi Mohamed Aboud na Omari Yussuf Mzee kwa madai kuwa ni mamluki wa CUF na hawana uchungu na CCM kwani hawana jimbo na wala hawagombei lakini Dr. Sheni anawakumbatia na kukigharimu Chama cha Mapinduzi.

Makada hao wa mrengu wa kihafidhina ndani ya CCM wanamtaka Dr Shein kuchagua ?Great Thinkers? wa CCM ambao wana damu ya Afro Shirazi sio akina Mohamed Aboud na Omar Yussuf Mzee ambao hawana uchungu na CCM, maana kama kweli ni CCM ngangari wangetafuta majimbo ya kugombea badala yake wanasimama nyuma ya Dr Shein na kumuhujumu yeye na CCM. sasa wakati umefika waondoke.

Aidha makada hao wametupa lawama kali kwa Balozi Seif Ali Idd kwamba pamoja na kuwa na mamlaka makubwa kiserikali ameshindwa kuiwezesha CCM kushinda na kurejea kushindwa kwake kumpatia Amani Karume ushindi wa kishindo mwaka 2000 akiwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM ambapo alitimuliwa na Karume aliposhika wadhifa wa makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar na kumteua Ramadhan Feruzi.

Kisonge wanadai Balozi Seif hana mbinu za kushinda siasa za kiushindani ingawa hawana mashaka na U-CCM wake, aidha wametaka pia Dr Shein kuachana na makada wengine maarufu wakitajwa kuwa ni Pandu Ameir Kificho aliyekuwa spika wa baraza la wawakilishi, haji Omar Kheri na Ramadhani Abdallah Shaaban kuwa ni mzigo kwa CCM na hawawezi kuisaidia CCM kuimarika kwani wapo kwa maslahi yao tu na si kwa maslahi ya CCM, na kwamba sasa umefika wakati kwa Dr Shein kutowakumbatia wachumia tumbo na kutaka apate ?

Great Thinkers? watakao imarisha CCM kwa kutokana na damu ya Afro Shirazi na pia wenye uwezo kitaaluma na kimkakati kwani Kificho, Shaaban na Kheri wamechoka akili na hawa elimu, na kwamba kwa sasa CCM inahitaji wasomi sio kuongozwa na vichwa mchungwa.

Aidha Ali Vuai Naibu katibu Mkuu wa CCM hakuachwa katika lawama za kushindwa kwa CCM katika uchaguzi huu kwamba hakuwa makini kuhakikisha maslahi ya CCM yametimizwa kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza na sasa kutoa visingizio visivy mashiko akidai mawakala wa CCM hawakutambuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wakati, hali ya kuwa siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuelezea tathmini ya maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi, ni kwa nini hakuliona hilo wanadai Kisonge. Na kumtaka aanchie ngazi mara moja, ili CCM ipate waliotayari kuifanyia kazi CCM kwa moyo wote na sio kuzembea na kutoa visingizio.

Kisonge wamedai historia ya CCM itawaandika vibaya akima Mohamed Aboud, Omar Yusuf Mzee, Pandu Ameir Kificho, Ramadhan Abdallah Shaabani na Haji Omar Kheri kwamba walichangia kuiangamiza CCM kutoka katika medani ya siasa za ushindani, na kuwataka waondoke, na kwamba hawako tayari kuona CCM ikitoweka kama ilivyo kwa KANU ya Kenya na ZANU ya Zambia.

Chanzo: Mzalendo
 
Maalim tayari ushachkua nchi,kikubwa ukomae hvyhvy...yale mambo uchaguz haukuwa wa haki hayatakusaidia..usirud nyuma wakt ndo huu
 
Maalim ameshawashukuru observers na kueleza kwamba atatoa ushirikiano kwa mujibu wa katiba. Amemaliza hayo ya ZEC amewaachia wenyewe
 
Ha ha ha haa! Sooon inakuja bara lumumba patam hapo
 
Tutalaumiana sana na bure, wakati ukifika kila mbinu huchemsha na ukweli huwa wazi na dhahiri
 
Ninachokiona hapo ni kwamba serikal kuu ya muungano itasubir kwanza huku bara then baada ya hapo ndio watahamia znz
 
Kwani Maalim Seif ameishatangazwa? Inaelekea ukombozi wa bara utatokea visiwani!!!!

Ndio maana hawataki kutangaza kwa sababu hio, bara kutaripuka vibaya.
 
Ntaharamwe hawataki kutangaza Rais wetu maalim, icc iko wapi walinisuru taifa
 
Kisonge waanza kushosheana vidole

KISONGE WATAKA CCM YAO WAMTAKA DR. SHEIN KUTIMUA ?RIGHT HAND MAN? WAKE KWAMBA NI MAMLUKI WAMEIGHARIMU CCM
Maskani kaka na makada wahafidhina wa CCM wametaka wanawatuhumu mamluki ndani ya CCM na kutokuwajibika kama sababu ya CCM kushindwa na kumtaka Dr Shein kama makamo Mwenyekiti wa CCM kuwaweka pembeni.

Duru za siasa za kihafidhina ndani ya CCM zikishadidiwa na maskani kaka ya kisonge wanamtaka Dr. Sheni sasa kuwatema rasmi Mohamed Aboud na Omari Yussuf Mzee kwa madai kuwa ni mamluki wa CUF na hawana uchungu na CCM kwani hawana jimbo na wala hawagombei lakini Dr. Sheni anawakumbatia na kukigharimu Chama cha Mapinduzi.

Makada hao wa mrengu wa kihafidhina ndani ya CCM wanamtaka Dr Shein kuchagua ?Great Thinkers? wa CCM ambao wana damu ya Afro Shirazi sio akina Mohamed Aboud na Omar Yussuf Mzee ambao hawana uchungu na CCM, maana kama kweli ni CCM ngangari wangetafuta majimbo ya kugombea badala yake wanasimama nyuma ya Dr Shein na kumuhujumu yeye na CCM. sasa wakati umefika waondoke.

Aidha makada hao wametupa lawama kali kwa Balozi Seif Ali Idd kwamba pamoja na kuwa na mamlaka makubwa kiserikali ameshindwa kuiwezesha CCM kushinda na kurejea kushindwa kwake kumpatia Amani Karume ushindi wa kishindo mwaka 2000 akiwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM ambapo alitimuliwa na Karume aliposhika wadhifa wa makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar na kumteua Ramadhan Feruzi. Kisonge wanadai Balozi Seif hana mbinu za kushinda siasa za kiushindani ingawa hawana mashaka na U-CCM wake, aidha wametaka pia Dr Shein kuachana na makada wengine maarufu wakitajwa kuwa ni Pandu Ameir Kificho aliyekuwa spika wa baraza la wawakilishi, haji Omar Kheri na Ramadhani Abdallah Shaaban kuwa ni mzigo kwa CCM na hawawezi kuisaidia CCM kuimarika kwani wapo kwa maslahi yao tu na si kwa maslahi ya CCM, na kwamba sasa umefika wakati kwa Dr Shein kutowakumbatia wachumia tumbo na kutaka apate ?Great Thinkers? watakao imarisha CCM kwa kutokana na damu ya Afro Shirazi na pia wenye uwezo kitaaluma na kimkakati kwani Kificho, Shaaban na Kheri wamechoka akili na hawa elimu, na kwamba kwa sasa CCM inahitaji wasomi sio kuongozwa na vichwa mchungwa.

Aidha Ali Vuai Naibu katibu Mkuu wa CCM hakuachwa katika lawama za kushindwa kwa CCM katika uchaguzi huu kwamba hakuwa makini kuhakikisha maslahi ya CCM yametimizwa kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza na sasa kutoa visingizio visivy mashiko akidai mawakala wa CCM hawakutambuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wakati, hali ya kuwa siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuelezea tathmini ya maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi, ni kwa nini hakuliona hilo wanadai Kisonge. Na kumtaka aanchie ngazi mara moja, ili CCM ipate waliotayari kuifanyia kazi CCM kwa moyo wote na sio kuzembea na kutoa visingizio.

Kisonge wamedai historia ya CCM itawaandika vibaya akima Mohamed Aboud, Omar Yusuf Mzee, Pandu Ameir Kificho, Ramadhan Abdallah Shaabani na Haji Omar Kheri kwamba walichangia kuiangamiza CCM kutoka katika medani ya siasa za ushindani, na kuwataka waondoke, na kwamba hawako tayari kuona CCM ikitoweka kama ilivyo kwa KANU ya Kenya na ZANU ya Zambia

Chanzo: Mzalendo
 
Hakuna kinachidumu milele. Wamesahau wakati ni ukuta.
 
HABAR NJEMA WAZANZIBARI...............
MUDA WOWOTE KUANZIA SASA MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD ANATANGAZWA KUWA RAIS WA ZANZIBAR KAMATI KUU YA CCM IMESHAKUBALI DK SHEIN AMESHAKUBALI KUSAIN JAPO KWA MSHIKE MSHIKE CHINI YA USIMAMIZI MKUBWA WA UMOJA WA MATAIFA HIVYO MUDA WOWOTE MAMBO YANAAZA KUWA MAMBO ZNZ HATIMAYE WAZANZIBARI TUNAANZA KUUONA UHURU......Hizi habar ni za uhakika asilimia mia moja...
 
Back
Top Bottom