CCM KIMEISHIWA MTAJI?

CCM KIMEISHIWA MTAJI?

MANYORI Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2012
Posts
462
Reaction score
343
Ni swali tu ndugu zangu.Chama kikongwe katika ulingo wa siasa za Tanganyika na baadaye Tanzania na chenye historia ndefu juu ya uongozi kitaifa sasa kinaonekana dhahiri dhihiri kinapumulia mashine.Ndani hakukaliki,nje nako vilevile.Ukiivuka mipaka(borders) ya Tanzania napo hali yake imedhoofu sana.Madai ya chama kubebwa kwa mikono ya Dola nayo si mageni hasa nyakati hizi za giza nene.
Njia ambazo katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikitumiwa kukiendesha chama na kukipa uhai kwa kuongeza wanachama wapya nazo ni mpya! Zimewaacha wengi wakiwa na huzuni na manung'uniko lukuki achilia mbali ule msemo wa 'mgeni njoo wenyeji tufe'.
Kufuatia sintofahamu iliyotanda ndani na nje ni wazi hali yake si shwari hasa.Pepo za tufani na vimbunga zimeharibu kabisa nguzo ,miundombinu na mwelekeo wake.Kitendo cha makada wake kuitwa na wengine kuonywa kwa kuanza kampeni mapema nazo ni ishara kuwa nyumbani pagumu.
Vitendo vya watu wanaodhaniwa kuwa ni wakosoaji wa chama, mfumo na taasisi zake kupigwa(Mabomu,virungu na risasi), kutekwa na wanaoitwa wasiojulikana na wengine kulazimika kuikimbia ardhi yao navyo vinaashiria mapafu yaliyochakaa na yasiyojiweza kuendelea kuwezesha pumzi yake.
Makundi yote yaliyokiunga na ambayo yameendelea kukiunga mkono chama hiki kikongwe yanaelekea na mengine yameshabwaga manyanga.Wahitimu wanalia-hakuna ajira na zilizopo ni za ubaguzi wa hali ya juu.wanaotarajiwa kustaafu nao bado presha zimewagandia juu kuliko juu.Watumishi nao hawaelewi hatma za madaraja na ongezeko la masurufu yao.Kina mama nao wanaisoma tena kwa sauti.Wafanyabiashara na wawekezaji hawajui nini lini kitakuwaje.
Kwa kurejea utafiti uliofanywa na TWAWEZA juu ya wanaoiunga mkono,nyakati zimebadilika.Wajinga wamepungua japo umasikini ndio kwaaaanza unaongezeka kila uchao na uchwao.
Sasa mimi ninauliza,CCM kimeishiwa mtaji?
 
Napita mkuu
 
Ngoja waje utatukanwa na pia wewe unaongeza uwezekano wa mkuu wa cdm kuwekwa ndani maisha, ngoja wapinga kila kitu waishe maaana yake maendeleo yatakwenda juu juu juu sana
 
Ina maana huu UZI utapelekwa mahakamani kama ushahidi kwenye case ya huyo mkuu wa CHADEMA, ili awekwe ndani maisha??? Au kama vipi fafanua vizuri sababu juu ya hilo ulilosema hapo kwa mwandika huu uzi.

Nimeshangaa hoja yako, ndo maana nimeuliza.[emoji53]
 
Nimesoma mkuu kwa sababu umeniambia ila mwandishi ana tatizo kichwan sio bure
Bahati mbaya suala la 'ukichaa' au kama ulivyoita wewe 'tatizo kichwani' ndiyo moja ya credit zinazotumika kumpa mtu chakumemena.
 
Hahah nimecheka sana ilo neno cha kumemena , neno ka kihehe kama sijakosea, ok bro naona unaungana nae , mpe moyo tu had 2020 atapo ona chama kinavo peta kama haja comet sucied sijui
 
Iko hoi[emoji381], ndembendembe, chali[emoji724] kifo cha mende. Inapumulia machine [emoji602][emoji595][emoji603][emoji603][emoji603][emoji379].
 
Mtaji wake ndio unazidi kukua. Ni ujinga na umasikini!
 
Back
Top Bottom