Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 198
- 209
Sintofahamu imeibuka ndani ya chama cha Mapinduzi(ccm)mkoa wa Kilimanjaro kufuatia hatua ya chama hicho kumwengua katibu wa siasa na uenezi wa mkoa kushiriki vikao vya kamati ya siasa ya mkoa ambayo ilikuwa na jukumu la kupitia majina ya watia nia wa nafasi mbali mbali ikiwamo za udiwani na ubunge.
Kitendo hicho kinatajwa kuwa ni ukiukwaji wa katiba ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la januari 2025 Ibara ya 90 inayoainisha wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa katika kila mkoa.
Ibara hiyo ya 90 1 inasema na hapa nanukuu “kutakuwa na kamati ya siasa ya mkoa katika mkoa ambayo itakuwa kama ifuatavyo”,mwisho wa kunuuu.
Wajumbe hao kwa mujibu wa katiba ya ccm ya mwaka 12977 toleo la januari 2025 ni (a)mwenyekiti wa ccm mkoa,(b)Katibu wa ccm mkoa,(c)mjumbe/wajumbe wa Halmashauri kuu ya ccm Taifa,(d)mkuu wa mkoa anayetokana na ccm,(e)Katibu wa siasa na uenezi wa mkoa,(f)mwenyekiti wa mkoa wa kila jumuiya.
Hapa katiba inawataja wenyeviti wa kila jumuiya za chama ikimaanisha Jumuiya ya wazazi,Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi(uwt) na umoja wa vijana wa chama cha mapunduzi(uvcc).
Wajumbe wengine wanaoingia kwenye kamati ya siasa ni wajumbe watatu waliochanguliwa na Halmashauri Kuu ya ccm mkoa na mwenyekiti wa kamati ya madiwani,hawa ndiyo wajumbe halali wa kamati ya siasa ya mkoa.
"Ni vyema mkawauliza viongozi wa chama ni kanuni ipi ilitumika kumzuia mwenezi wa mkoa asishiriki vikao vya kamati ya siasa ya mkoa wakati huyo huyo alikuwa ni miongoni mwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa ambao walishiriki kupitia jina la Mwenyekiti watu wa chama Taifa,Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea tena wa Urais katika uchaguzi mkuu ujao",anahoji kada mmoja wa chama hicho.
Sasa tuwaulize viongozi wa CCM mkoa walitumia mizania gani kumvurusha katibu huyo wa siasa na uenezi wa mkoa ambaye ndiye anayepaswa kutoa pia taarifa hata kwa vyombo vya habari juu ya mwenendo mzima wa namna mchakato mzima ulivyoendeshwa .
Kwa faida ya wasomaji wangu naweka hapa katiba inavyosema
kazi kwenu viongozi