CCM kidedea umeya Sumbawanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kidedea umeya Sumbawanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Mar 27, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa mara nyingine tena CCM kimetwaa kiti cha umeya ktk manispaa ya Sumbawanga baada ya meya wa awali kujiuzulu kutokana na "kashfa" ya kuwa na elimu ndogo.
   
 2. k

  kiche JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  toa habari iliyokamilika,mfano uchaguzi umefanyika lini na wapiga kura walikuwa walikuwa wangapi.
   
 3. m

  matawi JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kaumza wewe ni seniour jf member toa habari kamili ubabaishaji hausaidii jamvini
   
 4. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  BARAZA la madiwani la Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa limemchagua Sabas Katepa ambaye ni diwani wa kata ya Ntendo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Meya mpya wa manispaa hiyo.

  Uchaguzi wa kumpata Meya umefanyika kwenye ukumbi wa manispaa hiyo, ambapo Mkurugenzi wa uchaguzi huo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Silvia Siriwa alimtangaza Kapeta kuwa mshindi kwa kupata kura 16 akimshinda, Field Kasitu aliyegombea kwa tiketi ya Chadema na kuambulia kura 4.

  Diwani mmoja wa CCM hakupiga kura kutokana na kuwa na udhuru. Uchaguzi huo umefanyika kufuatia kujiuzulu Januari 28 mwaka huu kwa aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo, Samwel Kisabwiti kupitia CCM kwa madai ya kulinda heshima yake binafsi na ya chama chake.

  Kisabwiti ambaye ana elimu ya darasa la saba alifikia uamuzi huo baada ya kutambua kwamba meya ni mtu muhimu na anatakiwa kuwa na elimu ya kutosha ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi, alihitaji kupata muda wa kutosha ili ajifunze.

  Meya huyo amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja na nusu, alichaguliwa kushika nafasi hiyo Desemba 17, mwaka jana ambapo alikuwa mgombea pekee baada ya mgombea wa
  Chadema kujitoa.

  Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa na madiwani hao, Katepa alisema kuwa uchaguzi ulikuwa mgumu kwa upande wake, lakini anashukuru Mungu kwa kupata nafasi hiyo na hatakikisha anasimamia kwa ukaribu mapato na matumizi ya halmashauri hiyo ambayo ina vyanzo vichache vya mapato, lakini vikisimamiwa vizuri vitasaidia kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

  Aliongeza kuwa katika kipindi chote akiwa kwenye nafasi hiyo atajitahidi kuhakikisha manispaa haipati hati chafu, inayoweza kusababishia kukosa fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu.

  Halmashauri hiyo ina madiwani 21 kati yao 16 ni wa CCM, wanne wa Chadema na mmoja ni diwani kupitia tiketi ya DP.

  Source: HabariLeo
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kulikuwa hakuna element za kuchakachua...maana hawa jamaa ni moja ya sera zao......
   
 6. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ongera zao maana siasa si chuki wala vita kama walistahili ushindi na wameshinda wanastahili pongezi pia
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  inasikitisha sana kusikia na kuona poeples power wakipata kura 4 tu kat ya 21. mimi naanza kulia na wengine mnifuatilizie hiiiiiihiiiiiiiiiiii!
   
 8. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  usilie mbona kwenye maandamano watu wanaajaga.
   
Loading...