CCM Kahama acheni hizo!

CCM Kahama acheni hizo!

Michael Scofield

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
1,225
Reaction score
473
Mie ni mfanyabiashara katika maduka yaliyopo hapa ofisi za chama cha mapinduzi wilayani Kahama.
Hivi vibanda tumepangishwa na watu waliopewa na CCM wavijenge miaka ya nyuma (Sijui makubaliano yao na chama).
Mwanzoni mwa mwaka huu, tulipitiwa na iliyokuwa kamati ya kufuatilia mali za ccm (kama skosei) tukaojiwa bahadhi ikaonekana wale waliotupangisha kama hawafikishi pango za vyumba tunazowapa.
Tukaitishwa kikao kwa katibu (ingawa mie sikuhudhuria) nilivyowauliza wenzangu wakanambia tumeambiwa tuwarudishie gharama za ujenzi waliotupangisha ili tuingie mikataba mipya na CCM.

Kikubwa nachojiuliza, Naambiwa nitoe milioni 3 kuwarudishia gharama wenye vibanda! je CCM ilishindwa vipi kumalizana nao hao wenye vibanda?
Pili kwa usawa huu kibanda nilipe milioni 3, hapo bado hakijawa changu ni mali ya chama mie naingia mkataba na ccm niilipe tena, hapo ni sawa kweli?

Tatu miaka yote hao watu tunawalipa na huko pesa hawafikishi, inamaana gharama zao hazijarudi tu?
Na wahusika wote wa vibanda ni wanachama kindakindaki wa CCM.

CCM Kahama mnaboa, nyie malizaneni na watu wenu, muingie mikataba mipya na sisi wapangaji kuliko kutubebesha hilo zigo la milioni 3.
 
hao ni wakupeleka mahakamani kitaeleweka au njoo huku mhongolo
 
Back
Top Bottom