Inasikitisha tena saana kushuhudia nchi inazidi kugubikwa na simanzi kila kukicha. Makundi yote ya jamii ya ya Tanzania yameguswa na msukosuko kwa namna moja au nyigine. Kinachosikitisha kwa serikali yetu ni pale ambapo haifanyi juhudi zozote kuziba ombwe hili linalotokana na jinamizi la sintofahamu nchini mwetu. Nafahamu kwamba watawala wa CCM akiwemo Nape wamesomea Propaganda na bahati mbaya wanatumia vibaya elimu muhimu.
Kwa mtanzania makini atakumbuka siku chache zilizopita jinsi tulivyovurugwa kwa tiba fake ya ukimwi kule loliondo ili tusijadili hoja madhubutu za nchi yetu kama vile malipo ya Dowans na masuala ya richmond wakati huo. Mbinu hiyohiyo inatumiwa na watawala wa ccm sasa hivi kwa kuzua kesi kwa viongozi wa chadema ili kuvuruga M4C na uanzishwaji wa kanda za CHADEMA. Sina hakika kama watafanikiwa maana hapa tulipofikia wengine ni ile hatua aliyoasisi mh waziri mkuu mizengo pinda: kuliko kushabikia, kuchagua, au kuunga mkono ccm haiwezekani-LIWALO NA LIWE!
Hebu jiulize kauli ya Mwigulu na Wasira kabla ya tukio la kuteswa kwa mhariri Kibanda halafu video inatolewa mara tu baada ya tukio kana kwamba ilikuwa inangojea tukio litokee! Hivi serikali inafikiri ni juu yetu sisi watoto wa mama ntilie? Kwamba hatujui kinachoendelea, au jeuri hii inatoka wapi nyie CCM? Hamumuogopi hata Mungu aliyeumba mbingu na nchi hii manyoringi....Ole wenu nyie mnaochuja ngamia na kunasa mbu! Hizo nyavu zenu Mungu anaziona.
Dr ulimboka ameteswa na mtesaji anafahamika kwa jina lakini amelindwa hata saa hii....jeuri hii mnaitoa wapi? Mwakyembe alinyemerewe na mafisadi wa ccm kila kona, hata alipotoa taarifa kwa igp aliziba masikio! Akimwagiwa sumu na wakubwa wakaishia kubishana, wizara ya afya inasema lake, waziri wa mambo ya ndani, DCI na wengine kila mtu anasema lake.....cha kushangaza CCM mnadhani hatuelewi kabisa; mnakosea mno!
Albino, vikongwe, wanauawa kila mwaka lakini CCM hakijachukua hatua madhubuti ili kuzuia mauaji hayo huenda kwa sababu viungo vya albino vinatumiwa na .........Ukweli ni kwamba kipindi tulicho nacho si cha kudanganyana, tunaelewa kila ujinga mnaoufanya.