CCM ishinde, ishindwe, nakata rufaa mahakamani

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Wazee
Salaamuni kwa mpigo.
Mimi pia niko Igunga. Ninayoyaona yananifanya niaumue kukata rufaa baada ya uchaguzi kwa sababu ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi. CCM ishindwe au ishinde, ni lazima nikate rufaa kwa sababu kubwa mbili:

1. Kitendo cha dhehebu la dini kutamka hadharani kuwataka waumini wake wasikipigie kura chama fulani ni ukiukwaji wa sheria za uchaguzi. Hata kama serikali ingekemea, bado nisingeridhika. Labda kama chama kilichopigiwa kampeini kingejitokeza hadharani na kukemea jambo hilo ningeridhika. Kama madhehebu mbali mbali yakiruhusiwa kuvipigia kampeini vyama vya siasa, tutaingia kwenye mgogoro mkubwa kitaifa. Nina hakika dhehebu lolote kama lingethubutu kutamka hadharani kuwa waumini wake wapigie chama kingine kisicho hicho kilichotetewa, uchaguzi huu ungesimamishwa.

2. Kitendo cha Waziri Magufuli kusimama hadharani kama wazirimwenye dhamana ya ujenzi na kutamka kuwa atajenga daraja la Mbutu ni rushwa ya waziwazi kwa wapiga kura wa chama chake. Angesubiri uchaguzi uishe, au angetoa tamko hilo katika hadhara nyingine si katika kampeini za CCM.

Haya mawili kwangu yanatosha kunipandisha chati kuliko Mtikila na Kainerugaba katika medani za utetezi wa haki hapa nchini. Achilia mbali mawaziri, Ma-DC na Ma-RC kuonekana wakikimbiza magari yetu huko Igunga.
 
Hili la kutumia dini halitakuwa na uzito wa kisheria ukizingatia Bakwata ndiyo walitoa tamko tena hawakusema wazi watakipigia kura chama gani ila walisema waislam wasiipigie kura CDM labda uikatie rufaa Bakwata!
 
Kama wataka kutetea haki tetea haki na si kwa ajili ya kutaka kujipandisha chati!
 
Naona CCM walikiuka taratibu nyingi tu ikitaka kukata rufaa utashinda tu maana hata GE2010 ukiukwaji wa taratibu ulikuwa mkubwa, bila kukiuka taratibu magamba hayachaguliki!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom