Nilidhani kuna jambo la maana kumbe ni hoja nyepesi hivi? Labda nikusaidie tu Mkuu kama CCM kutoka au kutoshika tena dola basi inaweza ikawa mwaka wa 10000 au mwaka 10,015 ila siyo kwa sasa, kesho, keshokutwa na mtondogoo. Fanyeni mambo mengine ila msipoteze muda wenu mkidhani CCM itang'oka leo na kwanza bado sijaona Chama cha Upinzani nchini Tanzania bali nawaona tu Wanaharakati ambao hata Wao pia mdomoni ni Wapinzani ila Mioyoni mwao ni wana CCM wazuri tu.