CCM inaua MUUNGANIKO..

Yes!Lakini umekosea sehemu moja tu,sisi sio wadanganyika sisi ni WATANGANYIKA,naomba usituvunjie heshima!!!

Hahaa...nitaona msimamo wenu katika hili na kama tutajitambua na kusimamia lile tunaloliamini kutaka Jamhuri yetu ya watu wa Tanganyika kama "wenzetu" wa visiwani walivyofanikiwa kutupeleka puta na kuchomoa kwenye hii "ndoa" basi nitaamini sisi sio Wadanganyika ni Watanganyika.

Nikiangalia tunavyoyumba na kupelekwa pelekwa katika siasa na vilaza ambao hata Civics wana F , hakika narudia kuwa sisi ni Wadanganyika. Tumeibeba mno Zanzibar, ona wanayotufanyia, ubaguzi wa wazi hata katika teratibu za muungano wenyewe....tumekuwa tukienda visiwani kwa passport until recently, wabongo wananyanyaswa hadi wengine kuchomewa biashara zao lkn hakuna kilichotokea. Wameuawa na kujeruhiwa hata viongozi wa dini wenye asili ya bara yoote hayo yakiwa ni harakati za wenzetu kujitenga na muungano.

Ona hata tume ya katiba nusu kwa nusu linganisha watu milioni moja wanawakilishwa na watu 15 hali kadhalika watu millioni 44 wajumbe 15...huu si udanganyika Deony?? Wenzetu walishaandaa katiba yao ambao kwa sheria za Tanzania ni wazi walitangaza uhaini kwani vifungu vya katiba yao vinasigana wazi kabisa na katiba ya JMT lkn nani analiona hilo?Tutaendelea kupandiwa kichwani hadi lini? Kwa faida ya nani? Kwanini sisi tuwe vimbele mbele vya kuutetea huu muungano as if kuna kikubwa sana tunachofaidi humo? Nimeomba nitajiwe faida za Muungano kwa sasa ambazo sisi wabara tunaweza kuziexperience sioni wa kunijibu sasa huku si kujidanganya?

Nina uhakika hata kama leo utaitisha "Referundum" ni mawazo ya CCM tena ya kina Nape yatachukuliwa...watasema serikali 2 na kushinikiza wana ccm wenzao hasa wadanganyika na kwa kutumia ujinga na wingi wao watapiga kura kuruhusu serekali 2 za kinafiki ziendelee..Je huusi Udanganyika ndg yangu?

Wenzetu wamekubali hata kuzika tofauti za CUF na CCM (THOUGH NAJUA HILI TIME BOMB) ili watetee wanachokiamini "Nchi yao na mamlaka kamili, sisindio kwanza wele ni ndg zetu...nk...sioni jina jingine la kujiita kwa mwenye mawazo ya namna hii kama sio Mdanganyika!!
Kweli sisi ni Wadanganyika na hapa tunazungumzia swala moja tu la Muungano yapo mengi tunayodanganyika nayo kirahisi na nitaendelea kuamini hivyo hadi tutakapo amka. Wenzetu wameamka sisi bado tumelala. Sio lazima tukaanzisha uamsho kuchinja na kuchoma biashara za wengine lakini Tuamke usingizini.

Nahitimisha kwa kusisitiza kuwa nitaomba radhi kuwaita Wadanganyika pale nitakapoona msimamo na kujitambua kwenu kuhusiana na hili swala la Muungano kwenye katiba mpya. Kusema ukweli sio kuvunja heshima hata siku moja. Uzuri mpira uko kwetu, tuna uhuru wa kuucheza ama kuendelea kubung'aa kama ilivyo kawaida yetu tuendelee kupigwa magoli
 
Pana ombwe kubwa sana juu ya sintofaham Za Muunganiko huu.. Nadhani ni wakati wa kuweka mjadala Wa kitaifa tuamue ni kekundu au cheusi ndipo masuala ya KATIBA yaendelee


Hoja yako (hapo kwenye bluu) inalazimisha tukae tukizungumzia kitu ambacho tayari wananchi wa pande zote wameshaonesha njia sahihi ni kuuvunja muungano. sijaelewa kwanini wewe kwa maelezo yako unashauri tuendelee kulea yale makupe bungeni na humu mitaani huku bara. Kuyatoa haya makupe haraka ni kuvunja huu muungano kesho pasipo ajizi. Sasa kwa sababu ni jambo la Kisheria, inabidi tukubali huu mchakato wa serikali tatu, halaf tukiweka serikali makini 2015, bara tunakataa kabisa serikali ya Muungano wakati taasisi inayoitwa Tanganyika ipo ofisini.
 
Ili Muungano uendelee it is either serikali moja au mbili. Serikali 3 (which is just delayed kuvunja muungano) ni sawa na kuuvunja muungano. Ni afadhali basi tuuvunje tu sasa hivi. Kwa nini hawa wazee wananoa mapanga ili vijana waje wauvunje kirahisi wakati wao watakuwa wameondoka? Warioba asitudanganye. halafu kama serikali tatu ni mapendekezo tu bado, mbona tayari wameandaa katiba inayotambua serikali tatu? Anatu preempt! Mimi naona tujadili kwanza aina ya muungano, tukishakubaliana ndipo katiba inayotambua tulichokubaliana ije tuijadili.

Hapo kwenye Bluu napinga kabisa. Katika Serikali mbili tumelazimishwa kubeba zigo kubwa ambalo wala hata si la lazima bungeni na mitaani. Sikubaliani kabisa na dhana ya viijiji vya Zanzibar kuitwa majimbo ya Uchanguzi, kuitwa wilaya. Hiyo Mishahara wanayopewa hao wawakilishi wa vijiji kutoka Zanzibar inaeza fanya mambo mengine ya maendeleo hapa nyumbani. Na huku mitaani wakae kama wawekezaji wengine na wafuate masharti yote ya wahamiaji wengine; no special treatment! Muungao kwenye EAC.
 
Mkimaliza porojo msimamo wa waz'br upo palepale wala hawatetereki,jamhuri ya watu wa z'br kwanza longolongo baadae.
 
umenena vema. CCM wangesimamia Serikali Moja ingekaa vizuri sana hiyo. Kwa hali iliyopo Zanzibar watakataa Serikali moja kwa malengo wanayoyajua wao. Tanganyika hatupotezi kitu katika hilo. Kitachowapata mbele kitakuwa chao. Kiutu, ni hekina tu tunawapa angalizo kwamba Serikali Tatu haitakubaliwa in the long run kwa sababu mfumo huo utaleta zigo la serikali ya Muungano ambalo ni gharama ya uendeshaji nchi isiyokuwa na sababu wala umuhimu utaokulika kwenye eneo ambalo linaelekea kwenye Federation ya nchi pengine sita au saba.

Katika Serikali moja ni kwamba Zanzibar itapata bahati ya kuingia kwenye Federation ya EAC wakiwa na upendeleo maalum ndani ya Tanganyika. Hii ni bahati ya mtende kuota jangwani ambayo mwenye busara yeyote angeiona. In reality, Serikali Tatu ni dhana unviable; ni boya ambalo litapasuka mara tu litapotupwa majini na kuvunja muungano. Zanzibar kukataa Serikali Moja wanapoteza kabisa bahati ya upendeleo ndani ya Tanganyika. CCM ingekuwa makini ingewapelekea huu msimamo wakatae wenyewe. Waliokubali Serikali Tatu katika uhalisia hawataki Muungano. Kama CCM inautaka muungano njia ya kuuendea ni kuitisha serikali moja. Mbili hapana kwa sababu hakuna anayezitaka. That would be where to go for CCM.
akili ndogo wewe.. kale dawa zako zakichaaaa
 
akili ndogo wewe.. kale dawa zako zakichaaaa

Point: ngoja niziwahi... ha ha ha ha.....
We dozi yako ushamaliza? manake nakumbuka tulilazwa vitanda jirani mirembe.

na ile baragashia yako iliyoliwa na panya ushaishona? ha ha ha ha.....
 
Back
Top Bottom