CCM inatumia mfumo wa Frog boiling effect kuendesha nchi

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,941
Reaction score
51,063
Frog boiling effect au boiling frog syndrome ni maelezo ya dhana ya kisaikolojia kuwa binadamu anaweza kuvumilia jambo baya akifanyiwa kwa taratibu (awamu kwa awamu) kuliko jambo hilohilo akifanyiwa kwa ghafla kwa wakati mmoja.

Maelezo ya dhana hiyo yanaonesha kuwa kuna chura aliwekwa Kwa ghafla kwenye jungu linalochemka maji na chura huyo kutokana na joto la maji kuwa kubwa akaruka nje ya jungu kwa haraka.

Lakini chura yule yule alipoweka kwenye jungu lile lile likiwa na maji ya baridi na Kisha maji kuongezwa joto kwa awamu, alitulia bila ya kutoka ndani ya jungu.

Maji yalipofika kiwango cha juu cha joto kama cha maji ya awali, chura akawa amechelewa kujenga mazingira ya kujiokoa.

Wanasiasa wanaotumia dhana hii kutawala, huanza kufanya jambo baya kwa awamu kiasi kwamba watawaliwa hukubali na kuona kama jambo hilo baya, ndiyo aina mpya ya maisha yao.
 
Unateka mtu mmoja, Kisha wa pili, unaongeza na mwingine... Halafu utekaji wa kijumla unaanza... Hii huko mexico na Venezuela inaeleweka Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…