CCM inatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu

CCM inatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu

Kumbe ya nini? Humu jf tunaombana namba acha ushamba?
Unapost mabandiko ya kipumbavu ya kichawa kusifia ujinga ili kuwapendezesha wenye mamlaka ya uteuzi lakini wamekuona pumbavu chawa usiyejitambua
Hasira ya Nini ndugu yangu,kwanini umejaza hasira na chuki kifua chako? Tuliza Akili yako
 
Utabaki chawa milele mngejua kwenye corridors of power wanavyowadharau nyie machawa msingeandika huu upuuzi mitandaoni Kuna mwenzako aina Yako sehemu Fulani alijitia anajulikana na watu wa usalama kisa uvccm akaenda kulishika lile limwenge lenu alipata kipigo Cha paka jizi na uchawa wake wa ki uvccm!
 
Umeamua kujitoa ufahamu , hivi ikiwepo tume huru ccm mnauwezo wa kushinda uchaguzi wowote , uchaguzi 2020 walimu walilazimishwa kupiga kula baada ya kupeleka kura zilizopigwa kwa mkurugenzi kwa ahadi ya kupewa hela kama watashinda, leo unakuja na andiko la hovyo kabisa, au ndo kunyemelea teuzi kazana
 
Tizama hii kenge, chawa ni mmoja wa maadui wakubwa wa nchi hii,
Na namba unaweka ili wa kuone kabisa..
Unasifia visivyosafishika.

Uchawa na uchoko vimetenganishwa na kauzi kadunchu tu.

Mwaka wa 60+ toka tupate uhuru kila siku ni afadhali ya jana, gharama za maisha zinapanda tu, wakati mwingine bora mkae kimya kuficha upumbavu wenu, unaonekana mroho, ukipewa nafasi ndio utatumbua kweli.

Mengi magufuli naweza kumsamehe ila hili la "walamba makalio alituzingua mnoo" haya ni matokeo yake, diku hizi watanzania wanasifia sifia tu hata km ni ujinga, mradi asifie huenda akaonekana,akapata chochote kitu
 
Ndugu zangu watanzania,

Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kwa kujiamini na bila hofu yoyote ile kuwa CCM Inatosha Kuendelea Kuliongoza Taifa Letu Kama chama Tawala,kwa kuwa imeonyesha ushupavu ,umadhubuti ,uimara,ujasiri ,uhodari ,uzalendo ,umakini,utayari na mikakati Bora katika kuwahudumia na kuwatumikia watanzania.

CCM ndio chama pekee kilichoonyesha na kujiweka karibu na wananchi, kuwasikiliza na kuwapatia majibu ya maswali Yao, Ni CCM pekee iliyoonyesha usikivu kwa sauti za makundi yote katika jamii,Ni CCM pekee iliyoonyesha kuwa na uchungu na maisha ya watanzania,Ni CCM pekee hapa nchini yenye kujuwa Mahitaji ya watanzania na kuyapatia kipaombele,Ni CCM pekee yenye kubeba Sera na ajenda za kugusa maisha ya watanzania.

Ndio sababu ya kuwa chaguo la watanzania kila uchaguzi,ndio sababu ya kupigiwa kura na kupita kwa kishindooo katika kila uchaguzi,ndio sababu ya Kuendelea kuaminika na kupendwa na mamillion ya watanzania,ndio sababu ya kuwa na wanachama wengi kuliko chama chochote kile hapa nchini,ndio sababu ya kuwa na uwezo ya kupenyeza mikono yake kwa vyama vyote nchini,ndio sababu ya kuwa na ushawishi katika mioyo ya watanzania.

Ndio sababu ya kuyateka makundi yote hapa nchini,ndio sababu ya vikao vyake kuteka mijadala ya kisiasa hapa nchini ,ndio sababu watanzania kujenga Imani kubwa kwa CCM na viongozi wake,ndio sababu kuwa chuo Cha malezi ya uongozi na viongozi wa Leo na kesho kwa Taifa letu,ndio sababu ya ofisi zake kuwa Tumaini la wanyonge na waliokata Tamaa au kuonewa au kudhurumiwa haki mahali popote pale, ndio sababu Hakuna Jambo lolote au ajenda au Sera au hoja au sheria au mswaada unaoweza kupita au kukubalika ikiwa CCM na wanaccm hawajaridhia na kukubali kutoa baraka zao.

Kwa hakika ni CCM pekee iwezayo kuliongoza Taifa letu na Ni CCM pekee ambapo Taifa letu linakuwa katika mikono salama, ndio maana huwezi ukakuta Wala kuona Wala kusikia kauli za kuhatarisha usalama wa Taifa letu zikitoka katika vinywa vya viongozi wa CCm, maana wanajuwa dhamana kubwa waliyo nayo ya jasho ,machozi na Damu katika kuhakikisha Taifa letu linakuwa salama muda wote.

Wakati ni kawaida kusikia kauli za ajabu ajabu zilizokosa uzalendo za kuhamasisha uvunjifu wa amani na machafuko hapa nchini kutoka katika vinywa na midomo ya viongozi wa upinzani. Ni Rahisi kusikia kiongozi wa upinzani akiwa jukwaani akitamka kuwa nchii hii haitatawalika au Moto utawaka au hapatakalika hapa nchini au akitamani umwagikaji wa Damu utokee hapa nchini ili yeye na chama chake wapate madaraka.

Hayo yanatokea na kusikika kutoka upinzani kwa kuwa hawana uchungu Wala uzalendo na Taifa letu, wao na familia zao mawazo yao ni juu ya matumbo Yao na maslahi yao binafsi, hawawazi juu ya watanzania wanyonge wasioweza kupeleka watoto wao marekani na ulaya ,hawawazi juu ya wajane na yatima, hawawazi juu ya wazee na akina mama,wao wapinzani hayo hayawahusu Wala hawana habari nayo ndio maana Dua zao na maombi Yao wakati wote ni hasi, ndio maana hata watoto wao uraia wao Ni wa marekani na ulaya na hivyo kukosa uzalendo na moyo wa kulipenda kwa dhati Taifa letu.

Ndio maana nasema kuwa CCM Inatosha na inastahili Kuendelea Kuliongoza Taifa Letu kwa kuwa inajuwa uzito wa kiapo ilichoapa katika kulilinda, kulipigania na kulitetea Taifa letu,viapo hivi vizito na vya kutetemesha na vya kujenga uzalendo ndani ya moyo viongozi wa upinzani hawana na hawajawahi kuapa popote na hawajuwi uzito wake Wala umuhimu wake juu ya maisha ya watanzania na mstakabali waTaifa letu.

CCM Itaendelea kuwa chama kiongozi , Tegemeo la watanzania, Tumaini la watanzania, mfano wa kuigwa, suluhisho la kero na changamoto, mboni ya watanzania,jicho la Taifa letu maana ikizima CCM ni sawa na kuzima kwa Taa ya Taifa jambo litakaloleta Giza kwa Taifa na kuitetemesha nchi na Taifa, hakuna mtanzania mwenye akili Timamu ambaye atataka Hilo litokee kwa kuitoa CCM madarakani.

Ni lazima CCM ilindwe kwa nguvu zote na watanzania wazalendo Kusalia madarakani, na tayari Watanzania Wameonyesha dhamira hiyo ya kuilinda CCM kwa nguvu zao zote kwa kuipigia Kura kila uchaguzi na kuiunga mkono serikali Yake, ndio maana huwezi ukasikia chochote kilichokibaya kikifanikiwa katika Taifa letu, maana watanzania hawapo Tayari na hawaji kujaribu wala kuthubutu kuvuruga amani ya Taifa letu kwa mikono yao wenyewe.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
CCM ina wenyewe boya wewe weka mpaka umri wako hapo utabaki na jembe lako la mkono.
 
Tizama hii kenge, chawa ni mmoja wa maadui wakubwa wa nchi hii,
Na namba unaweka ili wa kuone kabisa..
Unasifia visivyosafishika.

Uchawa na uchoko vimetenganishwa na kauzi kadunchu tu.

Mwaka wa 60+ toka tupate uhuru kila siku ni afadhali ya jana, gharama za maisha zinapanda tu, wakati mwingine bora mkae kimya kuficha upumbavu wenu, unaonekana mroho, ukipewa nafasi ndio utatumbua kweli.

Mengi magufuli naweza kumsamehe ila hili la "walamba makalio alituzingua mnoo" haya ni matokeo yake, diku hizi watanzania wanasifia sifia tu hata km ni ujinga, mradi asifie huenda akaonekana,akapata chochote kitu
Tanzania chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa CCm imepiga hatua kubwa Sana za kiuchumi na kimaendeleo mpaka kufikia uchumi wa Kati, watanzania tuna kila sababu ya Kuendelea kuiunga mkono serikali ya CCM na kuiamini maana tulikotoka Ni mbali Sana kama Taifa mpaka kufika hapa tulipo
 
Umeamua kujitoa ufahamu , hivi ikiwepo tume huru ccm mnauwezo wa kushinda uchaguzi wowote , uchaguzi 2020 walimu walilazimishwa kupiga kula baada ya kupeleka kura zilizopigwa kwa mkurugenzi kwa ahadi ya kupewa hela kama watashinda, leo unakuja na andiko la hovyo kabisa, au ndo kunyemelea teuzi kazana
Hata ije tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itashinda kwa kishindo kwa kuwa Ina Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania ,ndio sababu ya kukubalika na kupendwa na mamillion ya watanzania na Kuendelea kupigiwa kura na kuchaguliwa kila uchaguzi
 
Back
Top Bottom