Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,454
- 34,475
Tangu tukio la kujiuzulu Makamu wa Rais marehemu Abdu Jumbe (RIP) vyeo vyake vote ndani ya serikali na chama. likaja tukio la G55 ambapo wabunge 55 wa CCM waliungana kusimamia hoja ya serikali 3 Bungeni ambapo chama kilivuka salama chini ya Mwalimu Nyerere. Kipindi alichojitoa Augustine Mrema kwenda Upinzani ilikuwa heka heka hadi ikamlazimu Baba wa Taifa azunguke nchi nzima kumdani Mr. Clean kwenye Uchaguzi Mkuu 1995.
Ugumu ama mtikisiko uliorekodiwa kuwa na ritcher 8.2 ulitokana na Waziri Mkuu aliyestaafu kwa tuhuma za ufisadi almaarufu mzee wa Monduli alipovuka mstari kutoka CCM kwenda UKAWA baada ya jina lake kukatwa kwenye hatua za awali za kinyang'anyiro cha kura za maoni nafasi ya urais. Hili la mtikisiko lilitolewa maelezo na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mzee JK lakini alikiri walipita salama ingawa hofu ilizidi kiwango.
Naam Chama kilivuka salama tetemeko hilo la 2015 na sasa kuna tatizo jipya limejitokeza. kuna nyufa zinazoonekana usoni ambapo kunaashiria Lava inatokota kutafuta upenyo wa kupasua na kulipuka ili iweze kupoa. Nyufa hizi hazijajitokeza kwa sababu ya ukavu wa uso bali mtikisiko utokanao na nguvu za asili kukinzana huko ndani. Suala la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kufufua upya vita dhidi ya wahusika wa dawa za kulevya ni jambo ambmalo lilipokelewa kwa fikra chanya na jamii hususani wanaoelewa ama kuishi katika madhara yatokanayo na dawa hizi za kulevya. kikajitokeza kikundi kidogo cha waliojificha nyuso zao wakaanza kupambana kuhakikisha vita hii inapata mushkeli. lakini cha ajabu kabisa ni kwamba tetesi nyingi zilivuma bila mambo kuwekwa sawa na hatimaye jamii ikapokea mwangwi wa tetesi hizo kwa kiasi kikubwa. Suala la vyeti, Ukwasi na haiba ya Mkuu wa Mkoa vilikuwa katika ndimi za jamii chini ya uratibu wa hao waliotaka iwe hivyo.
Baada ya mkutano mkuu wa CCM hivi karibuni kungebadilisha suala la vyeti vya shule ya Mkuu wa Mkoa wa Dar na kuingiza single mpya sokoni ya wanachama nguli kuvuliwa uanachama wa CCM kwa kosa la usaliti. Badala yake mkuu huyo wa mkoa alibeba dumu la petroli na kukimbilia kuzima moto wa vyeti kwa style ya kashfa kujibiwa na kashfa.
Tayari leo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda biashara amejiuzulu na makamu wake. ukisikiliza maelezo yao utagundua kuna tatizo kubwa ndani ya magma. Baadhi ya wabunge na hata viongozi wa serikali na jamii wamejitokeza kupaza sauti zao dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa maadili ya uongozi uliofanywa na RC wa Dar kwa kuvamia kituo cha redio Clouds akiwa na askari wenye silaha....
Ongezeko la gharama za maisha unaochangiwa na mamlaka za serikali zinazosimamia na kuratibu inflation ya bidhaa ghafi kama vile mafuta na umeme ni wazi hisia za wananchi dhidi ya serikali yao zinazidi kuongezeka.
Matukio haya yanayojiri sasa ni pigo jipya kwa CCM ambapo majeraha yake yatachukua muda mrefu sana kujitibu na hata kupunguza morali ya makada wake kuwa waaminifu wa dhati kwa chama inapokaribia uchaguzi.
Na haya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambapo Nape kuenguliwa ni wazi magma inakaribia kufika uso wa ardhi ili isambae na kupoa.... Nape alitangaza kutaka kujiuzulu na kilichotokea amewekwa pembeni haraka kabla hajafikia huko.
CCM inapita katika nyakati ngumu kabisa kwa wakati huu na inahitajika akiliya ziada kuvuka salama.