CCM inapambana na kifo (Damage control) wananchi msiisadie kulia!!

Lusungo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
29,517
Reaction score
42,653
Tangu kumalizika kwa uchaguzi wa ndani 2015 CCM imekua ikipambana na kifo chake kwa gharama kubwa!!

Kilichotokea Dodoma 2015 kilikua mwanzo wa mwisho wa CCM Chama pekee kikongwe kwa East Africa na Kati.

Wengi wetu huwa tunatazama sana matukio badala ya issues. Wanaotazama matukio hawawezi ona jinsi CCM inapambana na kifo chake isipokua kwa wenye macho na uwezo wa kujionea issues.

Baada ya mchakato wa hila...ghilba na chuki kubwa wa kumpata mgombea urais wa CCM pale Dodoma wengi wenye akili na maono ndani ya Chama walionya sana juu ya mbegu ya mauti inayopandikizwa lakini kama ilivyo desturi ya kukata roho watu walishupaza shingo...

Kwa sasa Rais Magufuli ana upinzani mzito ndani ya CCM kuliko Marais wote waliopita ndani ya CCM!!

Rais Magufuli ameonesha ishara zote ambazo CCM kwa miaka mingi imekua ikiziogopa sana kwa wagombea wake hivyo aliaminiwa Magufuli kwa kigezo cha unyenyekevu lkn hali imekua tofauti sasa CCM inawaka moto!!

Kwa mlio na jicho la tatu na muonayo ya sirini mtakumbuka hofu kuu iliyoifanya CCM kumwondoa Lowassa haikua ufisadi bali udikteta... na kilichompora Lowassa uwaziri mkuu hakikua ufisadi kwa mujibu wa CCM bali mkono wake wa chuma!! Sasa ikaonekana heri C kuliko A na B lakini kilichotokea kila mtu hana hamu ndani ya CCM..

Kundi kubwa likiongozwa na katibu mkuu wa CCM limenuna!! Kundi kubwa halina raha wala furaha!!

Kuna kundi kubwa sana la wabunge na mawaziri lilipanga kuondoka CCM na Nyalandu lkn wakapima upepo kwanza then wasambae...

Kuna fukuto zito juu ya uchaguzi wa 2020 ndani ya CCM na mwenyekiti ameziona cheche zake hivyo hiki kinachoendelea ni kutafuta kujiponya.

Kwa mara ya kwanza CCM haifanyi tena siasa badala yake imekabidhi jukumu hilo kwa Dola!!

Zamani ushindi wa CCM ulikua ukipangwa kwenye vikao vya chama na wakereketwa sasa ni tofauti!! Ushindi sasa unapangwa serikalini.

Hivyo hii nunua nunua ya wapinzani msifikiri CCM inapambana na wapinzani wa vyama big No!! CCM inapambana na upinzani wa ndani ambao ndio kifo na kaburi lake.

Historia ni mwalimu mzuri na muda ni hakimu wa yote.
 
Mkuu sana lusungo, respect sana kwa ukweli huu. Hawa vijana waliomwagwa humu jf kwa kazi ya kuponda na kukandia ukweli ni njaa zao zinawasukuma kwani mbwa akiwa na kipande cha mkate habweki! Ajira walizotarajia badala ya kupewa, wanaahidiwa!
Ukweli ni kuwa sisi tuliopo kitaa tunasisikia sana kauli hizi na ushahidi upo wazi. Pita mitaani kama utaziona tena zile bendera za ccm na hata yale mashina ya wakereketwa wa ccm yamafutika! Ile mikutano ya ccm mitaani haipo tena!
Jk alimwambia waziwazi kuwa chama ni wanachama but yeye anafikiri chama na polisi na vyombo vya dola! Kadanganyika kwelikweli kwa taarifa anazopewa na wakuu wa wilaya na mikoa kuhusu uhai wa wanachama! Laiti angaliijua nguvu na maana ya makamanda aliowafutia vyeo vyao ambavyo havikuwa na posho wala mshahara angejilaumu sana kwa uamuzi wake ule!
Kawakosa washawishi kwa ubabe wake na lililobaki na anguko kuu kama lile la kanu! Wacha ccm ife kabisa na isifufuke tena kama kanu!
 
ukweli mchungu ccm inaendelea kupumua kwa msaada wa polisi
 
CCM imechokwa nchi nzima.kwa sasa iatafuta wanachama wa kukodi
 
Ngoja niendelee kuomba pumzi zaidi nione maajabu zaidi
 
Mkuu sana lusungo, respect sana kwa ukweli huu. Hawa vijana waliomwagwa humu jf kwa kazi ya kuponda na kukandia ukweli ni njaa zao zinawasukuma kwani mbwa akiwa na kipande cha mkate habweki! Ajira walizotarajia badala ya kupewa, wanaahidiwa!
Ukweli ni kuwa sisi tuliopo kitaa tunasisikia sana kauli hizi na ushahidi upo wazi. Pita mitaani kama utaziona tena zile bendera za ccm na hata yale mashina ya wakereketwa wa ccm yamafutika! Ile mikutano ya ccm mitaani haipo tena!
Jk alimwambia waziwazi kuwa chama ni wanachama but yeye anafikiri chama na polisi na vyombo vya dola! Kadanganyika kwelikweli kwa taarifa anazopewa na wakuu wa wilaya na mikoa kuhusu uhai wa wanachama! Laiti angaliijua nguvu na maana ya makamanda aliowafutia vyeo vyao ambavyo havikuwa na posho wala mshahara angejilaumu sana kwa uamuzi wake ule!
Kawakosa washawishi kwa ubabe wake na lililobaki na anguko kuu kama lile la kanu! Wacha ccm ife kabisa na isifufuke tena kama kanu!
Mkuu ni suala la muda tu... haya maigizo yanayoendelea ni kujaribu kupooza uji unaotokota
 
Ushamba unaongoza nchi
Mtu anatumia psychomotor domain kuongoza badala ya cognitive.
 
Huu ni ukweli mtupu..chama kimepoteza dira..kimekufa kimeoza kinasubiri kuzikwa! sad!
 
Ee mwenyezi Mungu hata sasa nakuona ukitenda.
 
Back
Top Bottom