Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,621
- 6,511
Ukifanya tathmini ya kina kuhusu CCM utagundua hakuna jambo wanaloliogopa kama ajitokeze mtu mwenye nguvu ndani ya chama, aseme "mabadiliko ya mfumo wa kuendesha nchi hayakwepeki tena na ni lazima yafanyike".
Miaka ya mwanzo wa 1990s, Rais wa Urusi Mikhail Gorbachev, baada ya kuona mzigo wa Ukomunisti haubebeki tena, alilazimika kuanzisha mabadiliko makubwa ya kimfumo. Alipata upinzani mkubwa sana kutoka kwa wale waliotaka mfumo uendelee na baadae hadi kupinduliwa. Kutokana na upinzani alioupata, ndiyo ukawa mwanzo wa majimbo mbalimbali yaliyokuwa yanaunda USSR kuanza kumegekamegeka na kujitangazia uhuru.
Humphrey Polepole alitaka kujitokeza na kusimama kama 'Gorbachev', akatokewa mpaka sasa haijulikani alipo. Horace Kolimba, alikuwa Katibu Mkuu wa CCM aliibuka akasema CCM imepoteza dira na muelekeo, akaitwa kwenye kikao ajielezee, kesho yake tukatangaziwa hatupo naye tena.
Kikwete alitubeep kwa mchakato wa Katiba Mpya ingawa sina uhakika kama alikuwa na dhamira ya kweli maana ndiye Rais wa mwisho aliyekuwa na nguvu ndani ya CCM za kufanya haya mabadiliko bila kupoteza ushawishi wake ndani ya chama.
Ili kuzuia hilo lisitokee, wamebaki kuhakikisha wote waliomo ndani wanachafuana ili 'Gorbachev' asitokee miongoni mwao. Ukiwa mchafu ndiyo unaaminika zaidi maana ni rahisi kukucontrol kwa sababu uchafu wako ndiyo dhamana yako.
Ni ngumu sana kupata kiongozi, hasa mwenye mamlaka ya Urais ndani ya CCM hii atakayekubali au kuruhusiwa kufanya mabadiliko ambayo raia wa Tanzania wanayalilia na kuyadai. Kila anayejaribu au atakayejaribu atakumbushwa na kuulizwa "unataka wewe ukumbukwe kwa kukivunja chama na nchi?" Hii "push-back" tunayoona ikiwepo kilichotokea MO29 ni jitihada za kunyamazisha presha hii ya mabadiliko.
Kwa kuwa wanaijua vizuri historia, wanataka kutishia kuwa Tanzania itagawanyika na kupasuka iwapo mabadiliko hayo yatafanyika (tumeone wale Masheikh) ila ukweli ni kuwa wanalinda uhai wa chama chao na maslahi yao tu.
Kwa hapa tulipofikia, mabadiliko yakitokea na inaonyesha yatatokea kwa nguvu ya umma, cha kwanza kitakachoparaganyika ni CCM na itaanguka kwa kishindo kikuu. Wanataka kutengeneza mazingira kwa kujifungamanisha na hadi vyombo vya UnU ili ikiparaganyika, wote tuumie maana wananchi wataona wote kuanzia CCM na taasisi hizo zote ni wabaya.
Inahitaji busara kubwa kutoka nje kututoa hapa tulipo, bila hivyo hatutoboi.