'CCM inanadi sura badala ya maendeleo' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'CCM inanadi sura badala ya maendeleo'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sijafulia, Mar 27, 2010.

 1. s

  sijafulia Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewashambulia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwashutumu kwa kuwavalisha Watanzania fulana za kunadi sura za viongozi wake, badala ya maendeleo kama walivyoahidi wakati wakitafuta ridhaa ya kuongoza nchi.
  Hayo yalisemwa na mwenyekiti mpya wa chama hicho mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, alipokuwa akitambulisha safu mpya ya viongozi wa mkoa waliochaguliwa hivi karibuni.
  Alisema CCM kwa makusudi imeshindwa kutekeleza sera zake zilizoandikwa na kupangiliwa vizuri vitabuni na kuwasababishia Watanzania kuishi maisha magumu.
  “Nawaambia wenzetu hawa ni mafundi wa midomoni, lakini utekelezaji ni kitendawili hivyo sisi CHADEMA tumeiona hali hiyo na kauli hizo siyo sahihi bali ni usaliti mtupu kwa Watanzania,” alisema Shitambala.
  Shitambala alisema ugumu wa maisha unaowakabili wananchi ni fundisho kwamba wasiendelee kuing’ang’ania CCM ambayo kimsingi haina mpango wa kuwaletea maendeleo na badala yake viongozi wa chama hicho wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kujilimbikizia mali.
  Shitambala alisema mfano ni viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kulumbana kwenye siasa badala ya kushughulikia masuala ya maendeleo ya wananchi.
  ‘’Kwa ujumla hali ya kimaendeleo mkoa huu imegubikwa na kelele za ushindani wa siasa, lakini wazalendo wenzangu pamoja na fursa zote zilizoshushwa na Mungu kama mipaka ya nchi mbili ya Zambia na Malawi na ardhi, watu wenye nguvu na bidii, madini, makaa ya mawe, Ziwa Nyasa, misitu na rasilimali nyingi lakini viongozi wenye dhamana katika mkoa huu ni mabingwa wa propaganda.’’  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewashambulia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwashutumu kwa kuwavalisha Watanzania fulana za kunadi sura za viongozi wake, badala ya maendeleo kama walivyoahidi wakati wakitafuta ridhaa ya kuongoza nchi.

  Hayo yalisemwa na mwenyekiti mpya wa chama hicho mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, alipokuwa akitambulisha safu mpya ya viongozi wa mkoa waliochaguliwa hivi karibuni.
  Alisema CCM kwa makusudi imeshindwa kutekeleza sera zake zilizoandikwa na kupangiliwa vizuri vitabuni na kuwasababishia Watanzania kuishi maisha magumu.
  “Nawaambia wenzetu hawa ni mafundi wa midomoni, lakini utekelezaji ni kitendawili hivyo sisi CHADEMA tumeiona hali hiyo na kauli hizo siyo sahihi bali ni usaliti mtupu kwa Watanzania,” alisema Shitambala.
  Shitambala alisema ugumu wa maisha unaowakabili wananchi ni fundisho kwamba wasiendelee kuing’ang’ania CCM ambayo kimsingi haina mpango wa kuwaletea maendeleo na badala yake viongozi wa chama hicho wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kujilimbikizia mali.
  Shitambala alisema mfano ni viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kulumbana kwenye siasa badala ya kushughulikia masuala ya maendeleo ya wananchi. ‘’Kwa ujumla hali ya kimaendeleo mkoa huu imegubikwa na kelele za ushindani wa siasa, lakini wazalendo wenzangu pamoja na fursa zote zilizoshushwa na Mungu kama mipaka ya nchi mbili ya Zambia na Malawi na ardhi, watu wenye nguvu na bidii, madini, makaa ya mawe, Ziwa Nyasa, misitu na rasilimali nyingi lakini viongozi wenye dhamana katika mkoa huu ni mabingwa wa propaganda.’’

  Source
  http://freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=14377
   
Loading...