tubadilike-sasa
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 681
- 167
Hapo zamaNI CCM ilikuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi. Kilikuwa ni mali ya hawa wawili,wakulima na wafanyakazi.Na ukisoma historia na ukawafanisha viongozi wa wakati ule na walichohubiri majukwaani,kwenye mikutano na hata kwenye majarida mbalimbali unasema naam! Hii sawa. Na viongozi walifanana alau kwa asilimia kubwa na kile walichokisema au na wale waliokuwa wanaambiwa. Na hivyo bila maandishi wakawa na hati miliki katika nyoyo zao ya kuwa CCM ni mali yao. Hivyo kabla ya mambo kubadilika,wakulima na wafanya kazi ndio walikuwa wamiliki wa CCM na Serikali ya CCM.
Je kwa mambo yalivyo leo hii na vituko tunavyoshuhudia bado CCM na Serikali yake ni mali ya Wakulima na Wafanyakazi? Jibu ni hapana. Hii ni kwa sababu tabia na haiba ya CCM vimebadilika sana. Nitatoa mifano michache tu kuainisha mabadiliko ya tabia ya CCM. CCM ninayoijuwa haikuwa ni chama ambacho mwandishi wa habari anauawa mikononi mwa polisi halafu kinakaa kimya bila kukemea na bila kujali mhusika ni nani. CCM haikuwa ni chama ambacho kingeshindwa kukemea kauli nzito ya Waziri mwandamizi na aliye katika ofisi ya Rais wa Jamhuri wa muungano kuwa " watahakikisha wanaisambaratisha CHADEMA ndani ya mwaka mmoja" Hii ni kauli nzito sana katika mazingira tuliyonayo sasa. CCM haikuwa chama ambacho unatoa vijisenti halafu unapigiwa kura na baada ya kupigiwa kura unafanya utakavyo. Sasa swali ni je CCM inamilikiwa na nani?
Kwa haraharaka hivi sasa CCM na Serikali yake vina mmiliki mmoja tu. Jina la huyo mmiliki ni mfumo-fisadi(corrupt system). Mfumo huu unamiliki maeneo yote nyeti,kuanzia CCM kada mbalimbali, Ikulu, mashirika ya uma yote, mawizarani, JWTZ,Polisi,Usalama wa Taifa, nk. Umeenea na kuota mizizi kiasi kwamba kuung'oa lazima ujiandae kufa. Huu ndio umekuwa mfumo rasmi(usio wa kiofisi) katika CCM na Serikali yake. Na sasa umehitimu na kuwa na meno makali yanayong'ata kila anayejaribu mambo ambayo yanakwenda kinyume na mfumo huu. Mfano dhana ya kujivua gamba iliyoanzisha kwa tambo nyingi na akina Mukama na Nape ilishindwa kwa sababu ya mfumo huu. Wao kwa uwezo wao mdogo wa tafakuri hawakuweza kuligundua hili mapema kwa kuwa mbwembwe zilitangulia fikra zao na hivyo kushindwa kuona umauti wa dhana ya kujivua gamba.Pengine hii ni kwa sababu walidhani bado CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi,wapi! Chama kishapata mmiliki mwigine. Niliwahi kumsikia Katibu Mkuu wa CCM jukwaani akisema" CCM bado chama kinachooendasha siasa ya Ujamaa na kujitegemea na bado chama cha wakulima an wafanyakazi. Mimi nikaguna!
Mfumo-fisadi umejipanga vyema na kila unapotishiwa lazima ung'ate na ukinga'ta ni maumivu makali kama ya Dr. Ulimboka au kifo kama cha Mwangosi.Na hii Movement for Change(M4C) ya CHADEMA inatishia mfumo huu,inasukuma mizizi ya mfumo wakati mfumo hautaki kuguswa na pia una dola na nguvu nyingi. Na inabidi CHADEMA wajizatiti kwelikweli maana mfumo umetikiswa,una kizunguzungu na sasa upo tayari kwa lolote-kucheza faulu, kusingizia, kusema uongo,kuchonganisha, kusingizia, kuchafua hali ya hewa, kutumia fedha, kuteka,kutesa,kung'ata,kuuwa nk,. Waingereza wanasema "If you rattle a snake you must be prepared to be beaten".
Hata hivyo nashangaa kuona watu wengi wakishangaa haya mauaji yanayotokea kama ya mwandishi,kule Morogoro,Arusha,Bulyankulu, Tarime nk.Eti hii siyo staarabu ya Watanzania. Mimi nawashangaa tu. Watu wanatakiwa washingae kwa sababu CCM na Serikali si mali yetu tena. Ina mmiliki mwingine na jina lake ni mfumo-fisadi ambao ni mfumo dhalimu kwa maana asili,hurka na mambo yatendwayo na mfumo huu. Ni kweli kuwa sura zilizopo kwenye mfumo huu ni za kiaafriaka haswa,pengine za asili ya kiasia na kiarabu kidogo. Wanazunguza kiswahili kama sisi,wanaweza wakawa ni baba zetu,wanetu,shangazi zetu,wajomba zetu, nk lakini ni mfumo.
Haya mauaji yanayotokea kwa sasa na ambayo yataendelea kutokea(Mungu tusaidie) ni matokeo ya mfumo-fisadi (corrupt system)kujilinda na wale wanaopinga uwepo wa mfumo huu.
Vifo au maafa mengine yataendelea kutokea hadi pale ambapo ama kundi moja kati ya haya mawili litashindwa,ama kundi mmojawapo kujawa na busara ya isiyoelezeka.
Kimsingi mapigano ya kati ya makundi haya mawili ni athari ilyotoka na CCM kubadilisha umiliki wa siasa zake toka mmiliki wa awali ambaye alikuwa ni Wakulima na Wafanyakazi kwenda kwa mmiliki wa sasa ambaye ni mfumo-fisadi (corrupt system). Na kusema kweli huyu mmiliki wa sasa ana sifa zote za ubeberu.