CCM inafurahia udhaifu wa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM inafurahia udhaifu wa watanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masauni, Sep 19, 2010.

 1. M

  Masauni JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimemesoma kwa masikitiko makubwa kuwa wananchi wa monduli wataendelea kumchagua lowasa kwa sababu amewaletea maendeleo makubwa katika jimbo lake. Kwa mtazamo wangu naona hii inaonyesha jinsi watanzania tusivyojali umoja na uzalendo wetu wa kuipenda tanzania. Pia niliwahi kusema katika moja ya post zangu kuwa tatizo kubwa ninaloliona tanzania ni 'ubinafsi(umimi)'. wamasai wameshindwa kuona hasara aliyoleta lowasa kwa taifa? wao wanachoona amewafanyia nini watu wa jimbo lake, Basil mramba ufisadi uko wazi kabisa lakini watu wa Rombo wameshindwa kuona hasara aliyoileta kwa taifa bali wanachojali ni nini amekifanya Rombo. Kwa rostam aziz hasara aliyoleta kwa taifa letu iko wazi kabisa, lakini watu wa jimbo lake hiyo hasara ya taifa haiwahusu? ,kinachowahusu ni amefanya nini katika jimbo lake! TABIA HII YA WATANZANIA NDO INAWAPA OPPORTUNITY VIONGOZI KUFUJA MALI YA UMMA NA KUFANYA WATAKAVYO (katiba pia ina changia) kwa sababu wanajua udhaifu wetu. na wakirundi majimboni mwao wanaweka mambo sawa. WATANZANIA HIKI NI KIPINDI CHA KULIKOMBOA TAIFA
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wala Lowasa na Mramba hawajawaletea watu wao mendeleo ya kustahili kupongezwa. Wizi wa mali ya umma waliofanya walijinufaisha wao wenyewe. Ni mtazamo finyu tu wananchi wa Monduli na Rombo unaofanya waendelee kuwapa hao nafasi tena.

  Hivi umeenda Mondoli ukaona mahekalu ya Lowasa pale Monduli juu? Ni nyumba za kulala wageni. Amechukua eneo kubwa karibu na benki nmb, nadhani hata ameibana nmb. Kwa hakika eneo lile amejipatia kwa kutumia nafasi yake aliyokuwa nayo, ama akiwa waziri wa ardhi au akiwa katika nafasi nyingine ya juu serikalini.

  Sipingani na maendeleo ya mtu yoyote, ila nasema Lowasa ni mbinafsi. Alijifaa mwenyewe kuliko alivyowafaa wana Monduli ambao ndio wanaompigia makofi miaka yote abaki bungeni.

  Lakini najiuliza, hivi hakuna wamasai wengine waliosoma huko Monduli?
   
 3. fige

  fige JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa mkuu hilo limekuwa jambo la kawaida kwa watz kwaenzi mafisadi na kuwaponda kwa mawe wadokozi.
  Nchi hii ukiwa na madraka ukawa chwee watu wanakucheka ,unaonekana mzembe na kilaza.
  Watz tuamke tusiponde mawe vibaka tu
   
 4. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Masauini hivi hujuagi kuwa hili linchi limerogwa siju na nani Tobah!! Wadanganyika oyee!!
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Sep 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Si mliambiwa ilikuwa ni "ajali ya kisiasa?" Ohoo, endeleeni kuchokonoa mtaambiwa ni "wavivu wa kufikiri!"
   
 6. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,453
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Udhaifu hupo sio tu kwa wana Monduli jikumbushe miaka ya nyuma wakati wa chama kimmoja tulivyochangia kujenga viwanja vikubwa vya mipira kama CCM Kirumba na viwanja vikubwa vya michezo mbali mbali,majumba na miradi mbalimbali nchi nzima tukilazimishwa na kukatwa mishahara,kukatwa mapato kwenye mazao yetu kupitia vyama vya ushirika,kutumia vijana wa JKT kujenga maofisi na nyumba mbali mbali ya chama kwa kujitolea tukiamini hii ni mali yetu sote.Lakini baada ya kuruhusiwa nchi kuwa na vyama vingi mali zote za CCM zikabakia CCM badala ya kuwa mali ya serikali.Upumbavu kama huo jirani zetu Kenya waliukataa. KANU ilidai Kenyatta conference center ni mali yao lakini serikali ya NARC ilivyoiangusha KANU ikarudishwa serikalini.
   
Loading...