Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,641
- 22,240
Kwa kawaida timu ya mpira huwa na wachezaji kumi na moja ndani ya uwanja, hata hivyo huruhusiwa kubadilisha mchezaji endapo watahitaji na bado timu itakuwa na idadi ileile kumi na moja kwani yule wa akiba hatahesabika wa kumi na mbili.
Mgombea urais huteua mgombea mwenza na bado inahesabika mgombea ni mmoja kwa kila chama, inapotokea kama ilivyotokea ila kabla ya mgombea husika kushinda urais basi mgombea mwenza hupoteza nafasi.
Sasa mgombea ameshinda labda kwa bahati mbaya amedumu ofisini kwa wiki moja tu na nafasi yake kuchukuliwa na mgombea mwenza kwanini huyu mwingine tuambiwe ana awamu yake wakati hatukumpigia kura na siyo anaendeleza awamu aliyoianza mwenzake.
Swali langu CCM inafaidika nini kwenye hili.