CCM haikosi usingizi kwa harakati za ACT na CHADEMA, ila nadhani itatikisika kwa hoja zao zaidi zinazolenga kuonesha na kutatua shida za wananchi. CCM ijiandae kupoteza kura kwa makundi yafuatayo km haitakua na majibu.
(1) Kundi la watumishi wa umma; kundi hili lina hasira ya kutoongezewa mishahara, kurefushiwa muda wa kupanda madaraja na majibu ya kejeli kuwa km unaona mshahara mdogo, acha kazi, kuonekana matajiri na watoto wao kutopata mikopo elimu ya juu, kuwaondoa watoto wao kwenye bima za afya wangali wapo vyuoni.
(2) Kundi la wanafunzi wa vyuo. Kundi hili linaumizwa kwa kukosa mikopo na hata wale waliopata mikopo wanatakiwa kulipa riba zaidi ya 80%. yaani ktk kila TZS 100 ulizokopa, utalipa TZS 180. bora ungekopa benki.
(3)Kundi la vijana, kundi hili lina hasira ya kutoweza kuajiriwa na kujiajiri. Ndio kundi hatari zaidi na lenye hasira kuu. Kundi hili halisikilizi execuses, halina uvumilivu. Huwezi kujitetea kuwa unanunua ndege kwanza, wenyewe wanataka kufanya kazi na kupata fedha.
HIVYO, makundi yote niliyoyataja ukiongeza na la wafanyabiashara wana uwezo ku influence wapiga kura wengine. unaweza kuona CCM inakosa usingizi maeneo gani.
CCM waombe wapinzani wasitembee na hizo hoja pia waombe Membe na Lissu wagombee ili wagawanyishe kura, vinginevyo, uchaguzi utakua mgumu mno kwa CCM kuliko ule wa 2015.
CCM ikiwa na majibu mujarrab kwa makundi hayo, itakua na uhakika wa ushindi.