Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,400
- 38,683
John Mnyika aliposema Bungeni kwamba Serikali imekuwa dhaifu kwa kuwa inaongozwa na mtu dhaifu wana CCM kariba ya kina January Makamba na wenzake kina Livingstone Lusinde walihanikiza kwamba Mnyika kamkosea adabu aliyekuwa Rais wakati ule.
Leo hao hao kina Makamba na wenzake ndiyo wako mstari wa mbele kuonesha kwamba serikali iliyopita iliendeshwa kwa kuoneana aibu na kuleana!! Kwa maneno mengine wanakiri kwamba Kikwete alikuwa dhaifu na serikali iliyokuwa inasimamiwa na yeye pia ilikuwa dhaifu. Kiungwana wanatakiwa wamuombe radhi Mnyika kwamba alikuwa sahihi aliposema kwamba Kikwete ni dhaifu na serikali aliyokuwa anaiongoza ni dhaifu!!